Skip to main content

Posts

Showing posts from July 25, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

POLISI KATAVI YAFANYA MATENDO YA HURUMA

 Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi limefanya matendo ya huruma kwa kutoa m saada wa vitu mbalimbali kwa wagonjwa waliopo katika kituo cha afya Ilembo kilichopo Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi. Akikabidhi msaada huo Julai 25, 2026 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Kaster Ngonyani amebainisha kuwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi kama sehemu ya jamii limeona ni vyema kufanya matendo ya huruma na kutoa faraja kwa wagonjwa hao ili wasijione wapweke. Msaada uliotolewa kwa wagonjwa hao ni pamoja na taulo za kina mama, pempasi, sabuni, sukari, unga, mafuta ya kupaka, maji, juice, mafuta ya kupikia, miswaki na dawa za meno pamoja na kuchangia damu. Akipokea msaada huo Mganga Mfawidhi kituo cha afya Ilembo Dr. Veneranda Musati amelishukuru Jeshi la Polisi kwa msaada huo na kutoa wito kwa jamii kuiga mfano huo kwa kuwa na moyo wa kusaidia wahitaji.

WANANCHI WA BUKOMBE WAIPONGEZA SERIKALI KWA UTEKELEZAJI WA MIRADI MIKUBWA YA MAENDELEO*

*▪️Waziri Mavunde akagua soko na stendi ya kisasa ya Shilingi bilioni 22 Ushirombo* *▪️Mradi wa maji Businda-Buntubili kunufaisha wakazi 9949* *▪️Wachimbaji wamshukuru Rais Samia kwa ugawaji wa Leseni* *▪️Ujenzi wa barabara-Uyovu na kituo cha polisi na zahanati katika eneo la machimbo ya Msasa wapongezwa* Bukombe, Geita Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, ameendelea na ziara yake ya kukagua na kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo mkoani Geita kwa kutembelea miradi mbalimbali katika Wilaya ya Bukombe, huku akisisitiza umuhimu wa kukamilika kwa miradi hiyo kwa wakati ili wananchi waanze kunufaika na huduma zinazotarajiwa. Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara, Waziri Mavunde amesema serikali chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuleta miradi mingi ya maendeleo ili kupeleka huduma za msingi kwa wananchi. Awali, Waziri Mavunde alikagua mradi wa maji katika Kijiji cha Businda, Kata ya Bulangwa, wenye...

RIDHIWANI KIKWETE: CHALINZE IWE MFANO WA UTEKELEZAJI WA DIRA YA TAIFA 2050

 WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete, amefanya kikao kazi na madiwani pamoja na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, akisisitiza umuhimu wa ushirikiano na uwajibikaji katika kuharakisha utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Kikao hicho kiliwahusisha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, Ndg. Ramadhani Possy, Wakuu wa Idara, Maafisa Tarafa, Watendaji wa Kata pamoja na madiwani, ambapo walijadili kwa kina namna bora ya kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia vipaumbele vya maendeleo vilivyowekwa na Serikali. Akizungumza katika kikao hicho,kilichofanyika wilayani chalinze Mhe. Kikwete amesema mafanikio ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 yanategemea kwa kiwango kikubwa utendaji wenye weledi, uwajibikaji na ushirikiano wa viongozi na watumishi katika ngazi zote za Serikali.  " Halmashauri zina nafasi muhimu ya kutafsiri dira hiyo kwa vitendo kupitia utekelezaji wa miradi ya maendeleo n...

KUANZIA SASA WATAKAONG'ATWA NA NYOKA MUHEZA KUTIBIWA BURE

 📍Ni baada ya MwanaFA kutoa fedha za kugharamia matibabu hayo MUHEZA:  MBUNGE wa Muheza na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma, maarufu kama 'MwanaFA', ametekeleza ahadi yake kwa kutoa chupa 99 za dawa ya kutibu sumu ya nyoka (antivenom) zenye thamani ya shilingi milioni 15, ili ziweze kutolewa bure kwa wananchi. Mhe. Mwinjuma amekabidhi dawa hizo Julai 24, wakati wa kikao cha ndani cha wana CCM wa Kata za Tongwe na Nkumba, na kueleza kuwa hatua hiyo ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa wakati wa kampeni mwaka jana. "Mganga Mkuu, niliahidi kwamba endapo wananchi wa Muheza watanichagua tena, dawa za sumu ya nyoka nitazitoa ili wananchi watibiwe bure. Leo nakukabidhi chupa hizi 99 zenye thamani ya shilingi milioni 15," alisema Mhe. Mwinjuma. Wilaya ya Muheza, yenye jumla ya vijiji 126 na kata 37, imezungukwa na mazingira ya misitu ambayo hupelekea wananchi kung'atwa na nyoka mara kwa mara wanapokuwa katika shughuli zao za mashamban...