Skip to main content

Posts

Showing posts from February 1, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dc Itunda Azindua Kituo Cha Polisi Igoma

📍Ahimiza ulinza wa miundombinu na mapambano dhidi ya ukatili *NA MWANDISHI WETU, MBEYA* MKUU wa Wilaya ya Mbeya, Mhe. Solomon Itunda, amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Beno Malisa, katika hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Polisi cha Kata ya Igoma, kilichogharimu Shilingi milioni 150.  Hatua hiyo ni mkakati wa serikali kuimarisha ulinzi, usalama, na kusogeza huduma za kijamii karibu na wananchi. Akizungumza katika uzinduzi huo uliokwenda sambamba na makabidhiano ya miundombinu hiyo, Mhe. Itunda amesema ujenzi wa kituo hicho ni matokeo ya juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuboresha mazingira ya kazi ya vyombo vya ulinzi nchini. Mhe. Itunda amebainisha kuwa uwekezaji huo mkubwa katika sekta ya usalama unalenga kudumisha amani na utulivu, mambo ambayo ni nguzo kuu katika kuchochea maendeleo ya kiuchumi ndani ya Mkoa wa Mbeya na taifa kwa ujumla. Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Wilaya ametoa onyo kali kwa watu wanaojihusisha na...

Mbunge wa Jimbo la Kyerwa Akoshwa na Utendaji wa Waziri Ulega

 Na Angela Sebastian; Kyerwa Mbunge wa Jimbo la Kyerwa, mkoani Kagera Khalid Nsekela, amemshukuru Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega kwa kuchukua hatua madhubuti na kufika jimboni humo kujionea hatua ya utekelezaji wa mradi wa barabara ya Omurushaka–Karagwe hadi Rwenkorongo (Kyerwa) ambapo amesema ni uthibitisho kwamba Serikali ya hawamu ya sita inajali wananchi wake. Hatua hiyo ya Ulega imetokana na mbunge huyo baada ya kuuliza swali bungeni wiki hii kuhusu ujenzi wa barabara hiyo usivyolidhisha na kusababisha wananchi kupata adha wakati wa kusafiri hususani wagonjwa na wajawazito ambapo waziri huyo alitoa majibu na kuahidi kufika kujionea hari hiyo ndani saa 72 ambapo ametekeleza ahadi hiyo. Nsekela amesema barabara hiyo imekuwa kilio cha muda mrefu kwa wananchi wa Kyerwa kutokana na umuhimu wake katika kuchochea maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kurahisisha usafiri wa watu na bidhaa zao. “Barabara hii ilikuwa imekwama kwa muda mrefu na imekuwa kilio kikubwa cha wananchi wa Ji...

Waziri Mkuu Ahimiza Malezi Ya Vijana Kwa Ajili ya Kuimarisha Maadili na Mshikamano wa Taifa

_Atoa tahadhari dhidi ya kuingiza mijadala ya kejeli katika masuala ya imani_ WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amehimiza malezi bora ya watoto na vijana kama silaha muhimu ya kudumisha maadili, mshikamano na amani katika jamii, huku akitahadharisha dhidi ya wanaoingilia masuala ya imani, hatua ambayo inaweza kuhatarisha mshikamano wa Taifa. Akizungumza leo jumapili Februari 01, 2026 katika ibada ya Kanisa Kuu la KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati, Usharika wa Arusha Mjini, iliyokuwa ikiongozwa na Baba Askofu Dkt. Godson Abel Mollel, Waziri Mkuu alisema mmomonyoko wa maadili unaoanza na kejeli mitandaoni, dharau kwa wazee na viongozi pamoja na kukosa staha kwa mamlaka, unaweza kuathiri misingi ya Taifa endapo hautadhibitiwa mapema kupitia malezi thabiti. Waziri Mkuu alibainisha kuwa malezi thabiti ndiyo msingi uliowezesha Tanzania kudumisha amani, mshikamano na kuheshimiana bila kujali tofauti za kidini, kikabila au kiuchumi. Alisisitiza jukumu la Serikali, taasisi za dini, familia na jam...

Waziri Mavunde Azindua Urushwaji wa Helikopta ya Utafiti wa Kina wa Madini

▪️Ni utafiti utakaofanywa na Kampuni ya Barrick kwa ajili ya uanzishwaji wa mgodi mpya ▪️Utagusa maeneo ya Msalala, Nzega,Nyangh’wale, Igunga na Mbogwe ▪️Waziri Mavunde aelekeza wachimbaji wadogo kupewa maeneo ambayo hayatatumiwa kwa uwekezaji mkubwa  ▪️Utafiti huu kuongeza eneo la Utafiti wa madini wa kina nchini Buzwagi, Kahama Ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa Serikali kuhakikisha inafikia lengo la kuongeza eneo la utafiti kufikia asilimia 50 ifikapo 2030, Waziri wa Madini, *Mh. Anthony Mavunde (Mb)* azindua urushwaji wa Helkopta iliyofungwa vifaa vya kisasa kwa ajili ya utafiti wa madini nchini. Amefanya uzinduzi huo leo tarehe 01 Februari, 2026 katika eneo la Buzwagi Wilayani Kahama kuashiria kuanza rasmi utafiti utakaofanywa na Kampuni ya Barrick kwa ajili ya uanzishwaji wa mgodi mpya. "Kupitia Dira ya Madini 2030: Madini ni Maisha na Utajiri, *Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan* ametuelekeza kuhakikisha tunaongeza eneo la utafiti wa kina wa madini kupitia uwekeza...