Na Mwandishi Wetu, Muheza MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Muheza kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hamisi Mwinjuma maarufu MwanaFA amesema endapo atachaguliwa kuwa mbunge wananchi wa kata ya Lusanga na Muheza kwa ujumla wataweka maji ya bomba nyumbani kwao badala ya kuchota kwenye vilula. Akizungumza katika mkutano wa kampeni katika kata ya Lusanga, MwanaFA alisema kuwa tatizo la maji Muheza kabla hajakuwa mbunge, wilaya hiyo ilikuwa na shida ya maji kubwa lakini Sasa kuna ahueni ya kutosha. Alisema kata ya Lusanga pekee ilipata kiasi cha shilingi milioni 700 kwa ajili ya miradi ya maji ambayo ilipunguza tatizo hilo kwa wananchi. Aliwahakikishia wananchi hao kwamba fedha zaidi za maji zitakuja wilayani humo kupitia mradi wa Green Bond ambao umechangiwa kiasi cha shilingi bilioni 100 kwa ajili ya miradi ya maji mkoa wa Tanga na Muheza utashughulikia kiasi cha kilomita 15 ili maji yawe majumbani. "Tunataka ndani ya miaka mitano ijayo sehemu ya Lusanga Kila mtu ameweka maji nyumbani...
Marato tv - Sauti ya Jamii