Skip to main content

Posts

Showing posts from March 21, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Tuwapende, Tuwajali na Tuwatunze Wanafunzi Wenye Mahitaji Maalum - Majaliwa

  _▪️Asema kwa kufanya hivyo kutawasaidia kutimiza ndoto zao_ _▪️Asisitiza Serikali itaendelea kufanya uwekezaji kwenye sekta ya elimu_ Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa wito kwa wanafunzi wa shule zote nchini kuwatunza, kuwapenda na kuwajali wanafunzi wenzao wenye mahitaji maalum ili nao waweze kutimiza ndoto zao. Amesema Serikali imejenga miundombinu bora ambayo sasa inawawezesha wanafunzi wenye mahitaji maalum kusoma na kufaulu na kupata nafasi katika shule mchanganyiko na hivyo ni wajibu wa wanafunzi wengine kuwapenda na kuwasaidia. "Nimevutiwa namna mnavyowajali na kuwapenda wanafunzi wenzenu wenye mahitaji maalum, ninaomba muendelee na upendo huo muwathamini na kuwapenda ili nao watimize ndoto zao". Ameyasema hayo leo, (Jumamosi Machi 22, 2025 ) alipotembelea Shule ya Sekondari ya Mkoa ya Wasichana ya Njombe iliyoko Wilaya ya Wanging'ombe Mkoani Njombe. Mheshimiwa Majaliwa amesema pamoja na mambo mengine ameridhishwa na ujenzi na mandhari ya shule hiyo na zaidi ame...

Dc Chikoka Ahimiza Ulipaji wa Bili za Maji Kwa Wakati

  Na Shomari Binda-Musoma  MKUU wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka amehimiza wananchi na taasisi mbalimbali kulioia bili zao kwa wakati ili kuisadia Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Musoma ( MUWASA) kutekeleza majukumu yake. Amesema wakati serikali imejidhatiti kuhakikisha inawafikishia wananchi huduma ya maji ya uhakika mjini na vijijini ni muhimu kulipia huduma. Kauli hiyo imetolewa jana machi 21,2025  katika kilele cha Wiki ya Maji 2025 kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa manispaa ya Musoma. Akizungumza na wenyeviti wa mitaa 73 ya manispaa hiyo na wadau mbalimbali wa huduma za maji amesema kwa manispaa ya Musoma zaidi ya asilimia 95 wananchi wamefikiwa na huduma ya maji na kudai hilo ni jambo jema na kuishukuru serikali. Amesema Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Musoma( MUWASA) imefanya kazi nzuri ya usimamizi wa mradi mkubwa wa maji Bukangc ulioghalimu zaidi ya bilioni 45 zilizopelekea kuwafikishia wananchi huduma. Chikoka amesema mradi huo li...

Mbunge Wa Muheza Azindua Mradi wa Maji Wenye Thamani ya Milioni 679

 📍 Ni mradi utakaowanufaisha wakazi wa Kijiji cha Kwatango  📍 Asema ni kazi nzuri za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan  📍 Amtaja Waziri Jumaa Awesso kwa kutekeleza miradi mingi Muheza 📍 Awataka wananchi waoneshe shukrani zao kwa kuwaunga mkono  NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamisi Mwinjuma maarufu MwanaFA, amezindua mradi wa maji katika Kijiji cha Kwatango wenye thamani ya shilingi milioni 679. Akizindua mradi huo kwenye uwanja wa Kijiji cha Kwatango kilichopo kata ya Kwemingoji wilayani Muheza, MwanaFA alisema mradi huo ni matunda yaliyofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika miradi mingi ya maji nchini ikiwemo wilaya ya Muheza. Alisema mradi huo ni kati ya miradi 17 iliyopo wilayani Muheza ambayo inashughulikiwa na Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) na inagharimu kiasi cha shilingi bilioni 8.4. fedha zote zilizotolewa kwa ajili ya miradi ya maji wilayani Muheza ni shilingi bilioni 11.890. Alisema wanamshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan wa...

Waziri Mkuu Akifurahia Jambo wa Watoto Kutoka Morogoro

 WAZIRI MKUU mh Kassim Majaliwa akifurahia jambo na Mtoto Jackline Eliadi wa Darasa la Tano kutoka Shule ya Msingi Maninga, Tarafa ya Turiani, Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro baada ya kutoa elimu kuhusu nishati safi na Utunzaji wa Mazingira mkoani Njombe Machi 21, 2025 Wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Misitu Duniani na Upandaji Miti Kitaifa yaliyofanyika Mkoani Njombe.

Waliokamatwa na Madini ya Milioni 18 Mkoani Kagera Wafikishwa Mahakamani

  Na Angela Sebastian; Kyerwa  Washitakiwa wanane wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kyerwa, mkoani Kagera kwa mara ya kwanza kujibu mashtaka yanayowakabili ya  uhujumu uchumi, ambapo walikamatwa wakiwa na madini ya bati yenye thamani ya zaidi ya milioni 18 bila kibali. Raymond Kimbe ni wakili wa Serikali mwandamizi kwa kushirikiana na Alfred Tairo wakili wa Serikali na Duke Mwanguku  Mwendesha mashitaka akisoma shauri hilo namba 6758/2025 yenye mashtaka matano  yanayowakabili washitakiwa namba moja mpaka sita  mbele ya hakimu mkazi mwandamizi Allen Ifunya.  Kimbe amesema  washitakiwa hao kwa pamoja wanadaiwa mnamo Februari 11 mwaka huu katika eneo la Mulongo Wilayani humo walikutwa na madini aina ya bati yenye uzito wa kilo 310 yenye thamani zaidi ya milioni 13 kinyume cha sheria  Washtakiwa hao ni Diana Dickson Antoni,Dickson Antoni,Deusi Daud,Benjamin Ernest, Alfred Ntiba na Brighton Sadiel ambao wanashitakiwa kwa makosa matano ikiw...

Balozi Nchimbi: Malezi ya Walimu ni Muhimu Katika Ujenzi wa Taifa Imara

_Atoa wito kwa viongozi wa dini kuiombea Tanzania dhidi ya vurugu_ Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amesema malezi na mafunzo wanayopata wanafunzi shuleni, hasa yanayosisitiza nidhamu na uwajibikaji, ni msingi muhimu katika kujenga taifa imara lenye uzalendo. Aidha, ametoa wito kwa viongozi wa dini na madhehebu mbalimbali kuendelea kuiombea Tanzania ili iendelee kuwa na amani na kuepuka athari za watu wanaotaka kuingiza nchi katika vurugu. Balozi Nchimbi aliyasema hayo wakati wa kikao cha umoja wa wanafunzi waliosoma Shule ya Sekondari ya Uru Seminari, kilichofanyika Moshi, mkoani Kilimanjaro, baada ya ibada na mazishi ya aliyewahi kuwa Baba Gombera wa seminari hiyo, Padri Canute Mkwe Shirima AJ, mnamo Machi 20, 2025. “Hakuna aliyesoma Uru Seminari asiyetambua mchango wa kipekee wa Padri Shirima. Tulifundishwa nidhamu, uwajibikaji, bidii kazini, na umuhimu wa kufuatilia mambo kwa umakini. Mafundisho hayo yametufanya kuwa watumishi bora katika...

Mbunge Muhongo Ahamasisha Upandaji wa Miti

Na Shomari Binda-Musoma  MBUNGE wa jimbo la Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo ametoa wito kwa wananchi na taasisi za umma na binafsi kufika bustani ya miche ya miti TFS kuchukua na kupanda kipindi hiki cha mvua. Katika taarifa yake iliyotolewa leo machi 21,2025 kupitia ofisi yake amesema miche ya kivuli,mbao na matunda imeoteshwa ya kutosha kupitia TFS hivyo ni wakati wa kuchukua na kupanda. Muhongo amesema miti ina umuhimu mkubwa katika utunzaji wa mazingira na kulinda uoto wa asili kwenye maeneo Amesema kupitia bustani hiyo iliyopo Musoma mjini miche hiyo inatolewa bure hivyo hakuna sababu za kutochukua na kupanda Mbunge huyo amesema kwa taasisi zikiwemo shule za msingi na sekondari wanatakiwa kupeleka maombi kwenye halmashauri ili waweze kusaidiwa usafiri wa kufikisha miche hiyo kwenye maeneo yao. " Upandaji wa miti ina umuhimu mkubwa katika utunzaji wa mazingira ili kuondokana na ukame ni wito wangu kwa taasisi na wananchi tukachukue na kupanda. " Pale kwenye busta...

Tanzania na Japan Kushirikiana Ukuzaji Ujuzi Kwa Vijana

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Ardhi, Miundombinu na Utalii wa Japan Mhe. Kenichi Ogasawara kuhusu kuimarisha ushirikiano katika masuala ya ukuzaji ujuzi na teknolojia kwa vijana. Mhe. Ridhiwani amebainisha hayo Machi 21, 2025 Jijini Dodoma alipokutana na ujumbe kutoka nchini Japan. Aidha, amesema kupitia programu ya ukuzaji ujuzi inayotarajiwa kuanzishwa baina ya nchi hizo mbili italeta tija kwa vijana kuweza kujiajiri au kuajiriwa kupitia ujuzi watakaoupata kutoka nchini Japan. Katika hatua nyingine Mhe. Ridhiwani amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. DKt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kufungua mipaka nje ya nchi ili kutoa fursa kwa watanzania kupata kazi nje ya nchi. Naye Naibu Waziri wa Ardhi, Miundombinu na Utalii wa Japan Mhe. Kenichi Ogasawara amesema kuwa Tanzania ni moja ya Nchi ya kipaombele katika program hiyo ya mashirikiano ya ukuza...