Skip to main content

Posts

Showing posts from January 7, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Halmashauri Zitoe Tenda Kwa Vikundi Vya Mikopo Ya Asilimia 10 Ili Kuongeza Wigo wa Ajira - Prof. Shemdoe

Na OWM TAMISEMI - Tanga Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI) Mhe. Prof. Riziki Shemdoe amezitaka Halmashauri kuvipa kipaumbele vikundi vya wanawake, vijana na wenye ulemavu vilivyonufaika na mikopo ya aslimia 10 kwa kuvipatia kazi (tenda) ili kuongeza wigo wa ajira kwa wananchi. Prof. Shemdoe ametoa maelekezo hayo hivi karibuni, akiwa jijini Tanga katika Uwanja wa Tangamano, mara baada ya kukagua shughuli za vikundi vya wajasiriamali walionufaika na mikopo ya asilimia 10 mkoani Tanga na kuvikabidhi vikundi hivyo hundi ya mikopo ya asilimia 10 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.761. “Nimeona kikundi cha vijana kilichokopeshwa na kuanzisha mradi wa kufyatua tofali na kimeweza kuajiri vijana wengine, hivyo nazielekeza Halmshauri zenye miradi ya ujenzi kutoa tenda kwa vikundi vya vijana kama hiki cha uzalishaji wa tofali,” Prof. Shemdoe amesisitiza. Prof. Shemdoe ameongeza kuwa, amejionea kikundi kingine kilichokopeshwa na kuanzisha kam...

Katibu Mkuu Ccm Dk.Migiro Aunguruma Dar… Atoa Maelekezo Utoaji Maelekezo

-Pia azungumzia nguvu ya wanachama walioko katika mashina,matawi -Asisitiza nafasi ya wazee katika kutoa elimu ya itikadi kwa vijana KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.Asha-Rose Migiro amesema kuna kila sababu ya kuhakikisha Chama hicho kinazingatia utaratibu wa kusikiliza maoni na ushauri kuanzia ngazi ya chini badala ya utaratibu wa maelekezo kutoka juu kwenda chini. Akizungumza mbele ya mamia ya mabalozi wa mashina wa Wilaya za Temeke na Kigamboni katika kikao kazi kilichofanyika ukumbi wa PTA uliopo Sabasaba jijini Dar es Salaam,Dk.Migiro ametumia kikao hicho kutoa rai kwa viongozi na wana CCM kuzingatia utaratibu wa kutoa maoni kuanzia ngazi ya chini kwenda juu. “Nitoe mwito kwa viongozi wetu tusifanye utaratibu wa kutoa amri kutoka juu kushuka chini maana uongozi mzuri ni lazima uanzie chini kwenda juu.Yale tunayoyapata kutoka kwenye mashina , matawi ndio yatapanda juu kwa lengo la kukiimarisha chama chetu. “Tusikilize kutoka chini kupanda juu tusiwe wa kutoa amri kutoka ...

Mining Commission Highlights Investment Opportunities At Zanzibar International Trade Fair

📍ZANZIBAR, January 7, 2026 The Mining Commission, in collaboration with various Government institutions and private sector stakeholders, is actively participating in the ongoing 12th Zanzibar International Trade Fair being held at Fumba, Zanzibar, to showcase a wide range of investment opportunities available in Tanzania’s mining sector. The exhibition, held under the theme “Building Inclusive Growth through Trade and Innovation,” has provided a platform for the Mining Commission to promote opportunities in mineral exploration, mining, mineral processing and trading, as well as the supply of goods and services to mining operations. A large number of Zanzibar residents have visited the Commission’s pavilion to learn about the contribution of the mining sector to national development, particularly its role in boosting Gross Domestic Product (GDP), employment creation and individual income growth. Mining Commission experts have outlined Tanzania’s strategic direction in strengthening sus...

Mabalozi wa Ccm Waagizwa Kuacha Kutegemea Amri za Juu

Asisitizwa kuwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) amri zinazotolewa ngazi ya chini zina uzito na zinapaswa kuheshimiwa. Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, amewataka Mabalozi wa mashina kuacha tabia ya kusubiri amri kutoka juu badala ya kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia mamlaka waliyopewa. Amesema kuwa wanaotekeleza majukumu yao kwa ufanisi katika ngazi ya chini ndio nguzo muhimu ya uhai na uimara wa chama. Dkt. Migiro ametoa kauli hiyo leo tarehe 7 Januari 2026, wakati akianza ziara yake ya kukutana na Mabalozi wa mashina katika wilaya za Temeke na Kigamboni, jijini Dar es Salaam. Akizungumza mbele ya maelfu ya Mabalozi hao, Dkt. Migiro alimpongeza Mwenyekiti wa CCM Taifa, Ndugu Kenani Kihongosi, kwa uongozi wake mahiri wa mkoa wa Dar es Salaam, pamoja na kuratibu ziara zilizolenga kutoa elimu na kuhamasisha wanachama kuhusu umuhimu wa kushiriki kikamilifu katika shughuli za chama. Akiweka mkazo katika suala la maadili na uimara wa CCM, Dkt. Migiro alisema kuwa cha...

Tume ya Madini Yaangazia Fursa za Uwekezaji Maonesho ya Kimataifa Zanzibar

ZANZIBAR, Januari 07, 2026 Tume ya Madini kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za Serikali na sekta binafsi inashiriki kikamilifu katika Maonesho ya 12 ya Biashara ya Kimataifa Zanzibar yanayoendelea katika eneo la Fumba, Zanzibar, kwa lengo la kutangaza fursa lukuki za uwekezaji zilizopo katika sekta ya madini nchini. Maonesho hayo yanaongozwa na kaulimbiu isemayo “Kujenga Ukuaji Jumuishi Kupitia Biashara na Ubunifu,” ambapo Tume ya Madini imeweka mkazo katika kuonesha fursa za utafiti wa madini, uchimbaji, uchenjuaji na biashara ya madini, pamoja na utoaji wa huduma na bidhaa kwenye migodi. Katika banda la Tume, wananchi wengi wa Zanzibar wamejitokeza kupata elimu kuhusu mchango wa sekta ya madini katika maendeleo ya taifa, hususan katika kuongeza pato la Taifa, ajira na kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja.  Wataalam wa Tume wameeleza mwelekeo wa Tanzania katika kuimarisha uchimbaji endelevu wa madini na kuongeza thamani ya rasilimali hizo, sambamba na sera, kanuni na mifumo rafik...

Mabadiliko Makubwa Uhamiaji,Simbachawene apendekeza wasomee utalii

Agusia kigezo cha elimu ili uajiriwe Uhamiaji Na Mwandishi Wetu,ZANZIBAR Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imedhamiria kuiboresha Idara ya uhamiaji ikiwa ni mpango mkakati wa kuendelea kuboresha sekta ya utalii ambayo imeliingizia taifa watalii Milioni Moja Laki Tisa Ishirini na Nne Elfu  na Mia Mbili Arobaini kwa mwaka 2024 huku kwa  mwaka 2025 watalii Milioni Mbili Tisini na Saba Elfu na Mia Nane Ishirini na Tatu ikiwa ni ongezeko la watalii Laki Moja Sabini na Tatu Elfu  na Mia Tano Themanini na Tatu. Akizungumza katika Kikao na Uongozi wa Juu,Maafisa Waandamizi na askari wa Idara ya Uhamiaji Visiwani Zanzibar, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,George Simbachawene amesema Maafisa Uhamiaji ni watu muhimu nchini kwa kuwa ndio watu wa kwanza mtalii au mgeni anapoingia nchini ndio anakutana nao ambapo amewataka kuwa wakarimu pindi wanapotoa huduma kwa wageni ikiwemo watalii ambao uliingizia Taifa kiasi kikubwa cha fedha ikikadiriwa Shilingi za Kitanzania Trilion...