▪️Atoa wito kwa nchi za Afrika kuimarisha ushirikiano wa kikanda, kuongeza thamani ya madini na kuharakisha utekelezaji wa Dira ya Madini ya Afrika. 📍Accra, Ghana Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Peter Mavunde, amezitaka nchi za Afrika kuacha kufanya kazi kwa kujitenga na badala yake kuunganisha nguvu katika usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za madini ili kukuza viwanda, ajira na uchumi wa bara hilo. Ameyasema hayo Oktoba 19 wakati akizungumza katika mjadala wa jopo la Mawaziri kutoka nchi za Tanzania, Nigeria na Liberia uliokuwa na mada isemayo “From Vision to Delivery: Making the African Mining Vision Work for Member States”,katika mkutano wa Kimataifa wa Mining in Motion unaofanyika kwasiku tatu kuanzia Oktoba 19 hadi 21, 2026 jijini Accra Ghana. Mhe. Mavunde alisema wakati umefika kwa nchi za Afrika kuweka pembeni tofauti zao na kushirikiana kutekeleza mikakati ya pamoja ya maendeleo ya Sekta ya Madini. Alisema Afrika ina zaidi ya asilimia 32 ya rasilimali za madini muhimu...
Marato tv - Sauti ya Jamii