Skip to main content

Posts

Showing posts from October 13, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

USHIRIKA AFRIKA WAGEUKIA TEKNOLOJIA KUVUTA VIJANA NA KUBORESHA HUDUMA ZA FEDHA

Vyama vya ushirika vya akiba na mikopo barani Afrika vinakabiliwa na umuhimu wa kuimarisha matumizi ya teknolojia na kuweka mazingira yatakayowavutia vijana kujiunga na kushiriki kikamilifu, hatua inayolenga kuboresha huduma za kifedha na kuongeza ufanisi wa taasisi hizo. Mjadala huo umeibuliwa Leo Oktoba 13 ,2026 Jijini Dar es Salaam katika mkutano wa vyama vya ushirika barani Afrika unaosimamiwa na Shirikisho la Vyama vya Ushirika vya Akiba na Mikopo Afrika (ASCOSCA), unaojadili mafanikio ya sekta ya fedha, nafasi ya teknolojia katika utoaji wa huduma na changamoto zinazokwamisha ushiriki wa vijana. Akizungumzia masuala hayo, Bw. Collin Nyaunga, Naibu Mrajisi wa Vyama vya Ushirika katika Tume ya Maendeleo ya Vyama vya Ushirika, iliyo chini ya Wizara ya Kilimo, anahusika katika mjadala unaogusa mwelekeo wa maendeleo ya vyama vya ushirika na umuhimu wa kuimarisha sekta hiyo. Amesema Mkutano huo unatoa fursa kwa wadau kutafakari namna vyama vya ushirika vinavyoweza kuendana na mabadilik...