Skip to main content

Posts

Showing posts from December 12, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Ujenzi wa Jengo la Kituo cha Mafunzo ya Kuongeza Thamani Madini ya Vito Waanza Jijini Arusha

  ■ Ni mkakati wa kuhakikisha madini vito yanaongezewa thamani nchini. ■Ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais.Dkt. Samia katika kuendeleza mnyororo wa madini thamani. ■Waziri Mavunde amtaka mkandarasi kuongeza nguvukazi kukamilisha mradi kwa wakati. ▪️Atoa siku 7 kwa Katibu Mkuu kukutana na wakandarasi,TGC na Taasisi za serikali kwa ajili ya upatikanaji vibali muhimu vya kuendeleza ujenzi. *Arusha* Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amemtaka mkandarasi wa ujenzi wa kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) kukamilisha ujenzi wa majengo ya kituo cha mafunzo ya Uongezaji thamani madini ya vito kwa kuongeza nguvukazi na kufanya kazi kwa masaa 24 ili kukamilisha ujenzi wa jengo kwa muda mfupi. Waziri Mavunde ameyasema hayo leo Desemba 12, 2025 mkoani Arusha wakati wa ziara yake ya kukagua mradi wa kituo hicho ulioanza ujenzi rasmi ambapo katika maelekezo yake amemtaka mkandarasi kuzingatia ujenzi bora wenye kukidhi vigezo vilivyoainishwa kwenye mkataba. Waziri Mavunde amefafanua kuwa, Serika...

Ndugu Wawili Wafikishana Mahakamani Kutaka Haki ya Kumtunza Mama yao Mzazi

 Ndugu wawili nchini Saudi Arabia walipeleka kesi mahakamani kuhusu mama yao. Lakini hapa ndipo jambo linapovutia — haikuhusu urithi, bali ni nani atakayemtunza mama yao. Watu wengi hudhani kwamba ndugu wakifika mahakamani basi lazima iwe ni mgogoro wa ardhi au urithi. Lakini hadithi hii ya kweli kutoka Saudi Arabia ni tofauti kabisa na inagusa moyo sana. Mzee mmoja anayeitwa Hizam Al-Ghamdi alijikuta amesimama mahakamani dhidi ya ndugu yake mdogo, na hawakupigania mali, bali kila mmoja wao alisisitiza apewe jukumu la kumtunza mama yao mzee na dhaifu. Hizam alisisitiza kwa nguvu kwamba angependa kuendelea kumtunza mama yake kama alivyokuwa akifanya siku zote, akisema kwamba mama yake ndiye uhai wake. Lakini ndugu yake mdogo hakukubaliana naye, akiamini kuwa Hizam mwenyewe tayari alikuwa mzee na alikuwa anahitaji kupumzika. Ukweli ni kwamba mahakama ilijawa na hisia wakati ndugu hao wawili walipokuwa wakimlilia hakimu wapewe heshima ya kumtumikia mama yao. Hakimu, akiwa hana uhakika...

Simbachawene Awataja Lissu,Mbowe na Lema Msibani Kwa Jenista

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,George Simbachawene ameweka wazi umakini na uthubutu wa aliyekua Mbunge na Waziri aliyehudumu wizara mbalimbali,Marehemu Jenista Mhagama wakati wa Bunge lililokuwa na Upinzani mkali akiwataja baadhi ya waliopata kuwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwemo Godbless Lema,Freeman Mbowe na Dkt Wilbrod Slaa. Ameyasema hayo leo alipofika kutoa pole kwa wafiwa katika eneo la Itega jijini Dodoma ambapo viongozi mbalimbali pia walifika kutoa pole kwa familia na wafiwa.

Dkt. Nchimbi Kuweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Majengo ya Chuo Kikuu Cha Dar Es Saalam Tawi la Bukoba

  Na Angela Sebastian ;Bukoba Makamu wa Rais Mh  Dk.Emmanuel Nchimbi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uwekaji wa jiwe la msingi  tawi la chuo kikuu cha Dar es salaam tawi la Bukoba kinachojengwa  kata Kalabagaine  kijiji  Itahwa halmashauri ya wilaya ya Bukoba  Mkoani Kagera.  Mkuu wa mkoa huo Hajati Fatma Mwassa ameyaswma hayo wakati akiongea na waandishi wa habari  ofisini kwake ambapo amesema uzinduzi huo utafanyika Desemba 15 mwaka huu ambapo pia uzinduzi huo utaudhuliwa na Rais mstaafu wa hawamu ya nne Dk.Jakaya Mlisho Kikwete ambaye ni mkuu wa chuo hicho huku akieleza kuwa uwepo wa chuo hicho unakwenda kufungua fursa katika mkoa huo. Naibu mratibu wa mradi wa chuo hicho Profesa  Liberato Haule amesema chuo hicho endapo kitakamilika ,kitakuwa na uwezo wa kubeba wanafunzi  800 na awamu ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/2027 chuo kitapokea wanafunzi 660 awamu ya kwanza ambapo huku matarajio yao ifikapo 2030 wafikie wanafunzi 16...

Miradi ya Umwagiliaji Kukamilika kwa Wakati na Kuleta Tija kwa Wakulima-Chongolo

Na MWANDISHI WETU Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo amesema kuwa Serikali itahakikisha miradi yote ya Umwagiliaji inakamilika na kuleta tija kwa wakulima hali itakayoimarisha uchumi na kuleta uhakika wa chakula. Chongolo ameyasema hayo wakati kutembelea mradi wa Umwagiliaji uliopo Ndanda wilayani Masasi mkoani Mtwara ambapo amewahakikishia wananchi kuwa Serikali itakikisha miradi yote ya Umwagiliaji inakamilika na kuleta tija kwa wakulima. Mradi huo unahusisha ujenzi wa bwawa la Umwagiliaji na uchimbaji wa mifereji mirefu, na ukikamilika unatarajiwa kunufaisha zaidi ya wakulima 700 kutoka vijiji saba. “Serikali itahakikisha miradi yote ya Umwagiliaji inakamilika na kuleta tija kwa wakulima hali Serikali itahakikisha miradi yote ya Umwagiliaji inakamilika na kuleta tija kwa wakulima hali itakayoimarisha uchumi na kuleta uhakika wa chakula,amesisitiza. Amesema ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa bwawa hilo ambalo litachochea matumaini mapya kwa wakulima wa Mtwara kwa kuwawezesha kulim...