Skip to main content

Posts

Showing posts from July 29, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Majaliwa Kufungua Mkutano wa Kitaifa wa Rasilimaliwatu Katika Sekta ya Afya

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Julai 30, 2024 atafungua  Mkutano wa kitaifa wa Rasilimaliwatu katika Sekta ya Afya sambamba na Kumbukumbu ya Hayati Benjamin  Mkapa. Mkutano huo unafanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam. kaulimbiu ya Mkutano huo ni *“Nguvukazi Sekta ya Afya: Mhimili wa Maendeleo Endelevu”.*  Kaulimbiu hii imebeba uhalisia wa masuala muhimu kwa mandeleo endelevu ya sekta ya afya.

Vitita Vya Bima ya Afya Kwa Wote (UHI) Vizingatie Mahitaji ya Jamii Kwa Ngazi Zote

Na WAF - Arusha Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. John Jingu ametoa rai kwa wataalam wanaoshughulikia maandalizi ya utekelezaji wa Sheria ya bima ya Afya kwa wote, kubuni vitita ambavyo vinazingatia mahitaji ya jamii kwa kujumuisha huduma muhimu ambazo mtu anaweza akazipata na kunufaika nazo kuanzia ngazi ya chini mpaka ngazi ya juu. Dkt. Jingu Ameyasema hayo  Jijini Arusha wakati akifungua kikao kazi cha wataalam wa maandalizi ya utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa wote kinachofanyika mkoani hapo ambapo amesisitiza umuhimu wa wataalamu hao kuangalia huduma ambazo ndio zina tija katika ustawi wa jamii na kuzipa kipaumbele katika vitita watakavyobuni kwa kuendana na mfumo wa rufaa. “Kitita ambacho tutakibuni, kiwe ambacho kila mtu atapata huduma muhimu, kwa mfano je mama mjamzito kitita kitaweza kumsaidia kuzifikia huduma za juu zaidi au hospitali za juu zaidi iwapo atapata changamoto wakati wa kujifungua, na sio kama kitakuwa na huduma zote ila kibebe zile huduma muhimu kulinga...

Kenya Yawasilisha Rasmi Nyaraka za Raila Odinga Kugombea Uenyekiti Tume ya Umoja wa Afrika

Serikali ya Kenya imewasilisha rasmi nyaraka za kumuunga mkono mgombea wake, Raila Odinga, katika azma yake ya kuwa mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AUC). Wakiongozwa na Katibu Mkuu wa wizara ya mashauri ya kigeni Korir Sing'oei, wajumbe wa Kenya waliwasilisha hati hizo kwa Mkuu wa Kanda ya Mashariki, Dharmraj Busgeeth na kwa Ofisi ya Wakili wa Kisheria wa Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa. Kulingana na Sing'oei, vipaumbele vya Raila katika usukani wa AU vitajumuisha; Ushirikiano wa Afrika na Maendeleo ya Miundombinu, Mabadiliko ya Kiuchumi, Kuimarisha Biashara ya Ndani ya Afrika, Uhuru wa Kifedha, Usawa wa Jinsia na Usawa, Mageuzi katika kilimo Hatua za Hali ya Hewa, Amani na Usalama na Ajenda ya kuwazesha vijana Afrika.

Rais Samia Kufanya Ziara Mkoa wa Morogoro

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt, Samia Suluhu Hassan anatarajia Kuanza Ziara ya Kikazi ya Siku Tano Mkoa wa Morogoro kuanzia August 02,2024 . Rais Samia mbali na kuzindua Miradi mbalimbali ya Maendeleo pia atazungumza na Wananchi wa Mkoa huo. Aidha Rais Dkt, Samia anatarajiwa pia kufanya Uzinduzi wa safari za treni ya kisasa ya SGR kutoka Dar es salaam mpaka Dodoma August 01,2024.

Mwenge wa Uhuru Wazindua Jengo la Nyamongo Plaza

Na Mwandishi wetu-Tarime Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024, Godfrey Eliakimu Mnzava, amezindua jengo la kisasa la Nyamongo Plaza lililopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, mkoani Mara. Jengo hilo la ghorofa mbili, ni mali ya mfanyabiashara Josephat Mwita lililojengwa kwa ajili ya shughuli za kibiashara katika mji wa Nyamongo, jirani na Mgodi wa Dhahabu wa North Mara. Akizungumza mara baada ya kuzindua jengo hilo wakati wa mbio za Mwenge katika mji ndogo wa Nyamongo, Mnzava amempongeza mwekezaji huyo na kusema hatua hiyo ni kielelezo cha ushiriki wa sekta binafsi katika kuchangia ukuzaji wa uchumi nchini. Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024, Godfrey Eliakimu Mnzava akizindua jengo la Nyamongo Plaza. Kushoto ni mmiliki wa jengo hilo, Josephat Mwita na kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Tarime, Mwalimu Saul Mwaisenye. Amempongeza mwekezaji huyo Bw Josephat Mwitakwa kazi hiyi nzuri na kusema ujenzi huo ni sehemu ya kuunga mkoni juhudi za Rais Dkt Samia Su...