Msajili wa vyama vya Siasa Tanzania, Jaji Francis Mutungi amesema hata kama kauli ya ‘No reform, no Election’ haijavunji sheria ya vyama vya siasa,lakini kamwe isitumike kama kichocheo cha kuvunja sheria za nchi na katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Amesema ofisi yangu inafuatia kwa karibu kauli kama hizo zinazotumiwa na baadhi ya vyama vya siasa katika kuvunja sheria na katiba ya nchi. Jaji, Mutungi amesema hayo wakati akizungumza na George Marato Tv huku akisisitiza kuwa hakuna chama cha siasa chenye uwezo wa kuzuia uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika badae mwaka huu 2025. Amesema katika mazungumzo yake na waandishi wahabari baada ya kushiriki warsha ya wadau wa kujadili namna ya kuzuia na kupambana na rushwa katika uchaguzi mkuu 2025,akiwaeleza wazi mazungumzo yake na vyama vya siasa ikiwemo Chadema kwamba ofisi yake hauwezi kuvumilia kauli zinazolenga kuvunja sheria za nchi. Tangu kumalizika kwa uchaguzi wa ndani, CHADEMA wamekuwa wakieleza kuwa, bila mabadiliko katik...
Marato tv - Sauti ya Jamii