Skip to main content

Posts

Showing posts from April 24, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Spika BWZ ataka Watanzania wauenzi Muungano kwa kushiriki uchaguzi

Na MASHAKA MHANDO, Pangani  SPIKA wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar Zubeir Ali Maulid, amewataka Watanzania wauenzi na kuulinza Muungano kwa kushiriki uchaguzi Mkuu ujao kwa kuchagua viongozi sahihi. Akizungumza Leo April 25 baada ya kukagua na kuzindua madarasa sita ya shule ya sekondari ya Bushiri wilayani hapa, alisema Muungano ni tunu iliyoasisiwa na viongozi hivyo hakuna budi kuulinda kwa nguvu zote. Alisema Watanzania wanapoazimisha miaka 61 ya Muungano, wanatakiwa kukumbuka faida na fursa zilizotokana na Muungano huo lakini pia kutazama namna ya kuepuka chokochoko zenye viashiria vya kuvunja Muungano huo. "Wote hapa zaidi ya asilimia 80 tuliopo hapa tumezaliwa ndani ya Muungano hivyo tunayo sababu kubwa ya kuenzi, kuulinda kwa kushiriki uchaguzi Mkuu ujao ili tuwapate viongozi wetu," alisema na kuongeza, "Tunapoadhimisha maadhimisho ya miaka 61 ya Muungano wetu tunatakiwa tukumbuke faida na fursa zilizopatikana kupitia Muungano wetu,". Akizungumza kuhusu s...

QATAR kushirikiana na NEMC kupambana na gugu vamizi ziwa Victoria

Na Mwandishi Wetu BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kupitia Ubalozi wa Tanzania nchini Qatar wamefanya mazungumzo yenye lengo la kuanzisha ushirikiano katika masuala mbalimbali ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi pamoja na kubadilishana uzoefu. Ushirikiano huo pia utahusu eneo la uhifadhi wa Ziwa Victoria hususani katika kufanya tafiti kuhusu  uondoshwaji wa gugu maji vamizi lililoshamiri kwa sasa Akizungumza na ujumbe kutoka Tanzania n chini QATAR, Katibu Mkuu wa Wizara ya  Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi wa nchini Qatar, AbdulAziz Ahmad Abdullah Al-Mahmoud alisema  majukumu ya kisheria ya Wizara yake ya mazingira yanafanana na majukumu ya NEMC. Alisema kutokana na hali hiyo  kuna kila sababu ya kushirikiana hasa katika suala la usimamizi wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi. Naye Balozi wa Tanzania nchini Qatar,  Habibu Awesi Mohammed aliishukuru NEMC na Mamlaka za maji kutoka Dar es Salaam, Dodoma na Mtwara kwa kuonesha u...

RC Batlida ataka ukarabati soko la Ngamiani uharakishwe

 MASHAKA MHANDO, Tanga  MKUU wa mkoa wa Tanga, Balozi Dkt Batlida Burian ameiagiza halmashauri ya Jiji la Tanga, kuharakisha ukarabati wa soko la Ngamiani ili mvua zinazoendelea kunyesha zisiharibu bidhaa za wafanyabiashara. Akizungumza katika soko hilo jana, alipofika kukagua na kuona shughuli za wafanyabiashara hao, Dkt Batlida pia aliagiza mkandarasi anayekarabati soko hilo awe na wafanyakazi wa kutosha ili kazi hiyo isichukue muda mrefu. "Mkurugenzi hakikisheni kazi ya ukarabati inakwenda kwa haraka, mnajua kipindi hiki ni cha mvua lazima tulinde bidhaa za wafanyabiashara wetu, hakikisheni mnakuwa na wafanyakazi wa kutosha ikibidi tunaweza kuongeza wafungwa ili soko likamilike kwa haraka," alisema Mkuu wa mkoa. Mkuu wa mkoa aliwataka wafanyabiashara wawe watulivu katika kipindi hiki cha matengenezo na kwakuwa soko linakarabatiwa huku wakiendelea kuuza bidhaa zao basi wasiwe kikwazo kwa wafanyakazi wa mkandarasi. Alimwagiza Mkurugenzi pia kuhakikisha wafanyabiashara wa sok...

waziri mkuu kufanya ziara ya siku moja nansio-ukerewe mkoani mwanza

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Aprili 25, 2025 amewasili mkoani Mwanza ambapo ataelekea Nansio-Ukerewe kwa ziara ya siku moja. Akiwa katika kisiwa hicho Mheshimiwa Majaliwa atakagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali yenye hadi ya Huduma za Rufaa ya Mkoa, ataweka jiwe la msingi la jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe pamoja na kufanya mkutano wa hadhara utakaofanyika katika uwanja wa Getrude Mongela. 

Naibu Waziri Mkuu Dkt. Biteko Akemea Migogoro Arusha

-Dkt. Doto Biteko Ataka Viongozi Kuweka Mbele Maslahi Ya Wananchi Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewataka viongozi kote nchini kuweka maslahi ya wananchi mbele na kuacha migogoro inayotokana na ubinafsi wao. "Hawa Watanzania hawataki migogoro yetu sisi viongozi na wakati mwingine migogoro tuliyonayo ni migogoro ya maslahi binafsi. Tumeacha kuwahudumia wananchi tunashughulikiana, tunataka huyu akwame, huyu afanikiwe kwa sababu tuna cartel (makundi)," amesema Dkt. Biteko  Akizungumza Aprili 24, 2025 Mundarara, Wilayani Longido, Dkt. Biteko amesema kuwa amani ndiyo msingi wa utoaji huduma bora  "Tunataka watu waungane, wafanye kazi ya pamoja. Hakuna kitu kinachotia aibu kama unakuta kiongozi umepewa nafasi mahali fulani ama wewe una cheo mahali fulani badala ya kuzungumza shida za watu unawazungumza watu, Huyu kwako mbaya, yule mbaya, huyu mbaya, Wewe ukiulizwa uzuri wako huna cha kuonesha."  Amesisitiza kuwa viongozi waliopata nafasi wa...

Wasira: Demokrasia Sio Vurugu

*Ataka isitumike kuchochea shari kama wanavyofikiri baadhi ya wanasiasa.* Na Mwandishi Wetu, Kongwa MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara Stephen Wasira, amesema maana ya demokrasia ni majadiliano, hoja na maelewano kwa lengo la kuimarisha umoja na ushirikiano katika kujenga taifa. Amesema demokrasia sio vurugu kama ambavyo baadhi ya wanasiasa hususan wa vyama vya upinzani wanavyofikiri na kupiga kelele kutaka shari jambo ambalo CCM haikubaliani nalo. Wasira alieleza hayo leo wilayani Kongwa Mkoa wa Dodoma akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 ikiwa sehemu ya shughuli za kuelekea maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 61 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliozaa Tanzania ambao uliingiwa Aprili 26, mwaka 1964. "Kama una hoja za kuwashawishi wapigakura wakukubali toa, kama huna kubali....kwa sababu hawana watu, uchaguzi wa serikali za mitaa wameshindwa kwa sababu hawana wagombea, sasa wanalalamika tumeibiwa mumeibiwa wapi? ...

Balozi Nchimbi: Wajumbe wa Ccm Kura za Maoni Sikilizeni Wananchi

_Asisitiza CCM daima itaenzi misingi ya Nyerere_ Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amesema CCM itahakikisha inateua wagombea wazuri wanaokubalika kwa wapiga kura, akiwataka wajumbe wa vikao vya kura za maoni kusikiliza maoni ya wananchi wanapoenda kupiga kura. Halikadhalika, Balozi Nchimbi ametoa wito kwa Watanzania wote, hususan wenye sifa za kupiga kura, kuwapatia maoni yao wajumbe wa vikao hivyo vya uchujaji wagombea wa CCM, ili wanapoenda kupiga kura za maoni wachague wagombea wanaokubalika katika jamii pana ya wapiga kura wa Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba, mwaka huu. Balozi Nchimbi amesema hayo alipozungumza na wananchi wa Butiama, katika eneo la Nyamisisi, aliposimama kuwasalimia wakati akiendelea na ziara ya kikazi ya siku tano katika Mkoa wa Mara, leo Alhamis tarehe 24 Aprili, 2025, ikiwa ni siku ya tatu ya ziara hiyo. “Napenda kuwahakikishia kuwa CCM daima itaendelea kujinasibisha na misingi ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere. Kamwe ...

Ongezeko la Mapato Namanga Lamkosha Dkt. Biteko

📌Ailekeza TANESCO kufunga Kituo cha Kupoza Umeme Longido 📌Maelekezo ya Serikali yatekelezwa Longido 📌Amuagiza Makonda kusimamia ufungaji vifaa vya maabara Sekondari ya Longido Samia Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameeleza kufurahishwa kwake na ongezeko la ukusanyaji wa mapato katika kituo cha huduma za pamoja mpakani mwa Tanzania na Kenya cha Namanga. Akizungumza Aprili 24, 2025 Namanga mkoani Arusha wakati katika ziara yake ya kutembelea miradi ya maendeleo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 61 ya Muungano Dkt. Biteko ameipongeza Mamlaka ya Mapato Tanzania Kituo cha Namanga kwa kufanya kazi kwa ufanisi. “ Nimefurahishwa sana na urahisi wa biashara na kila eneo limekuwa na ukuaji wa watu na bidhaa kwenye kusafirisha nje ya nchi ili kuleta fedha ya kigeni zitakazowezesha kufanya shughuli zingine nawapongeza sana, nawashukuru kwa kuwa na malengo makubwa ya kukusanya shilingi bilioni 124 na hadi kufi...