Skip to main content

Posts

Showing posts from March 28, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Mbunge Mathayo Awatembelea Wahanga Musoma Mjini

Mbunge wa Jimbo la Musoma Mjini Mhe Vedastus Mathayo Leo 28/03/2025 amewatembelea wahanga wa mvua ilionyesha juni 23 na kusababisha maafa makubwa katika mitaa ya mjini, Manispaa ya Musoma Mkoani Mara.  Mhe Mathayo amewapa pole watu wote waliofikwa na athari ya mvua na kuwaomba kuwa watulivu huku serikali ikianza kuyafanyia kazi Mambo mbalimbali ikiwemo kuwalipia Wananchi waliokuwa  wapangaji kwenye miji iliyokumbwa na ghasia hiyo ili waendelea na maisha kama kawaida. Mbunge huyo kwa kushirikiana na mamlaka za serikali wikaya na mkoa wamechukua hatua mbalimbali katika kuhakikisha wananchi hao wanapata msaada na kuendelea na maisha yao kama kawaida. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye ni mfaraji namba moja ametoa milioni mia moja kwa ajili ya wananchi 300 waliokubwa na janga hilo huku kamati ya maafa ofisi ya waziri mkuu ikiendelea na tathimini ili kujua ukubwa wa tatizo hilo na hatua za kuchukua. Katika tukio hilo nyumba za wananchi,baadhi ...

Serikali Yaagiza Magereza Kupewa Ruzuku ya Nishati Safi ya Kupikia

📌 Dkt. Biteko atoa mabati 300 ujenzi wa darasa Chuo cha Mafunzo 📌 Magereza yapongezwa kutumia Nishati Safi ya Kupikia 📌 Dkt. Samia apongezwa kwa kuimarisha vyombo vya ulinzi na usalama Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameilekeza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kutoa ruzuku kwa Jeshi la Magereza ili kutekeleza maelekezo ya Serikali kuhusu matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia na kuhakikisha  Magereza yote yanaondokana na Nishati isiyo safi. Dkt. Biteko ametoa agizo hilo leo Machi 28, 2025 jijini Dar es salaam katika hafla ya kufunga Mafunzo ya Uongozi  Ngazi ya Juu  Namba 27 - 2024/2025  katika Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCTA). “ Magereza yote 129 yamehama katika matumizi ya kuni na sasa yanatumia nishati safi ya kupikia. Naielekeza REA ile ruzuku tunayopanga kuitoa kwa wazalishaji mbalimbali kwa ajili ya vifaa vya matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia Magereza wapewe kipau...

Wasira Awahakikishia Wakulima Shinyanga Ccm itaendelea Kutatua Changamoto zao

Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira amewahakikishia wananchi wilayani Kishapu, Mkoa wa Shinyanga  Chama hicho kitaendelea kutatua changamoto zao ikiwemo ya kuhakikisha wanapata mazao mengi ya kilimo kwa kusambaza pembejeo na kujenga miundombinu muhimu. Wasira ameeleza hayo leo Machi 28, 2025 alipokuwa akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM wilayani humo akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 na kusikiliza changamoto za wananchi pamoja na kuhutubia mikutano ya hadhara mkoani Shinyanga. Wasira alihitimisha ziara yake ya siku tatu mkoani Shinyanga na kuanza ziara kama hiyo mkoani Simiyu.

Waziri Mavunde Asisitiza Miradi Mikubwa ya Madini Iliyopewa Leseni Kuanza Kazi Haraka

📍 *Dodoma* Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, ameagiza Miradi Mikubwa na ya Kati ya madini ambayo tayari imekwishapewa leseni kuanza utekelezaji wake mara moja ili kuchochea ukuaji wa sekta na kuleta manufaa kwa taifa kwa ujumla na kutimiza azma ya Serikali kutoa leseni hizo. Amesema hayo, leo Machi 28, 2025 Jijini Dodoma wakati akizungumza katika Mkutano maalum na Chemba ya Migodi Tanzania (TCM) kwa lengo kujadili masuala mbalimbali yanayohusu Sekta ya Madini ili kuboresha uendelezaji na usimamizi wa shughuli za uchimbaji na biashara ya madini kwa manufaa ya sekta na taifa kwa ujumla, ikiwa ni sehemu ya ratiba yake ya kukutana na makundi yote yayojihusisha na mnyororo mzima wa Sekta ya Madini nchini Waziri Mavunde amesema Serikali inataka kuhakikisha kuwa Miradi yote ya Uchimbaji Madini iliyopangwa kuanza inaanza mara moja bila kucheleweshwa, na kuwa Serikali kwa upande wake imejitahidi kurahisisha taratibu kwa wawekezaji na sasa ni wakati wa Sekta binafsi kuchukua hatua kwa upa...

Mkuu Wa Majeshi ya Ulinzi Nchini Jenerali Mkunda Ahitimisha Zoezi la Uvishaji wa Nishani

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda amehitimisha zoezi la uvishaji nishani kwa  kuwavisha Nishani mbalimbali Maafisa na Askari wa JWTZ Kanda ya Mtwara leo tarehe 28 Machi 2025. Rais na Amiri Jeshi Mkuu kwa kutumia madaraka aliyopewa chini ya kifungu cha 4 cha Sheria ya Shughuli za Rais,Sura ya 9,Toleo la Urekebu la mwaka 2002 alitunuku nishani mbalimbali ambapo Jenerali Mkunda amevalisha nishani hizo kwa niaba yake. Miongoni mwa waliovishwa nishani hizo leo ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Kanali Michael Mangwela Mntenjele . Akizungumza baada ya kuvisha nishani hizo, Jenerali Mkunda amewapongeza Maafisa na Askari waliotunukiwa nishani hizo kwa namna Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan alivyotambua mchango wao katika kulitumikia Taifa kwenye nyanja ya Ulinzi. Aidha,amewataka Maafisa na Askari kuendelea kuviishi viapo vyao na kuhakikisha mipaka yote ya nchi yetu inakuwa salama...

Makamu wa Rais Azindua Matawi Mawili ya Benki ya Nmb

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema kufunguliwa kwa matawi ya Benki karibu na wananchi kutasaidia kuondokana na wakopeshaji binafsi maarufu kama kausha damu ambao licha ya kutoza riba kubwa, wananyanyasa na kutweza utu kwa vitendo vya ukamataji mali za wadaiwa.   Makamu wa Rais amesema hayo mara baada ya kuzindua Tawi la Benki ya NMB Chanika na Tawi la Benki ya NMB Kinyerezi Jijini Dar es Salaam. Amesema uzinduzi wa matawi hayo ya Benki utachangia maendeleo ya Taifa kwa kulipa kodi mbalimbali na kutoa ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja. Hali kadhalika, amesema tawi la Benki hiyo litawezesha kufanyika kwa usalama zaidi wa miamala mbalimbali kama vile malipo ya bili za maji na umeme, ada za shule na mauzo ya bidhaa mbalimbali.   Makamu wa Rais ametoa wito kwa Benki ya NMB kuendelea kushiriki katika kutatua changamoto mbalimbali za kijamii ikiwemo katika sekta ya Afya na Elimu. Amesema uwajibikaji kwa ja...