📍Karatu, Arusha Wakulima wadogo katika Wilaya ya Karatu wamepokea ukombozi mpya wa kiuchumi kufuatia utekelezaji wa mradi wa uchimbaji wa visima vya Umwagiliaji unaofadhiliwa kwa asilimia 100 na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan. Kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC), mradi huu unalenga kutatua changamoto ya muda mrefu ya uhaba wa maji, hasa katika Kata ya Baray ambayo ni kitovu cha uzalishaji wa zao la kitunguu kinachousambazwa katika masoko ya ndani na nje ya nchi. Aidha furaha na matumaini mapya imetanda miongoni mwa wakulima wa Kanda ya Datoga baada ya kukamilika kwa uchimbaji wa visima viwili vitakavyohudumia hekta 66.5 za kilimo. Mkulima Gilbert Makirija, akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi iliyoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Dk. Lameck Karanga, alieleza jinsi walivyokuwa wakisota kwa kusubiri maji ya umwagiliaji kwa siku 11 hadi wiki tatu. Kwa sasa, uwepo wa visima hivyo pamoja na miundombinu ya usambazaji had...
Marato tv - Sauti ya Jamii