Skip to main content

Posts

Showing posts from March 31, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mkuu Ashiriki Swala ya Eid, Ruangwa

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Machi 31, 2025 amejumuika na waumini wa dini ya kiislam katika Swala ya Eid iliyofanyika kiwilaya kwenye Mtaa wa Maghalani, Ruangwa Mkoani Lindi. Akizungumza baada ya swala hiyo, Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa waumini hao na Watanzania kwa ujumla kuliombea Taifa, viongozi wake pamoja na kudumisha amani, umoja na mshikamano. Katika Swala hiyo pia Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Telack alishiriki.

Umuhimu wa Amani Wasisitizwa Swala ya Eid El Fitr na Dc Chikoka Msikiti Wa Ijumaa Musoma

Na Shomari Binda-Musoma  MKUU wa Wilaya ÿa Musoma Juma Chikoka amezungumzia suala la umuhimu wa amani na jamii kushirikiana. Kauli hiyo ameitoa leo machi 31,2025 kwenye Msikiti mkuu wa Ijumaa mjini Musoma baada ya kumalizika kwa swala ya Eid. Amesema suala la amani lina umuhimu mkubwa kwenye taifa na kuwaomba waumini ya Dini ya Kiislam kuendelea kuiombea amani ya nchi wakati wote. Chikoka amesema amani na upendo ambao umekuwepo kwenye kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhan inapaswa kuendelea katika kipindi cha miezi mingine. Amesema katika kipindi cha mfungo unyenyekevu ulikuwa mkubwa kwa waumini na kudai yale yaliyokuwa takihubiliwa na ma Sheikh misikitini yanapaswa kuzingatiwa kwa kipindi chote. " Tupo kwenye sherehe ya Eid baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa waumini wa Dini ya Kiislam. " Amani na upendo tulioishi nao kwenye kipindi hicho tunapaswa kuuendeleza kwani pasipo amani hakuna jambo lolote linaloweza fanyika",amesema. Katika swala h...