Skip to main content

Posts

Showing posts from March 7, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Rea Yaendelea na Usambazaji wa Mitungi ya Gesi kwa Wananchi wa Wilaya Korogwe Mooani Tanga

📌Mitungi 26,040 kusambazwa kwa bei ya ruzuku mkoa wa Tanga 📌Mitungi 3,255 kusambazwa kwa bei ya ruzuku wilaya ya Korogwe 📌Majiko ya gesi ni nishati safi na salama ya kupikia yenye kutunza mazingira na rafiki kwa afya ya watumiaji  REA imeendelea na zoezi la usambazaji wa mitungi ya gesi ya kilo sita kwa bei ya ruzuku wilaya ya Korogwe.  Ukiwa ni muendelezo wa uhamasishaji na upatikanaji wa nishati safi na salama ya kupikia vijijini pamoja na maeneo yaliyo pembezoni mwa miji. Gharama ya mradi ni milioni 455.7 na mwanachi atatakiwa kuwa na kitambulisho chake cha Taifa (NIDA) pamoja na pesa taslimu 17,500 tu. Mitungi inapatikana kwa gharama nafuu, yanatunza mazingira, yanadumu na rafiki kwa afya ya watumiaji.

Majaliwa Mgeni Rasmi Mashindano ya Kuhifadhi Qur’an

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo Machi 08, 2025 ni mgeni rasmi kwenye fainali za mashindano ya kuhifadhi Qur’an Tukufu ya Afrika Mashariki na Kati. Mashindano hayo yanafanyika katika uwanja wa mpira wa miguu wa Azam, uliopo Chamanzi jijini Dar es Salaam. Mashindano hayo yameandaliwa na Taasisi ya Mana’hil al Irfan Foundation. 

UDA na ODM wabuni muungano wa kisiasa kuelekea 2027

Chama cha United Democratic Alliance (UDA) Kinachoongozwa na Rais wa Kenya Dokta William Ruto pamoja na Orange Democratic Movement (ODM) Kinachoongozwa na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Nchi hiyo Raila Odinga vimebuni ushirikiano wa kisiasa katika hafla iliyoandaliwa katika Ukumbi wa KICC. Vyama hivyo viwili vimeafikiana kushirikiana katika masuala kumi kuu yafuatayo: 1. Utekelezaji kikamilifu wa ripoti ya uwiano wa kitaifa maarufu kama NADCO 2. Usawa katika ugavi wa Pato la Taifa (GDP) na nyadhifa za uongozi Serikalini.  3. Kulinda na kuimarisha ugatuzi 4. Uwekezaji wa kiuchumi kwa vijana.  5. Kuleta uadilifu na uongozi bora 6. Kudumisha uhuru wa kujumuika na kulipa dhamana kwa kesi zote za wanaharakati 7. Kufanya ukaguzi wa hesabu kuhusu deni la serikali na jinsi pesa hizo zilivyotumika 8. Kupambana na ufisadi 9. Kuzuia matumizi mabaya ya rasilimali za umma 10. Kulinda uhuru wa wananchi, kuzuia utekaji nyara, kuheshimu sheria, na uhuru wa raia Ushirikiano huo umeashiria muungano m...

Dkt.Mwinyi Azihamasisha Nchi za Eac Kuanzisha Mifuko ya Maendeleo ya Petroli

  📌 *Asema lengo ni kuwa na uhakika wa kuendeleza Sekta ya Mafuta na Gesi Asilia*  ðŸ“Œ *Afunga Kongamano na Maonesho ya Petroli ya Afrika Mashariki* 📌 *Ataka Rasilimali na Mafuta na Gesi Asilia kuchangia maendeleo ya Sekta nyingine* Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi amezihamasisha nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa na Mifuko ya Maendeleo ya Petroli (Petroleum Fund) ambayo itasaidia katika  utafiti, ubunifu, mafunzo na uendelezaji wa  Sekta ya Mafuta kwa ujumla. Dkt. Mwinyi ameyasema hayo tarehe 07 Machi 2025 jijini Dar es Salaam wakati akifunga  Kongamano na Maonesho ya Petroli Afrika Mashariki (EAPCE’25) ambalo limefanyika kwa Siku Tatu. Ameeleza kuwa, Dira ya Afrika Mashariki ya 2050 inaelekeza kuhusu kuanzishwa kwa Mfuko huo wa Petroli hivyo huu  ni wakati muafaka wa kutekeleza suala hilo kama lilivyoainishwa katika Ibara ya 114 ya Mkataba wa Afrika Mashariki ambayo inaelekeza kuimarisha mashirikiano k...

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi akabidhi Rambirambi ya Amiri Jeshi Mkuu kwa Familia ya Askari wa Jwtz

  Amiri Jeshi Mkuu,Rais Samia Suluhu Hassan amekabidhi rambirambi kwa familia ya aliyekuwa askari wa Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania(JWTZ)Private John Nyewata aliyefariki Januari 27 mwaka huu nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo(DRC) Rambirambi hiyo imekabidhiwa kwa familia hiyo kwa niaba ya Rais Samia na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda. Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo sanjari na kutoa pole,Jenerali Mkunda amesema kuwa Rais Samia ameguswa na vifo vya askari Private John Nyewata na Sajenti Mohamed Abdalah vilivyotokea wakiwa kwenye majukumu ya kikazi ya kurejesha amani iliyotoweka mashariki wa Drc. “Ndugu wanafamilia,Jamaa na Marafiki  pamoja na Majirani,Tambueni Msiba huu si wenu peke yenu wala Jwtz bali ni Msiba wa watanzania wote akiwemo Amiri Jeshi Mkuu ambaye ameguswa sana na Msiba huu na kunituma kuwasilisha ubani pamoja na salamu zake za pole”alisema Jenerali Mkunda Aidha Jenerali Mkunda ameiasa familia Mare...

Mchezo Umekwisha

 Rais William Ruto na aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga wakati wa kutia saini makubaliano ya kuimarisha ushirikiano kati ya ODM na UDA.

Rea Yaendelea Kutekeleza Mkakati Wa Taifa Wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia Kwa Vitendo

  Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unaendelea na jitihada mbalimbali za uelimishaji, uhamasishaji na usambazaji wa bidhaa za Nishati Safi za Kupikia katika Mikoa yote Tanzania Bara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kwa lengo la  kuhakikisha 80% ya Wananchi wanatumia Nishati Safi za Kupikia ifikapo Mwaka 2034. Hayo yameelezwa Machi 7, 2025 Jijini Arusha na Kaimu Meneja Usaidizi wa Kiufundi kwa Waendelezaji Miradi REA, Mhandisi Emanuel Yesaya wakati wa Maonesho ya Kuelekea Siku ya Wanawake Duniani 2025. "Tunashiriki kutoa elimu, kuonyesha bidhaa mbalimbali za nishati safi ya kupikia na kuhamasisha wananchi hususan akina mama kutumia nishati safi ya kupikia ili kurahisisha maisha yao sambamba na kulinda afya zao," alisema Mhandisi Yesaya Alisema REA imeandaa program mbalimbali zinazolenga kumrahisishia maisha mwanamke hasa ikizingatiwa kuwa mwanamke ndiye kinara wa jiko. Alisema Serikali inatambua umuhimu wa kulinda afya za wananchi wake sambamba na kuhifadhi mazingira ambayo...