Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametangaza uamuzi wa Tanzania kufungua tena ubalozi wake nchini Angola, huku akieleza mikakati ya kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kidiplomasia kati ya mataifa hayo mawili. huku hatua hiyo inaambatana na mipango ya kuandaa kongamano la wafanyabiashara na kuanzisha safari za ndege kati ya Tanzania na Angola kwa lengo la kukuza biashara, uwekezaji na maendeleo ya wananchi. Rais Samia ametoa kauli hiyo leo, Oktoba 29, 2026, Ikulu jijini Dar es Salaam, baada ya mazungumzo rasmi na Rais wa Angola, João Manuel Gonçalves Lourenço, aliyeko nchini kwa ziara ya kitaifa ambapo amesema Tanzania inakusudia kuimarisha uhusiano huo kupitia hatua mbalimbali zitakazorahisisha mawasiliano na kuongeza ushirikiano katika maeneo yenye maslahi ya pamoja. Akizungumzia kufunguliwa tena kwa ubalozi huo, Rais Samia amesema tayari amemweleza Rais Lourenço kuhusu uamuzi huo na kwamba katika kipindi kijacho atateua balozi wa kusimamia shu...
Marato tv - Sauti ya Jamii