Skip to main content

Posts

Showing posts from January 12, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Balozi Dkt. Nchimbi akutana na Mzee Mangula

   KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, akiambatana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Ndugu John Mongella, amemtembelea kwa ajili ya kumsabahi na kumjulia hali Mzee Philip Japhet Mangula, Makamu Mwenyekiti wa CCM Mstaafu (Bara), nyumbani kwake Msalato, Dodoma, leo Jumapili tarehe 12 Januari 2025.  Baada ya mazungumzo hayo yaliyofanyika kwenye maktaba ya Mzee Mangula, Balozi Nchimbi pia alipata wasaa wa kuchukua picha yeye mwenyewe kwa njia ya 'selfie', kama inavyoonekana pichani.

Rais Samia ashiriki Maadhimisho ya Miaka 61 ya Mapinduzi Zanzibar

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki maadhimisho ya kilele cha Miaka 61, ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yaliyofanyika katika uwanja wa Gombani, wilaya ya Chakechake, mkoa wa Kusini Pemba, Zanzibar leo tarehe 12 Januari, 2025. Mgeni Rasmi wa maadhimisho hayo alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Dkt. Biteko ashiriki Maadhimisho ya Miaka 61 ya Mapinduzi Zanzibar

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameshiriki katika Sherehe za Maadhimisho ya miaka 61 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yaliyofanyika katika Viwanja vya Gombani Kisiwani Pemba, Zanzibar. Mgeni wa heshima katika sherehe hizo alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Serikali ya Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi. Viongozi wengine wa Kitaifa waliohudhuria sherehe hizo ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Phillip Mpango, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman, Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla pamoja na viongozi wengine wastaafu wa Serikali zote mbili.

Rais Mwinyi akagua Gwaride la Mwisho ya Mapinduzi Kabla ya Uchaguzi Mkuu

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwasili katika Uwanja wa Gombani, Mkoa wa Kusini Pemba kushiriki kilele cha Sherehe za kutimiza Miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar tarehe 12 Januari 2025. Rais Dk.Mwinyi amepokea Salamu ya Rais na kupigwa Mizinga 21 pia amekagua Gwaride maalum la Maadhimisho hayo. Aidha , Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan ameshiriki Maadhimisho hayo, pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali kitaifa kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,  Mabalozi wanaowakilisha Nchi zao nchini,  Vyombo vya Ulinzi na Usalama,  Viongozi wa Dini na Vyama vya Siasa na Wananchi kutoka Mikoa ya Unguja na Pemba.