Na OWM - TAMISEMI, Morogoro Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) Mhe. Prof. Riziki Shemdoe amewaasa vijana wa vyuo vikuu kuwa waadilifu na wazalendo pindi watakapoajiriwa Serikalini kuwatumikia wananchi au kupata fursa za uongozi wa kulitumikia taifa. Prof. Shemdoe ametoa wito huo kwa vijana hao Juni 20, 2026, wakati akifungua Kongamano la Vijana (Youth Uongozi Forum) kwa niaba ya Mhe. Prof. Palamagamba John Aaidan Kabudi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge,Uratibu na Wenye Ulemavu) ambalo linalofanyika katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe mjini Morogoro, lililoandaliwa na taasisi ya Tanzania Leadership Foundation (TLF). “Vijana wangu, watoto wangu, wadogo zangu mjitahidi sana kuwa waadilifu na wazalendo kwani mkishindwa kuwa waadilifu na wazalendo hamtaweza kudumu katika nafasi mtakazoaminiwa kuzitumikia,” amesisitiza Prof. Shemdoe. Sanjari na hilo, Prof. Shemdoe amewataka vijana hao kuwa wanyenyekevu watakapopa...
Marato tv - Sauti ya Jamii