Na Wellu Mtaki, Geita Kampuni ya Yetu Motors imewataka Watanzania wanaopanga kuagiza magari kupitia mitandao kuwa makini na gharama na changamoto zinazoweza kujitokeza wakati wa mchakato wa ununuzi na usafirishaji wa magari kutoka nje ya nchi. Yetu Motors imesema kuagiza gari mwenyewe kupitia mitandao si jambo baya, lakini mteja anapaswa kufahamu kuwa anapochagua kufanya hivyo, anakuwa na wajibu wa kushughulikia changamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza katika mchakato huo. Kwa mujibu wa kampuni hiyo, miongoni mwa changamoto zinazoweza kujitokeza ni mabadiliko ya gharama wakati wa mchakato wa uagizaji na usafirishaji, ambapo gharama ambazo mteja alizikadiria wakati wa kununua gari zinaweza kuongezeka kutokana na sababu mbalimbali. Yetu Motors imesema tofauti na mteja anayeagiza gari mwenyewe, kampuni hiyo inabeba wajibu wa kushughulikia changamoto zinazoweza kujitokeza katika mchakato wa usafirishaji wa gari hadi kumfikia mteja. Aidha, kampuni hiyo imeeleza kuwa changamoto nying...
Marato tv - Sauti ya Jamii