Skip to main content

Posts

Showing posts from January 24, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mkuu Kuzindua Kanzidata na Mfumo Wa Taarifa Za Wenye Ulemavu

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Januari 25 2025 atazindua Kanzidata na Mfumo wa Taarifa za Watu Wenye Ulemavu Unaotokana Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022, kwenye Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma Mfumo huo utawezesha wadau wa maendeleo, na watunga sera katika kupanga, kutekeleza, na kufuatilia maendeleo ya Watu Wenye Ulemavu Nchini Pia, Takwimu zilizoandaliwa zinatoa taarifa za msingi ikiwemo idadi ya watu wenye ulemavu kwa jinsi na umri, aina ya ulemavu, kiwango cha elimu na aina ya shughuli za kiuchumi wanazojishughulisha nazo.

Yericko Nyerere ampongeza Lissu na Kumchambua Mbowe

  Na Yericko Nyerere Uchaguzi umeisha, demokrasia imeshinda! Nafanya maachilio mema kutambua na kuthamini demokrasia ya kisiasa hasa katika ardhi ya ubwa. Nilisimama wima kumuunga mkono Mh Mbowe, tumeshindwa katika sanduku la kura kidemokrasia kabisa   Kwamsingi huohuo wa kidemokrasia ya siasa za vyama, Ninapongeza uongozi mpya chini ya Mwenyekiti Mh Tundu Lissu kwasababu umepatikana kwa njia ya kidemokrasia ya haki, uwazi na ukweli. Ndio demokrasia ina pande mbili, upande wa furaha na upande wa huzuni, muda wa huzuni umeisha sasa ni muda wa ushindi wa taasisi yetu. Lakini, Niseme nini juu ya Mtu huyu Mh Freeman Mbowe? Hakika nitaandika kurasa milioni na bado sitamaliza kumuelezea na kumheshimisha. Wewe ni Kiongozi, Wewe ni Mwalimu, Wewe ni Baba, Wewe ni Kaka, Wewe ni Rafiki na wewe ni alama ya makuzi mema. Umejenga taasisi imara ya kidemokrasia, umeiishi demokrasia, na umeiishi kwa vitendo halisi kwa kuchagua kuwa ndio mlango wetu imara wa kuingia na kutokea! Nimejiuliza...

Yericko Nyerere ampongeza Lissu na Kumchambua Mbowe

Na Yericko Nyerere Uchaguzi umeisha, demokrasia imeshinda! Nafanya maachilio mema kutambua na kuthamini demokrasia ya kisiasa hasa katika ardhi ya ubwa. Nilisimama wima kumuunga mkono Mh Mbowe, tumeshindwa katika sanduku la kura kidemokrasia kabisa   Kwamsingi huohuo wa kidemokrasia ya siasa za vyama, Ninapongeza uongozi mpya chini ya Mwenyekiti Mh Tundu Lissu kwasababu umepatikana kwa njia ya kidemokrasia ya haki, uwazi na ukweli. Ndio demokrasia ina pande mbili, upande wa furaha na upande wa huzuni, muda wa huzuni umeisha sasa ni muda wa ushindi wa taasisi yetu. Lakini, Niseme nini juu ya Mtu huyu Mh Freeman Mbowe? Hakika nitaandika kurasa milioni na bado sitamaliza kumuelezea na kumheshimisha. Wewe ni Kiongozi, Wewe ni Mwalimu, Wewe ni Baba, Wewe ni Kaka, Wewe ni Rafiki na wewe ni alama ya makuzi mema. Umejenga taasisi imara ya kidemokrasia, umeiishi demokrasia, na umeiishi kwa vitendo halisi kwa kuchagua kuwa ndio mlango wetu imara wa kuingia na kutokea! Nimejiuliza sana, ...

Mbwa Afisa wa Jeshi aliyefuzu

  Pichani ni mbwa afisa wa jeshi, msomi, Jasusi na Komandoo aliyefuzu mafunzo ya kimedani ya kijeshi na ana force number.  Anaitwa "K9 police dog" ni aina maalumu ya mbwa wa kijeshi wanaotumika katika misheni maalum ikiwemo kubaini vilipuzi, madawa ya kulevya, wahalifu na kushambulia wahalifu wanaojaribu kutoroka mkono wa sheria. Mbwa hawa hawali mabakibaki wala viporo. Hawa sio wale mbwa koko wetu wanaokula hadi chips. Mbegu maarufu za mbwa hawa (kitaalam ikiwa na maana ya Breeds) ni aina ya German Shepherd, Dutch Shepherd na Belgian Mulinois. Hawa mbwa mmoja kibongo anauzwa sio chini ya milioni 5 hadi 10. Fikiria mbwa ni afisa wa serikali alafu wewe kazi huna yaani upo upo tu mtaani hata kujiajiri hutaki unapiga tu soga na kubeti Mungu akusaidie Aisee 🤣

Wavuvi 540 Waokolewa, 10 Wanatafutwa Ziwa Rukwa

Wavuvi 540 waliokuwaa wanafanya shughuli za Uvuvi katika Ziwa Rukwa wameokolewa na Wavuvi 10 wanaendelea kutafutwa kufuatia upepo mkali uliotokea mnamo tarehe 23 Januari 2025 katika ziwa Rukwa Wilayani Sumbawanga Mkoani Rukwa. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amefika Kata ya Nankanga kuungana na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dkt. Ashatu Kijaji kujionea kazi ya uokozi huku akiwa ameambata na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji CGF John Masunga pamoja na Askari Wazamiaji. Kwa Upande wake, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dkt. Ashatu Kijaji ametoa pongezi kwa Wananchi kwa kushiriki kikamkalifu katika uokoaji pamoja na kutoa ushirikiano wa kuwatambua wavuvi wengine ambao walikuwa hawajasajiliwa katika Vikundi na makampuni. Mkuu wa wilaya ya Sumbwanga Nyakia Chirukile ameelewa kuwa mnamo tarehe 23 Januari 2025, Jumla ya Wavuvi 550 kutoka Kata ya Nankanga na Mtowisa waliokuwa wanaendelea na shughuli za Uvuvi katika ziwa Rukwa walipatwa na dhoruba ya upepo mkali kat...

Daraja La Jp Magufuli (Kigongo-busisi ) Lafikia Asilimia 96.3, Kukamilika Februari 2025

Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega amesema Daraja la JP MAGUFULI (Kigongo-Busisi), linalounganisha mkoa wa Mwanza na Geita, linatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu. Akikagua Ujenzi wa Daraja hilo leo tarehe 24 Januari 2025 mkoani Mwanza, Waziri Ulega amemshukuru na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa zaidi ya shilingi bilion 611 kugharamia daraja hilo hadi sasa. " Mheshimiwa Rais Dkt. Samia amelikuta daraja hili ujenzi wake ukiwa asilimia 25 na kiasi cha shilingi bilioni 150 zikiwa zimelipwa leo hii tuko asilimia 96.3 na zaidi ya shilingi bilioni 611 zimelipwa katika daraja hili ambalo ni refu zaidi Afrika Mashariki litawezesha watu kuvuka kwa dakika 5", amesema Waziri Ulega. Amewapongeza wataalam wazalendo kwa kujifunza katika mradi huo na kusisitiza ujuzi walioupata ni hazina kwa Taifa na utawawezesha kupewa miradi mingine ya aina hiyo siku zijazo. "Fanyeni kazi usiku na mchana ili kazi ikamilike mkat...

Ushirikiano kati ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji na Wakurugenzi wa Halmashauri chachu ya usimamizi wa miradi ya Umwagiliaji nchini-Waziri Bashe

 ðŸ“ŒNa NIRC ;DODOMA Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, amehimiza ushirikiano kati ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri, katika kusimamia miradi ya Umwagiliaji nchini. Amesema Tume inatekeleza mradi wa Mifumo Himilivu ya Chakula nchini(TFSRP) lengo ni kuongeza uzalishaji wa chakula kutosheleza ndani ya nchi na kuilisha dunia,hivyo kuwapo na ushirikiano na Halmashauri.   Aidha amesisitiza kuwa katika utekelezaji wa mradi huo Tume imenunua zaidi ya Magari 17 na mitambo kwaajili ya uchimbaji wa Visima 56,000 vya Umwagiliaji na kuboresha miundombinu ya Umwagiliaji kwa lengo la kufikia adhina ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuongeza uzalishaji wa chakula.  “Magari hayo yanatarajiwa  kuwasili kuanzia Machi mwaka huu, ambapo mawili kati ya hayo yatakuwa na uwezo kuchimba visima virefu zaidi”, amesema Bashe Waziri Bashe amesema Tayari serikali imeshatangaza kandarasi ya kuchimba visima hivyo na tumepata wakandarasi kwa ajili ya kuanza kufa...