Skip to main content

Posts

Showing posts from July 23, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mkuu Amaliza Ziara Belarus, Anadi Fursa za Uwekezaji

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa ametumia ziara yake nchini Belarus kunadi fursa za uwekezaji katika maeneo manne ya kipaumbele ya Serikali ya awamu ya sita ambayo ni kilimo, afya, madini na ulinzi & usalama. Mhe. Waziri Mkuu katika siku mbili za ziara yake,  tarehe 22 na 23 Julai 2025 ametembelea kampuni kubwa nane zenye nguvu ya mitaji jijini Minsk na kuzihakikishia utayari wa Serikali ya Tanzania kushirikiana nazo kwa kuzipatia kila aina ya msaada zitakapokuja Tanzania kuwekeza. Kwenye eneo la kilimo, Mhe. Waziri Mkuu alikutana na viongozi wa Waziri Mkuu Amaliza Ziara Belarus, Anadi Fursa za Uwekezaji ya AFTRADE ambayo tayari ipo nchini na kuwasisitiza kuongeza kasi katika kuendeleza kilimo hususan kuwa na programu za kuwasaidia wakulima wadogo mitaji, utafiti na mafunzo ili kilimo  kiweze kuwa na tija, kizalishe ajira na kuongeza usalama wa chakula nchini. Katika eneo hilo la kilimo, Waziri mkuu pia alitembelea chuo cha...

Wanafunzi wadahiliwa papo hapo maonyesho ya vyuo vikuu nje ya nchi Dar

  Na Mwandishi Wetu MAMIA ya wanafunzi wanaotaka kusoma kozi mbalimbali nje ya nchi wamejitokeza kwenye maonyesho ya vyuo vikuu nje ya nchi ambapo wengi wamepata udahili wa papo kwa papo. Maonyesho hayo yaliyofanyika jana jijini Dar es Salaam  na kushirikisha vyuo zaidi ya 20 kutoka nchi mbalimbali yanatarajia kufanyika tena kwenye mikoa ya Dodoma na Arusha hivi karibuni. Hayo yalisemwa jana kwenye maonyesho hayo jijini Dar es salam  na Mkurugenzi wa wakala wa Elimu Nje ya nchi, Global Education Link, Abdulmalik Mollel. “Tulitarajia tuanze saa nne asubuhi lakini tulipofika tu saa moja tukakuta utitiri wa wanafunzi hata kabla hatujafungua kwa hiyo kwa kweli mwitikio umekuwa mkubwa sana wanafunzi wamekuja kwa wingi sana na wengi wamepata udahili,” alisema Mollel aliwataka watanzania wanaotaka kusomea nje ya nchi kuchangamkia ufadhili unaotolewa na vyuo mbalimbali ambavyo vinatoa ufadhili kwa asilimia mia moja.  Alisema kwenye maonyesho hayo na ambayo yanakwenda kufanyi...

Lukuvi Aipongeza Wizara ya Nishati Kutekeleza Azma ya Serikali ya Kuhamia Katika Mji wa Serikali Mtumba

📌 *Aishukuru Wizara kwa kumheshimisha Dkt.Samia Suluhu Hassan* 📌 *Ampongeza Dkt. Biteko kwa kuweka msukumo wa Watumishi kuhamia Mtumba* Wizara ya Nishati imepongezwa kwa kuhamia rasmi katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma ambapo Idara na Vitengo vyote vya Wizara sasa vimeshahamia katika jengo la Wizara lililopo katika Mji huo wa Serikali. Pongezi hizo zimetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge  na Uratibu, Mhe. William Lukuvi wakati alipotembelea jengo la Wizara katika Mji wa Serikali Mtumba ambapo alipokelewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba, Naibu Katibu Mkuu, Dkt. James Mataragio pamoja na Menejimenti ya Wizara. "Nakupongeza sana  Katibu Mkuu kwa hatua hii, pamoja na Mkandarasi wa Jengo  na Msimamizi, pia nawapongeza kwa nia thabiti ya kuhamia katika Mji huu wa Serikali baada ya Mhe. Rais Samia kutoa fedha zilizowezesha ujenzi wa majengo haya Serikali Mtumba".  Amesema Mhe. Lukuvi Ameongeza kuwa, nia ya Rai...

Rais Mwinyi:Hayati Mzee Mkapa ni Mfano Wa Kuigwa Kwa Mchango Wake

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameeleza kuwa Hayati Mzee Mkapa atabaki kuwa mfano wa kuigwa kwa kizazi cha sasa na kijacho kutokana na mchango wake mkubwa katika kujenga misingi ya maendeleo, utawala bora na ustawi wa Taifa. Amesisitiza kuwa Serikali ya Awamu ya Tatu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilijenga nguzo muhimu za umoja wa kitaifa, Muungano, amani na mshikamano wa Watanzania, pamoja na nafasi ya Tanzania katika bara la Afrika na ulimwenguni. Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Ibada Maalum ya Kumbukumbu ya Miaka Mitano ya Hayati Benjamin William Mkapa, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, iliyofanyika leo tarehe 23 Julai 2025 Lupaso, Wilaya ya Masasi, Mkoa wa Mtwara. Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amekumbusha kuwa Hayati Mzee Mkapa alikuwa muumini wa ujamaa na uchumi wa soko unaoongozwa na sekta binafsi, lakin...