Skip to main content

Posts

Showing posts from April 25, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt. Mwigulu Akagua Maendeleo ya Ujenzi wa Madaraja ya Mkwajuni na Kigogo, Dar es salaam.

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba leo Aprili 26, 2026 anafanya ziara katika mkoa wa Dar es Salaam ambapo amekagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Mkwajuni lenye urefu wa mita 20 na kimo cha mita 5.5 ambalo hadi kukamilika kwake litagharimu shilingi bilioni 11.6 Pia Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amekagua mradi wa ujenzi wa Daraja la Kigogo lenye urefu wa mita 50 kimo cha mita 8.9 na barabara unganishi zenye jumla ya urefu wa mita 625 ambalo hadi kukamilika kwake litagharimu shilingi bilioni 17.7.

Mbunge Ghati Asisitiza Umuhimu wa Kuwa na Vyama Vya Ushirika Vyenye Nguvu

MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Mhe. Ghati Zephania Chomete, amesisitiza umuhimu wa kujenga vyama vya ushirika vyenye msingi wa uadilifu, uwazi na uwajibikaji ili kuchochea maendeleo ya wanachama na Taifa kwa ujumla. Akizungumza leo Jijini Dodoma katika Mkutano wa Wadau wa Maendeleo ya Ushirika pamoja na Uzinduzi wa Kampeni ya Uadilifu katika Ushirika, Mhe. Chomete ambapo amemwakilisha Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, amesema kuwa ushirika usiposimamiwa kwa misingi sahihi unakosa tija inayokusudiwa. “Vyama vya ushirika vinapaswa kujengwa katika misingi ya uwazi na uadilifu, huku usimamizi thabiti ukiwa kipaumbele ili wanachama wanufaike ipasavyo,” amesema Mhe. Chomete. Ameongeza kuwa pamoja na usimamizi mzuri, vyama hivyo vinapaswa kuwajengea wanachama uwezo kupitia mafunzo ya kisasa ya biashara, masoko na usimamizi wa fedha ili viweze kuendana na ushindani wa kiuchumi wa sasa. “Ni muhimu kwa wanachama kupewa maarifa na stadi za kisas...

Waziri Mkuu Ashiriki Ibada ya Jumapili Katika Kanisa la Kkkt (Dmp), Usharika wa Azania Front

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameshiriki ibada ya Jumapili, leo, Aprili 26, 2026, katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani (DMP), Usharika wa Azania Front, jijini Dar es Salaam. Ibada hiyo iliongozwa na Katibu wa Umoja wa Utume wa Injili (United Evangelical Mission - UEM) Kanda ya Afrika, Dkt. Ernest Kadiva, kwa kushirikiana na Mchungaji Kiongozi wa KKKT Usharika wa Azania Front, Victor Makundi.

Rais Samia Azindua Meli ya Kwanza ya Uvuvi wa Bahari Kuu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amezindua meli ya kwanza ya uvuvi wa bahari kuu ya Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), akisema hatua hiyo ni msingi muhimu katika kuimarisha mchango wa sekta ya uvuvi kwenye uchumi wa taifa. Uzinduzi huo umefanyika leo Jumamosi Aprili 25, 2026, katika hafla iliyofanyika Kigamboni jijini Dar es Salaam, ambapo Rais Samia ameeleza kuwa uwekezaji huo unaakisi dhamira ya serikali katika kutekeleza sera na mikakati ya kukuza uchumi wa buluu. Amesema meli hiyo si chombo cha kuvulia samaki pekee, bali ni sehemu ya mfumo mpana unaounganisha uzalishaji wa ndani, uvuvi wa kisasa pamoja na masoko, hatua itakayosaidia kuongeza tija na thamani ya rasilimali za bahari kuu. Aidha, Rais Samia amebainisha kuwa serikali imejipanga kuliimarisha Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) ili liweze kushiriki kikamilifu katika usimamizi wa rasilimali za bahari kuu na kuhakikisha manufaa yake yanawanufaisha Watanzania. Katika hatua nyingine, ame...

Mawaziri Wajadili Udhibiti wa Silaha na Usalama wa Kikanda

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobass Katambi, ameshiriki mkutano kwa njia ya mtandao wa Kamati Ndogo ya Mawaziri ya Kikanda ya Udhibiti wa Silaha ndogo na nyepesi katika Ukanda wa Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika (RESCA). Mkutano huo umewakutanisha mawaziri wa usalama kutoka nchi wanachama, ukilenga kujadili hali ya usalama katika ukanda huo pamoja na changamoto zinazoendelea kujitokeza, hususan usambazaji na matumizi haramu ya silaha ndogo na nyepesi. Nchi zilizoshiriki mkutano huo ni pamoja na Tanzania, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Rwanda, Uganda, Kenya, Somalia, Sudan, Sudan Kusini, Ethiopia, Eritrea na Djibouti, ambapo zimejadili kwa pamoja masuala ya udhibiti wa silaha na mapambano dhidi ya biashara haramu ya silaha. Akizungumza baada ya mkutano huo, Waziri Katambi amesema serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imejipanga kimkakati kuimarisha ulinzi na usalama kwa kuboresha mifumo ya udhibiti wa uingizaji silaha nchini. Ameeleza kuwa hatua hizo ...

Makamu wa Rais Aongoza Kikao Cha Pamoja Cha Serikali za SMZ na Sjmt

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ameongoza kikao cha Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) ya kushughulikia Masuala ya Muungano kilichofanyika katika Ukumbi wa Golden Tulip Zanzibar. Makamu wa Rais amewapongeza viongozi na wataalamu wote walioshiriki katika kikao hicho kwa jitihada walizofanya wakati wa maandalizi na majadiliano. Katika kikao hicho Hoja ya Uingizaji wa Sukari kutoka Zanzibar katika Soko la Tanzania Bara imeridhiwa na kuondolewa katika orodha ya Hoja za Muungano, ambapo imeshuhudiwa kusainiwa kwa Hati ya makubaliano ya kuondoa Hoja hiyo katika orodha ya Hoja za Muungano ambayo ni miongoni mwa hoja nne za Muungano zilizokuwa zimesalia. Kikao hicho kimehudhuriwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, Waziri Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano n...