Skip to main content

Posts

Showing posts from August 19, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Masauni Ajivunia Maendeleo Jimbo la Kikwajuni Kwa Miaka Mitano

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar na mtia nia wa ubunge jimbo hilo kupitia Chama Cha Mapinduzi - CCM, Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amemshukuru Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi kwa utekelezaji mkubwa wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020, suala lililowezesha Jimbo la Kikwajuni na Tanzania kwa ujumla kupiga hatua kubwa za Kimaendeleo. Mhe. Masauni amebainisha hayo Agosti 19, 2025 wakati akitoa tathimini ya utekelezaji wa Ilani ya CCM kwenye Jimbo la Kikwajuni pamoja na ahadi zake mbalimbali, akijivuni kasi kubwa ya maendeleo iliyopatikana katika huduma mbalimbali za Jamii, ikiwemo Ongezeko kubwa la huduma ya Maji safi na ya uhakika kwa wananchi pamoja na Ajira kwa Vijana. "Nichukue fursa hii kuwashukuru sana Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, vilevile na Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa kazi kubwa na nzuri wa...

Mpango Bora wa Ufugaji Nyuki Wawafikia Machifu Rukwa

Na Sixmund Begashe, Rukwa.  Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) imewakabidhi  zaidi ya Mizinga 20O ya nyuki kwa Machifu wa Mkoa wa Rukwa ikiwa sehemu ya utekelezaji wa  Mpango wa Kuendeleza Sekta ya Ufungaji Nyuki kwa Tanzania iliyo Bora ujulikanao kama 'Achia Shoka Kamata Mzinga'. Akikabidhi Mizinga hiyo kwa machifu hao wa Wilaya ya Sumbawanga mkoani humo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anayeshughulikia Uhifadhi, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba, amesema  Mpango huo unalenga kuongeza uzalishaji wa asali kutoka tani 33,861 za sasa hadi kufikia tani 75,000 kwa mwaka ifikapo Juni 2035. CP. Wakulyamba amesema ugawaji wa mizinga hiyo unaunga mkono juhudi za Mhifadhi namba moja nchini Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuwainua wanachi kiuchumi kupitia Uhifadhi wa Maliasili hususan Misitu na Nyuki.  "Pamoja na kuhakikisha kuwa rasilimali hizi zinaendelea kuhifadhiwa Mheshimiwa Rais...

Dkt. Biteko Azindua Mpango wa Utekelezaji Ajenda ya Wanawake, Amani na Usalama

📌 Azitaka Wizara na Taasisi kutenga Bajeti kusimamia utekelezaji wa Mpango huo 📌 Awataka Wanawake kupambana katika maeneo waliyopo 📌 Awashukuru wadau wa maendeleo uandaaji wa Mpango huo  Na WMJJWM- Dar Es Salaam  Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Doto Mashaka Biteko amezindua Mpango Kazi wa Kitaifa wa Kutekeleza Ajenda ya Wanawake, Amani na Usalama 2025-2029. Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Mpango huo Agosti 19, 2025 uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani (TPTC) kilichopo Kunduchi mkoani Dar Es Salaam, Dkt. Biteko amezitaka Wizara na Taasisi za Serikali na Wadau mbalimbali wa maendeleo kuhakikisha wanatenga Bajeti ya utekelezaji wa Mpango huo ili kutimiza malengo yake "Naomba nitoe rai kwa Wizara zote zenye dhamana ya agenda hii; Tanzania Bara na Zanzibar; mkasimamie na kutekeleza mpango huu kama ilivyokusudiwa ili kufikia malengo stahiki" amesema Dkt. Biteko  Aidha Dkt. Biteko amesema katika utekelezaji wa Mpango huo amewataka Wak...

Dc Sima Amwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kwenye Harambee ya Kuchangia Ujenzi wa Kanisa

 ▪️Bukoba,  Kagera.  _Mkuu wa Mkoa atoa Mabati kuezeka Kanisa hilo, zaidi ya milioni 17 zapatikana kati ya 34 zinazohitajika._ Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe. Erasto Sima amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Hajjat Fatma Mwassa kwenye Ibada na harambee ya ujenzi wa Kanisa la KKKT, Mtaa wa Mishenye, Kata ya Butelankuzi lililopo Jimbo la Magharibi Dayosisi ya Kaskazini Magharibi. Mwaliko wa kushiriki Harambee hiyo ulitolewa na Askofu Msaidizi Prof. Josephat Rweyemamu.  Kwenye harambee hiyo, kiasi cha milioni 17,587,000 zilipatikana kati ya hitaji la milioni 31,100,000 ambapo Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Fatma Mwassa alichangia mabati ya kuezeka Kanisa hilo pindi likikamilika. Viongozi mbalimbali wa ushirika huo, Afisa Tarafa hiyo ya Rubale Ndugu Erick Ishengoma, Watendaji wa Kata na Vijiji mbalimbali walikuwepo pia.

Wananchi Waipongeza Serikali Ujenzi Wa Daraja La Mawe Kijiji Cha Buturu

#Limekuwa  Mkombozi kwa wajawazito na watoto #Kuunganisha Vijiji vya Buturu na Chifu Wanzangi Butiama Wananchi wa kijiji cha Buturu Wilayani Butiama Mkoani Mara wameipongeza Serikali kwa kuwajengea daraja ambalo linakuwa mkombozi kwa kupunguza vifo vya wajawazito wakati wa kijifungua pamoja na watoto kusombwa na maji wakati wa kwenda shule kutokana na kuwepo na bonde katika barabara  kuu ya kijiji hicho. Bw. Maningu kasombi, Mwenyekiti wa kijiji cha Buturu anasema kabla ya ujenzi wa daraja hilo la mawe wakazi wa kijiji hicho walikuwa inawalazimu kutumia gharama kubwa katika usafiri kwa kuzunguka vijiji  vingine ili kufikia huduma za kijamii na ameweka wazi kuwa wajawazito asilimia kubwa walikuwa wanajifungulia njiani au majumbani kwa kukosa miundombinu mizuri ya barabara. " Ubovu wa barabara ulikuwa unafanya akinamama kujifungulia njiani na wakati mwingine usafiri unakosekana hivyo wengi walikuwa wanajifungulia nyumbani lakini kwa sasa tunatumia barabara hii muda wowote n...