Skip to main content

Posts

Showing posts from December 4, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Rc Daniel Chongolo atoa wito kwa Mawakala wa Forodha Tunduma kujiepusha na fedheha

  Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Daniel Chongolo, amekutana na kufanya mazungumzo na mawakala wa forodha katika mpaka wa Halmashauri ya Mji wa Tunduma, tarehe 28 Novemba 2024, ofisini kwake iliyopo Nselewa, wilayani Mbozi. Katika kikao hicho, Mhe. Chongolo ametoa wito kwa mawakala wa forodha kujiepusha na vitendo vyovyote vinavyoweza kuwasababishia fedheha. Aidha, mesisitiza na kuacha na na vitendo vitakavyo waingiza matatani Mazungumzo hayo yamelenga kutafuta suluhisho la changamoto za foleni za malori katika mpaka wa Tunduma, ambazo zimekuwa zikiathiri ufanisi wa shughuli za forodha na usafirishaji. Mkuu wa Mkoa amehimiza ushirikiano wa dhati baina ya wadau wote katika kuboresha huduma mpakani na kuimarisha uchumi wa mkoa na taifa kwa ujumla. Kikao hicho kimehudhuriwa na mawakala wa forodha na wadau wengine wa forodha, ambao walipata nafasi ya kutoa maoni na mapendekezo yao kuhusu changamoto zinazowakabili.

Tarura yarejesha km 74.7 za Miundombinu Hanang

  Hanang, Manyara  Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Wilaya ya Hanang imefanikiwa kurejesha miundombinu ya barabara iliyoathiriwa na mafuriko ya tope, magogo na mawe  mwishoni mwa mwaka 2023. Meneja wa TARURA Wilaya ya Hanang, Mhandisi Paul Mlia amesema kwamba jumla ya Km. 74.7 ziliathirika zenye jumla ya madaraja 14, kati ya barabara hizo Km 19.7 ni za Katesh mjini na Km 55 ni barabara za pembezoni mwa mlima Hanang.“Serikali kupitia TARURA  ilifanya tathimini ya uharibifu uliojitokeza katika miundombinu hiyo ili kurejesha haraka huduma kwa wananchi”, alisema. Aidha, amesema maeneo mengine yaliyoathirika ni maeneo ya kijamii ikiwemo nyumba za Ibada, soko la kateshi na makazi ya wananchi ambapo utekelezaji wake wa muda mfupi walifanikisha uondoaji wa mawe, tope, magogo na kurejesha mawasiliano katika barabara ya kateshi mjini yenye urefu wa Km 19.7 pamoja na uondoaji wa matope ndani ya nyumba za wananchi 61. "Kwa upande  wa wilaya ya Hanang tulipe...

Waziri Kombo azuru Makumbusho ya Louvre ya UAE

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mahmoud Thabit Kombo ametembelea Makumbusho ya Louvre iliyoko Abu Dhabi katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Mhe. Waziri Kombo ametembelea Makumbusho hayo ambayo ni jumba la sanaa lililopo kwenye Kisiwa cha Saadiyat jijini Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu tarehe 03 Desemba, 2024 na kujionea jinsi jumba hilo lilivyohifadhi na kuelimisha kwa namna ya kipekee katika mazingira ya kisasa inayodhihirisha na kutafakarisha juu ya utawala, maarifa na ustadi wa ufundi wa utamaduni wa watu na viongozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu.  Makumbusho ya Jumba hilo la Louvre inaendeshwa  chini ya makubaliano kati ya UAE na Ufaransa yaliyosainiwa Mwaka 2007, yanayoruhusu kutumia jina la Louvre hadi mwaka 2047.  Makumbusho ya Louvre inaelezwa kuwa ni mradi mkubwa zaidi wa kitamaduni wa Ufaransa ulioko nje ya nchi hiyo.

Wahasibu Afrika Waaswa Kuisimamia Ukweli wa Taaluma yao

📌 Dkt. Biteko Amwakilisha Rais Samia Kufunga Mkutano AAAG 📌 Asema Afrika Inawategemea Wahasibu Kunufaika na Utajiri wake 📌 Asisitiza Matumizi ya Teknolojia kwa Wahasibu Afrika Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko amewaasa wahasibu barani Afrika kuisimamia taaluma yao kikamilifu ili kuendeleza umuhimu na mchango na ukuaji wa uchumi duniani. Ameyasema hayo Disemba 04, 2024 wakati akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kufungaji Mkutano wa Pili wa Jumuiya ya Wahasibu Wakuu wa Nchi za Afrika (AAAG) uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC). “ Nataka niwaombe wahasibu mtambue kuwa taaluma yenu ni muhimu hata chochote kinachotokea katika sehemu zenu za kazi mtalaumiwa, hivyo mzuie hasara zinazoweza kutokea," amesema Dkt. Biteko. Amewaasa  kusimamia taaluma yao kwa kuzingatia misingi ya kitaaluma hata kama uamuzi wao unaweza kuwa na gharama“ ...

Waziri Mkuu awasili Viwanja vya Kawawa Kumwakilisha Dkt. Mpango Mahafali ya 43 ya Chuo Kikuu Huria

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Desemba 05, 2024 amemwakilisha Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango kwenye Mahafali ya 43 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yanayofanyika katika viwanja vya Kawawa, Mkoani Kigoma. Mahafali hayo pia yanahitimisha maadhimisho ya miaka 30 tangu chuo hicho kianze kutoa mafunzo mwaka 1994.

Waziri Kikwete ashiriki Uzinduzi wa Mipango ya Haki Kwa Wenye Ulemavu

Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu kazi,Ajira na wenye ulemavu Mh Ridhwani Kikwete,amepata nafasi ya kumsindikiza Mh. Dotto Biteko , Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Tanzania kwenye uzinduzi wa Mpango Kazi wa Taifa wa Haki na Ustawi wa Watu Wenye Ualbino ( MTHUWWU) na Mkakati wa Taifa wa Teknolojia Saidizi katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar Es Salaam.  Mipango hii miwili ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025, maelekezo na ahadi ya Mh. Rais Dr. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa akihutubia Bunge kuhusu kuwalinda watu wenye Ualbino nchini. #KaziInaendelea

Tanzania & Umoja wa Mataifa Waratibu Kikao cha Washirika wa Maendeleo Comoro

Ubalozi wa Tanzania na Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Comoro wameratibu mkutano wa washirika wa maendeleo wa Comoro ulioshirikisha Balozi zote na Taasisi za Kimataifa zenye uwakilishi nchini Comoro na wengineo walioshiriki kwa njia ya mtandao kutokea Nairobi. Akizungumza katika Mkutano huo, Balozi wa Tanzania nchini Comoro Mhe. Saidi Yakubu ambaye alikuwa Mwenyekiti Mwenza alieleza hatua mbali mbali ambazo Serikali ya Tanzania kupitia ubalozi inazifanya ikiwemo kuvutia wawekezaji, kushiriki katika utoaji wa huduma za afya na kuratibu wafanyabiashara wa Comoro wanaokwenda Tanzania na pia kuomba ushirikiano zaidi wa pamoja ili kusaidiana na Serikali ya Comoro katika kuharakisha maendeleo yake. Kwa upande wake, Mwenyekiti Mwenza ambaye pia ni Mratibu Mkati wa Umoja wa Mataifa Comoro, James Tsok Bot aliishukuru Tanzania kwa kukubali uratibu wa mkutano huo unaolenga kujenga uelewa wa pamoja katika wadau wa maendeleo ya Comoro. Mkutano huo umeshirikisha nchi za Marekani, L...