Skip to main content

Posts

Showing posts from May 14, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt. Biteko Ateta na Spika Wa Bunge La Morocco

📌 Tanzania, Morocco wakubaliana kuimarisha ushirikiano Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe Dkt. Doto Biteko Mei 15, 2025 ametembelea Bunge la Morocco ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi nchini humo. Akiwa Bungeni hapo, Dkt. Biteko amefanya mazungumzo na Spika wa Bunge la nchi hiyo Mhe. Rachid Talbi El Alami na Naibu Spika Mhe. Lahcen Haddad katika ofisi za Bunge hilo zilizoko jijini Rabat nchini Morocco. Pamoja na mambo mengine, wamejadili kuhusu namna bora ya kuimarisha uhusiano na ushirikiano baina ya nchi hizo mbili hususan katika Sekta ya Nishati, Kilimo, Viwanda na Biashara. 

Diwani Merysiana Atoa Ujumbe Siku ya Familia Duniani

Na Shomari Binda-Musoma  WAZAZI kwenye familia wametakiwa kutatua migogoro ya kifamilia pale inapojitokeza ili kujiepusha kutengana na watoto kukosa malezi bora. Hayo yamesemwa na diwani wa viti maalum manispaa ya Musoma Meryciana Masasi leo mei 15,2025 alipozungumza na GMTV ikiwa ni siku ya familia duniani. Amesema wimbi la watoto wa mitaani linazalishwa na mambo mengi ikiwa ni pamoja na migogoro inayojitokeza kwenye familia. Diwani huyo amesema iwapo migogoro inapojitokeza na kushindwa kusuruhishwa upelekea wazazi kutengana na watoto kukosa malezi hivyo kukimbilia mitaani. Amesema watoto kukosa malezi ya pande mbili huwa kunatokea changamoto ya kimalezi na kushauri kuwepo na utatuzi wa migogoro ili kuepusha tatizo hilo. " Kupitia siku hii ya familia duniani nitoe ushauri kwa wazazi kuwa na utaratibu wa utatuzi wa migogoro ili tuwalee watoto wetu kwa pamoja na kujenga familia. " Watoto hatupendi waangaike mitaani na wanakuwa wanapata tabu na hii kwa asilimia kubwa inatokana ...

Misa-tan, Wan Ifra Na Thrdc Waendesha Mjadala Uendelevu Vyombo Vya Habari Katika Mawanda Ya Uchumi Unaobadilika

Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA TAN) kwa kushirikiana na Umoja wa Wachapishaji wa Magazeti Ulimwenguni (WAN-IFRA) na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umeendesha mjadala kuhusu uendelevu wa vyombo vya Habari katika mawanda ya uchumi unaobadilika uliowashirikisha wadau mbalimbali wa Habari nchini. Baadhi ya wadau hao ni wamiliki wa vyombo vya Habari, Wahariri wa Vyombo vya Habari, Wahadhiri wa Vyuo vya Uandishi wa Habari na Viongozi wa Taasisi za Habari. Katika mjadala huo, wadau hao wa sekta ya habari walijadili mambo mbalimbali ikiwemo sheria na kanuni za uchaguzi. Kwa upande wake Mwenyekiti wa MISA Tan Edwin Soko amechangia mjadala huo na kusema, kunahitajika jitihada za pamoja kati ya Taasisi za usimamizi wa Vyombo vya habari nchini, Wamiliki wa Vyombo vya habari na waandishi wa habari kukaa pamoja kwenye kujadili uendelevu na uhimilivu wa Vyombo vya habari kwani kufanya hivyo kutasaidia kuwa na mikakati ya pamoja ya namn...

Misa Tan Yamlilia Charles Hillary

Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA Tan), imetoa salamu za pole kufuatia kifo cha mwanahabari mkongwe Charles Hillary, ikisema itaendelea kukumbuka mchango wake mkubwa katika sekta ya habari hapa nchini. Mwenyekiti wa MISA Tan, Edwin Soko, amesema kuwa marehemu Hillary alikuwa na mchango mkubwa sana katika kukuza taaluma ya habari na kutetea uhuru wa vyombo vya habari. “Tumempoteza mtu muhimu sana katika tasnia ya habari. Charles Hillary alikuwa mfano wa kuigwa kwa wanahabari wengi kutokana na weledi, ujasiri na kujitolea kwake kwa maslahi ya taaluma,” alisema Soko. MISA Tan imeeleza kuwa itaendelea kuenzi ujasiri wa marehemu kwenye kuipambania sekta ya habari na pia inatoa pole Kwa familia na watanzania wote

Mke wa Rais wa Finland Suzanne Innes-Stubb atembelea Makumbusho ya Taifa la Tanzania

Mke wa Rais wa Finland Suzanne Innes-Stubb atembelea Makumbusho ya Taifa la Tanzania Ujio wa ziara hiyo umefanyika leo tarehe 14/05/2025 Makumbusho ya Taifa la Tanzania katika kituo cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni kilichopo Posta, Dar es salaam. Ziara hii ni utangulizi wa ziara ya kesho tarehe 15/05/2025 ambapo Makumbusho ya Taifa inatarajia kumpokea Rais wa Jamhuri ya Finland, Alexander Stubb, aliyewasili jijini Dar es Salaam, Tanzania kwa ziara rasmi ya siku tatu kuanzia Mei 14 hadi 16, 2025. Akiwa kituo cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni, Mke wa Rais wa Finland Bi. Suzanne Innes-Stubb alipokelewa kwa ngoma za asili kisha wenyeji wake Dkt. Hassan Abbasi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Dkt. Noel Lwoga, Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa la Tanzania walimkaribisha. Akiongea baada ya kumpitisha maeneo mbalimbali na kujionea mikusanyo na historia ya Tanzania iliyohifadhiwa kituoni hapo Dkt. Lwoga amesema ni mafanikio makubwa ya Serikali ya awamu ya sita kati...

Tanzania na Finland Zasherekea Miaka 70 ya Ushirikiano

Tanzania na Finland zinasherehekea miaka 60 ya ushirikiano uliojengwa katika misingi ya urafiki, maelewano na kuheshimiana. Ziara hii ni hatua ya nchi zetu kuendelea kuimarisha ushirikiano huo ambao matunda yake tumeendelea kuyaona katika sekta za utawala bora, elimu na utunzaji mazingira. Tumejadili na kukubaliana kuongeza maeneo mapya ya ushirikiano katika sekta zinazogusa maisha ya watu wetu kama vile uchumi wa buluu, nishati, elimu na teknolojia. Aidha, nimetumia nafasi hii kuwakaribisha wafanyabiashara alioambatana nao kuangalia fursa za biashara na uwekezaji nchini.

Serikali ya Kenya yafunga jengo la Freemason kwa kutolipa kodi

Serikali ya Kaunti ya Nairobi nchini kenya imelifunga jengo la Freemasons  Hall la Grand Lodge of East Africa lililoko katikati ya jiji kutokana na deni la kodi ya ardhi lililofikia Ksh. milioni 19 [TZS milioni 396.6]. Operesheni hiyo imeongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Afya katika Baraza la Mawaziri wa Kaunti, Suzanne Silantoi, ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kaunti dhidi ya wadaiwa wa kodi, aliyeongozana na maafisa wengine ambao walisema taratibu zote zilifuatwa kabla ya kufunga jengo hilo ikiwa ni pamoja na kutuma barua na kutoa ilani za madai na matangazo kwenye magazeti. Silantoi ameongeza kuwa kaunti haitaishia kufunga majengo ya wadaiwa pekee, bali pia itazuia huduma kama maji na mifereji ya majitaka kwa wale wanaoshindwa kulipa. Kufungwa kwa Freemasons Hall kumekuja siku moja baada ya kaunti kufunga majengo manne katika eneo la biashara jijini Nairobi kwa sababu ya kutolipa kodi ya pango. Kaunti imeahidi kuendelea na zoezi hilo kwa majengo mengine. Freemasons Hall, ni jengo la ...

Chama cha Gachagua kimeiva, tayari kutajwa rasmi Alhamisi

ALIYEKUWA Naibu Rais wa Kenya Rigathi Gachagua Alhamisi, Mei 15, 2025 anatarajiwa kutaja chama cha Democracy for Citizen Party (DCP) kama chombo kipya cha kisiasa atakachokitumia  kulemaza kabisa chama cha United Democratic Alliance (UDA) cha kwake Rais William Ruto katika ngome yake ya Mlima Kenya. Duru zinasema kwamba Bw Gachagua na wandani wake wamekamilisha mipango ya hafla hiyo itakayofanyika katika kaunti ya Nairobi. Mbunge huyo wa zamani wa Mathira anapania kukitumia chama hicho kuunda muungano mpya wa kisiasa na vyama vingine vya upinzani kwa nia ya kumwondoa mamlaka Rais William Ruto 2027. “Ndio tuko tayari kwa shughuli muhimu kesho (Mei 15, 2025). Alivyosema bosi wetu chama hicho kipya ni cha kitaifa wala sio cha kikabila au cha eneo la Mlima Kenya inavyodhaniwa,” amesema Mbunge mmoja wa Nairobi, ambaye ni mwandani wa karibu wa Bw Gachagua. Lakini mwanasiasa huyo alidinda kutaja mahala mahsusi ambako shughuli hiyo itaendeshwa akisema “hatutaki maadui wetu waharibu ha...

Rais Samia akiwa na Mgeni wake Rais wa Finland Alexander Stubb,Ikulu Dar es salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Finland Mhe. Alexander Stubb mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Mei, 2025. Rais wa Jamhuri ya Finland Mhe. Alexander Stubb akikagua Gwaride la heshima lililoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Mei, 2025.