Skip to main content

Posts

Showing posts from January 12, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Cosmas Bulala Amefanya Kikao Kazi na CMT-Kwimba

*Kwimba -Mwanza* *Mbunge wa Jimbo la Kwimba na Mwanadiplomasia Mhe COSMAS BULALA ( MWANZA FINEST ) amefanya kikao kazi na wakuu wa idara  ( CMT ) wa halmashauri ya Kwimba na kuonyesha dira yake ya miaka mitano ( 2025-2030 ) ya ubunge wake.* *Mhe BULALA kawapongeza wataalamu wote Kwa KUENDELEA kuchapa kazi za kuwahudumia Wana Kwimba muda wote* *Wataalamu wote wamemshukuru Kwa kuzungumza nao na kumuahidi kushirikiana nae Mhe COSMAS BULALA ( MWANZA FINEST)* *Kwimba ni yetu sote tutaijenga Kwa pamoja🤝🤝🤝🤝*

Waziri Mkuu Aongoza Mkutano Kazi wa Mawaziri.

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameongoza mkutano kazi wa Mawaziri, Makatibu Wakuu na Viongozi Waandamizi wa Serikali uliofanyika, Januari 12, 2026, katika Ukumbi wa Kambarage, Hazina, jijini Dodoma. Katika mkutano huo, viongozi hao wamejadili utekelezaji wa masuala mbalimbali ya Serikali yanayolenga kuimarisha utendaji kazi na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

Dkt.Migiro Kuunguruma Ilala Kesho, Akihitimisha Ziara Jijini Dar Es Salaam

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi-CCM, Dokta Asha-Rose Migiro, kesho tarehe 13.1.2026 anatarajiwa kuhitimisha ziara yake ya kimkakati katika wilaya ya Ilala, mkoani Dar es salaam, kwa kuzungumza na Mabalozi wa mashina. Ziara ya Dokta Migiro iliyobeba kauli mbiu isemayo ShinaLakoLinakuita, tayari imeshafanyika katika wilaya ya Temeke, Kigamboni, Ubungo na Kinondoni na kesho itafanyika wilayani Ilala kwa kuzungumza pia na Mabalozi wa mashina katika ukumbi wa Diamond Jublee. Katika ziara yake Katibu Mkuu wa CCM, anazungumzia zaidi nguvu ya wanachama walioko katika mashina, matawi, huku akisisitiza nafasi ya wazee katika kutoa elimu ya itikadi kwa vijana Siku ya kwanza ya ziara, akizungumza na mabalozi wa mashina wa Wilaya za Temeke na Kigamboni katika kikao kazi kilichofanyika ukumbi wa PTA uliopo Sabasaba jijini Dar es Salaam, Dokta Migiro, alisema kuna kila sababu ya kuhakikisha Chama Cha Mapinduzi kinazingatia utaratibu wa kusikiliza maoni na ushauri kuanzia ngazi ya chini badala ya u...