Skip to main content

Posts

Showing posts from October 31, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Profesa Kithure Kindiki aapishwa kuwa Naibu rais wa kenya

Profesa Kithure Kindiki ameapishwa kuwa naibu rais wa Jamhuri ya kenya.  Profesa Kindiki amechukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Naibu rais wa Kenya Rigathi Gachagua aliyeondolewa ofisini na Bunge la kitaifa na Bunge la seneti baada ya kuhusishwa na tuhuma kadhaa zikiwemo za kuendeleza ukabila.  Akizungumza Mara baada ya kula kiapo,Profesa Kindiki ameahidi kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria za nchi pamoja na kumshauri vyema Rais wa taifa hilo Dkt.William Ruto.  Profesa Kindiki ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa waziri wa usalama wa ndani na utawala wa Taifa na anakuwa Naibu rais wa 14 katika historia ya kenya na wa tatu chini ya katiba mpya ya mwaka 2010. Kabla ya kuteuliwa waziri mwaka 2022 na Naibu rais mwaka 2024,Profesa Kithure Kindiki alihudumu kama seneta wa kaunti ya Tharaka Nithi kuanzia mwaka 2013 hadi 2022 ambapo katika kipindi hicho pia alihudumu kama Naibu Spika wa Bunge la Seneti pamoja na kiongozi wa wengi katika Seneti.  Akiwa Kiongoz...

Mpango kuongoza makamanda na watanzania kuaga mwili wa mkuu wa majeshi mstaafu

MAKAMU wa Rais mh Dkt Philip Mpango kuongoza Maafisa Jenerali,  Maafisa Wakuu, Maafisa wadogo na Askari wa JWTZ kuaga mwili wa mkuu wa majeshi mstaafu Jenerali David Bugozi Musuguri. Mh Mpango atamwakilisha amiri jeshi mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania mh Dkt SamiaSuluhu Hassan kuaga mwili huo leo novemba 01- 2024 katika hospitali kuu ya Jeshi Lugalo Jijini Dar es Salaam.  Zoezi hilo linatarajiwa kufanyika saa tatu asubhi kabla ya mwili huo kusafirishwa kuelekea Butiama mkoani Mara kwa ajili ya shughuli ya mazishi. Jenerali Musuguri alifariki dunia asubhi ya Oktoba 29 mwaka 2024 wakati akapatiwa matibabu hospitali ya Kanda ya Bugando jijini Mwanza,enzi za uhai wake ameshika nafasi mbalimbali ndani ya jeshi hadi kuwa mkuu wa majeshi kuanzia mwaka 1980 hadi 1988 alipostaafu kwa heshima. Jenerali Musuguri akiwa jeshini amekuuwa mkufunzi wa askari wakati wa ukoloni wa Mwingereza. Mwaka 1953 alimfundisha pia Idd Amin katika kambi ya mafunzo ya Kahawa Barracks nchini Keny...

Waziri Aweso alivalia njuga suala la upatikanaji wa maji jijini dodoma

▪️Aelekeza timu ya wataalamu kufanya utafiti wa kina wa upatikanaji wa maji ▪️Ataka visima virefu vichimbwe kwa uwingi ▪️Apiga marufuku wananchi kubambikiziwa bili za maji ▪️Mbunge Mavunde aomba utekelezaji wa Mradi wa Nzuguni A kupunguza mgao wa maji 📍𝐃𝐨𝐝𝐨𝐦𝐚 Waziri wa Maji *Mh. Jumaa Aweso* jana amefanya ziara katika maeneo ya Miganga-Mkonze na Nkuhungu kuangalia hali ya upatikanaji wa maji Jijini Dodoma na kutoa maelekezo kwa watendaji maji kuimarisha utafiti wa kina wa upatikanaji wa maji ili zoezi la uchimbaji visima virefu lianze kwa uharaka. “Mh Rais Dkt. Samia S. Hassan ametupatia vifaa vya kisasa vya utafiti wa kina wa upatikanaji wa maji,nataka vianze kazi hiyo hapa Jijini Dodoma ili tuendelee na uchimbaji wa visima virefu kutatua adha ya upatikanaji wa maji iliyosababishwa na ongezeko kubwa la watu Jijini Dodoma. Wakati tunasubiri mradi mkubwa wa kutoa maji Ziwa Victoria na Mradi wa Bwawa la Farkwa,endeleeni kuchimba visima virefu maeneo tofauti tofauti ya Jiji ili kup...

Aicc ni muhimili wa sekta ya utalii nchini

Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) kimeelezwa kuwa ni moja ya muhimili muhimu katika kufanikisha agenda ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kukuza sekta ya utalii nchini. Kauli hiyo imetolewa leo Oktoba 31, 2024 na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (EAC), Mhe. Denis Londo alipokutana na uongozi wa kituo hicho chini ya Mkurugenzi Mtendaji, Bi. Christine Mwakatobe. Mhe. Londo alisema kuwa Rais Samia amelipa umuhimu mkubwa suala la utalii ndiyo maana amecheza filamu ya Tanzania: The Royal Tour, na manufaa yake yameaanza kupatikana kwa kuongezeka kwa watalii na fedha za kigeni nchini.  "Utalii una maeneo mengi na moja kati ya hayo maeneo ni utalii wa mikutano. Hivyo, kwa  Tanzania hakuna taasisi nyingine inayotegemewa na Serikali kulitekeleza kwa ufanisi eneo hili na kulitolea  miongozo isipokuwa AICC pekee", Naibu Waziri Londo alisema. Mhe. Londo aliongeza kuwa AICC ndiyo sura na kioo cha nchi na ni moja ya kituvu cha diplomasia ya Ta...

Wajumbe wa bodi Nirc waahidi ushirikiano na mwenyekiti mpya wa bodi

 Na NIRC; Dodoma Wajumbe wa Bodi ya Uongozi na Menejimenti ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumteua  Dkt. Richard Joseph Masika kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji na kuahidi kumpa ushirikiano ili kufikia malengo ya serikali ya Agenda10/30. Wakizungumza baada ya kuhitimisha Kikao cha Bodi cha Robo ya Tatu na Nne kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024  kilichofanyika jijini Dodoma, baadhi  ya wajumbe wa Bodi ya Uongozi ya Tume wameahidi kumpa ushirikiano katika kukuza sekta ya kilimo cha umwagiliaji nchini. Aidha wajumbe hao wamekiri kuridhishwa na namna Tume inavyofanya shughuli zake za ujenzi miundombinu ya umwagiliaji, ukusanyaji wa ada ya huduma za umwagiliaji, uendelezaji wa miundombinu ya umwagiliaji,utafiti na usanifu wa miradi ya umwagiliaji. Dkt.Richard Joseph Masika ni Mhandisi Mshauri aliyeidhinishwa katika Uhandisi wa Miundombinu na  aliwahi kuwa Mkuu...

Idara ya habari nchini kuhifadhi nyaraka za Taifa kidijitali

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Thobias Makoba, leo Oktoba 31, 2024 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Firimin Msiangi ambapo wamekubaliana kushirikiana katika kuitangaza idara hiyo na kuwezesha uhifadhi wa nyaraka kidijitali.  

Naibu rais mteule wa kenya kuapishwa kesho 1/11/202

 Na Mwandishi Wetu;Nairobi Naibu Rais mteule wa kenya Profesa Kithure Kindiki Kesho novemba mosi anatarajia kuapishwa kuwa Naibu Rais wa Kenya Profesa Kindiki anachukua nafasi ya Rigathi Gachagua aliyeondolewa ofisini kutokana na tuhuma mbalimbali ikiwemo ya kuendeleza ukabila.  Kwa mujibu wa Tangazo lililotolewa usiku huu kwenye gazeti rasmi la serikali,Uapisho wa Profesa Kindiki utafanyika Kesho katika kituo cha kimataifa wa Kenyatta international convention Center(K.I.C.C) uliopo katika kaunti ya Nairobi kuanzia majira ya saa nne kamili za asubuhi.  Naye Kaimu Waziri wa usalama wa ndani na utawala wa kitaifa Musalia Mudavadi ametangaza siku ya Kesho kuwa sikukuu ya taifa ili kutoa fursa kwa wakenya kushiriki pamoja kufuatilia uapisho wa Naibu Rais mteule.  Profesa Kindiki anatarajia kuapishwa baada ya mahakamani kuu kuondoa zuio la kuapishwa lililokuwa limewekwa na mtangulizi wake Rigathi Gachagua.  Kindiki ambaye kwa sasa ni Waziri wa usalama wa ndani na uta...

Naibu rais wa kenya aliyeondolewa ofisini Rigathi Gachagu agonga mwamba mahakamani

 Na Mwandishi Wetu ;Nairobi Juhudi za Naibu Rais wa Kenya aliyetimuliwa ofisini Rigathi Gachagua kusimamisha kuapishwa kwa Naibu rais mpya Profesa Kithure Kindiki zimegonga mwamba Leo alhamisi Oktoba 31. Gachagua amepata pigo mara mbili,pigo la kwanza ni pale mahakama ya rufaa ilipokataa takwa lake la kusimamisha majaji watatu wa mahakama kuu walioteuliwa na Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu kusikiliza kesi ya kupinga kuondolewa ofisini huku pigo la pili likiwa ni m ahakama kuu kuondoa zuio la kuapishwa kwa mrithi wake.  Muda mfupi baada ya uamuzi wa mahakama ya rufaa,Majaji watatu ambao Gachagua alikuwa akipinga kusikiliza kesi yake waliondoa agizo lililompa ahueni kwa wiki mbili tangu atimuliwe na Bunge la kitaifa na Bunge la Seneti pamoja na Rais William Ruto kumteua profesa Kithure Kindiki kuwa naibu rais. Majaji wa mahakama ya rufaa Patrick kiage,Agrey Muchelule na George Odunga waliagiza kesi iliyowasilishwa na Gachagua isikilizwe novemba sita mwaka huu. ‘’Hatuwezi kuondoa...

Mwanahabari mahiri na kiongozi wa Taasisi za kihabari Edwin Soko aelekea kuachana na ukapela

 "Wakati wa Bwana ukifika Mungu anatenda" Edwin Soko alisema hayo kwenye sendoff ya mke wake mtarajiwa Lulu Samson Mbwaga Jijini Mbeya Bibi. Harusi mtarajiwa. Lulu Samson Mbwaga

Waziri mkuu ameagiza mamlaka za serikali kutenga bajeti kabla ya kutwaa ardhi

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema taasisi yoyote ambayo inahitaji kutwa ardhi ambapo wananchi wanaishi au wanafanya shughuli mbalimbali za maendeleo lazima iwe imetenga bajeti ya kuwafidia kabla ya kufanyika kwa zoezi hilo ili kuondoa usumbufu.   Ameyasema hayo leo (Alhamisi, Oktoba 31, 2024) wakati akijibu swali la Mbunge wa Kilwa Kusini, Ali Kasinge ambaye alitaka kujua kwa nini Serikali isione uwezekano wa kuruhusu watu waliofanyiwa tathmini kwa ajili ya kutwali maeneo yao wasiruhusiwe kuyaendeleza wakati wakisubiri kulipwa fidia.   “...Utwaaji huo unapaswa kuzingatia sheria, nitoe wito kwa taasisi zote ziwe za umma au sekta binafsi pale ambapo wanafikiria kuanzisha mradi na mradi huo unagusa maeneo ya wananchi ni lazima wajipange kwanza kibajeti kabla hawajaenda kufanya tathmini ili wanapokwenda kufanya tathmini ukipata gharama unalipa mara moja na wananchi waweze kupisha na kwenda eneo lingine.”   Wakati huo huo, Waziri Mkuu amewaagiza Makatibu Tawala wa Mik...