Skip to main content

Posts

Showing posts from November 4, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

WAZIRI MKUU AAGIZA TAASISI ZA UMMA ZITUMIE BIDHAA ZA NDANI

*_▪︎ Ataka mianya ya sheria inayokwamisha matumizi yake irekebishwe_* *_▪︎ Asisitiza kuheshimiwa kwa sekta binafsi na mitaji ya wawekezaji_* WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amezitaka taasisi za umma kutumia bidhaa zinazozalishwa nchini katika ujenzi, ununuzi wa samani na mahitaji mengine, akisisitiza kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kukuza viwanda, kulinda ajira na kuongeza mapato ya Taifa. Ametoa maelekezo hayo leo (Jumatano, Novemba 4, 2026), wakati akimwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uzinduzi wa Sera ya Maendeleo Endelevu ya Viwanda ya Mwaka 2025 na Sera ya Maendeleo ya Jasiriamali Ndogo na za Kati ya Mwaka 2003 (Toleo la Mwaka 2025), katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete, Dodoma. “Na jambo hili lianzie serikalini. Hata serikalini tunajenga majengo, tutumie bidhaa zinazozalishwa hapa nchini,” amesema. Dkt. Mwigulu ametaja vioo, nondo, marumaru na samani kuwa miongoni mwa bidhaa zinazozalishwa nchini ambazo taasisi za umma zinapaswa kutumia, akisisitiza kuwa Seri...

DRC YAFURAHISHWA NA UJENZI WA MJI WA SERIKALI MTUMBA

Uzoefu wa Tanzania katika ujenzi wa Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma umefungua ukurasa mpya wa ushirikiano wa maendeleo kati ya Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), baada ya nchi hiyo kueleza nia ya kutumia uzoefu huo katika kutekeleza mpango wa kujenga Mji wa Serikali katika mji mkuu wa Kinshasa. Waziri Mkuu wa DRC, Mhe. Judith Suminwa Tuluka, amesema Tanzania imekuwa mfano muhimu wa kujifunza katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati, akibainisha kuwa ziara yake katika Mji wa Serikali Mtumba imempa fursa ya kuona kwa vitendo namna mradi huo ulivyotekelezwa na jinsi unavyoweza kuwa rejea katika mipango ya nchi yake. Mhe. Judith ameyasema hayo leo, Novemba 4, 2026, jijini Dodoma, mara baada ya kutembelea Mji wa Serikali Mtumba na kukagua eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa Ubalozi wa DRC. Amesema ziara hiyo ni sehemu ya kunufaika na ushirikiano uliopo kati ya mataifa hayo mawili, ambao umekuwa ukitoa fursa ya kubadilishana uzoefu na kujifunza mbinu mbali...

MWAIMU AMKABIDHI MPELUMBE OFISI, ATOA WITO WA KUKAMILISHA MIRADI YA THBUB

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Mhe. Wakili Dunford George Mpelumbe amekabidhiwa Ofisi rasmi na mtangulizi wake Mhe. Jaji (mst.) Mathew P. M. Mwaimu katika hafla iliyofanyika katika Ofisi za Tume, Mtaa wa Makole Jijini Dodoma na kushuhudiwa na Katibu Mtendaji, Bw. Patience Ntwina leo Novemba 04, 2026. Mhe. Mwaimu, ambaye aliongoza Tume hiyo kuanzia mwaka 2019 hadi 2026, amemkabidhi ofisi Mhe. Mpelumbe aliyeteuliwa na kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan hivi karibuni. Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mhe. Jaji ( Mst) Mwaimu ametoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa ushirikiano na ushauri walioutoa, uliowezesha Tume kutekeleza majukumu yake ya kulinda na kutetea haki za binadamu pamoja na kusimamia misingi ya utawala bora nchini. Aidha, ameitoa wito kwa uongozi mpya wa THBUB kuendeleza na kukamilisha miradi aliyoiacha, ikiwemo kifuatilia ...

BUKOBA KUNUFAIKA NA NJIA NNE, SERIKALI YAZUNGUMZIA HATUA ZA UJENZI

Serikali imesema inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara za njia nne kuanzia eneo la Rwamishenye kwenda Kyakairabwa na Ibura mjini Bukoba, baada ya kukamilika kwa usanifu wa miradi hiyo. Kauli hiyo imetolewa leo Novemba 4,2026 Bungeni jijini na Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya wakati akijibu swali la Mbunge wa Bukoba Mjini Mhandisi Johnston Mutasingwa aliyehoji ni lini ujenzi wa barabara hizo utaanza, akieleza kuwa upembuzi yakinifu ulikuwa umekamilika. Katika majibu yake, Mha. Kasekenya amesema barabara hizo tayari zimefanyiwa usanifu na zitaingizwa katika mipango ya bajeti ili kuwezesha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wake. Awali, mbunge huyo ameishukuru Serikali kwa kukamilisha ujenzi wa barabara ya njia Nne kutoka Rwamishenye Roundabout hadi eneo la TRA, huku akitaka ufafanuzi kuhusu hatua zinazofuata za upanuzi wa miundombinu hiyo katika maeneo mengine ya Bukoba.

TEMESA TANGA YAZITAKA TAASISI ZA SERIKALI KUTOWASALITI.

Na Mwanamkuu Mwandoro,Tanga  TAASISI za serikali zinazotengeneza magari yake nje ya mfumo wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) zimetakiwa kuacha mara moja tabia hiyo kwani inasababisha upotevu mkubwa wa fedha kwa serikali . Akizungumza changamoto hiyo Meneja wa TEMESA Mkoa wa Tanga Mhandisi Riziki Lukali amesema y magari ya serikali yaliyosajoliwa kwaajili ya kufanyiwa matengenezo TEMESA ni zaidi ya 200 lakini yanayo kwenda kwao ni machache mno. Aidha Mhandisi Lukali ameongeza kuwa ili kutatua changamoto hiyo anahitaji kuonana na taasisi zote za serikali zinazofanya hivyo ili kujua changamoto ni nini na kutafuta suluhisho la kudumu. Sambamba na hayo Mhandisi Lukali pia ametoa onyo kali kwa gereji zote zilizopatiwa kibali cha kutengeneza magari ya serikali na badala yake kutumia vibaya vibali hivyo kwa kupokea magari bila kuwa na kibali cha gari husika. "Najua kuwa kuna gereji zinazotumia vibaya nafasi walipewa ya kupatiwa vibali vya kutengeneza magari ya serikali kwa ...

DCP LYIMO AHIMIZA MIRADI YENYE TIJA KWA WANACHAMA WA MTANDAO WA WANAWAKE

 Na Ssgt Mawazo Mtondo - DODOMA. Mwenyekiti wa Mtandao wa wanawake wa Jeshi la Magereza, Naibu Kamishna wa Magereza (DCP) Lipina Lyimo, leo Novemba 4, 2026, ameongoza kikao cha majumuisho ya tathmini ya Mkutano Mkuu wa Mtandao wa Wanawake wa Jeshi la Magereza, kilichowakutanisha washiriki kutoka Mkoa wa Dodoma. Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Msalato, jijini Dodoma. Akizungumza katika kikao hicho, DCP Lyimo amewashauri wanawake hao kupendekeza miradi yenye tija itakayoongeza thamani ya michango ya wanachama wa mtandao huo. Aidha, ameitaka Sekretarieti kupokea na kufanyia kazi maoni ya wanachama ili kuwezesha tathmini, majumuisho na maandalizi bora ya mkutano mkuu ujao. Kwa upande wake, Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Edith Mbogo amewataka washiriki kuzingatia usalama na faragha zao kwa kuepuka kurekodi na kusambaza picha binafsi kwenye mitandao ya kijamii. Ushauri huo ameutoa akishirikisha uzoefu alioupata wakati wa kuhudhu...

WAITARA AHOJI MKAKATI WA SERIKALI KUHUSU VITENDO VYA USHOGA NA USAGAJI

  MBUNGE wa Jimbo la Tarime Vijijini, Mhe. Mwita Waitara, amehoji mkakati wa Serikali katika kusimamia maadili kwa watumishi wa umma, akitaka kufahamu hatua zinazochukuliwa kukabiliana na vitendo vya ushoga na usagaji ambavyo amedai vinaanzia katika shule za msingi, sekondari na vyuo mbalimbali. Akizungumza Novemba 4, 2026, Bungeni jijini Dodoma, Waitara amehoji namna Serikali inavyohakikisha watumishi wanaoingia katika ajira za umma wanazingatia maadili yanayokubalika katika jamii. Akijibu swali hilo la nyongeza, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray, amesema Serikali inaendelea kusisitiza umuhimu wa maadili kwa watumishi wa umma katika utekelezaji wa majukumu yao. Amesema Serikali pia imeimarisha elimu ya maadili kupitia mabadiliko ya mtaala wa elimu kwa kuanzisha somo la Historia na Maadili, linalolenga kuwajengea watoto uelewa wa maadili ya Kitanzania tangu wakiwa katika umri mdogo.

KAZALA AISHAURI SERIKALI KUDHIBITI UPOTEVU WA MAPATO NA UBADHIRIFU WA FEDHA ZA UMMA

 MBUNGE wa Jimbo la Kasulu Vijijini Mheshimiwa, Edibilly Kazala ameishauri Serikali kuchukua hatua madhubuti kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato, kusimamia matumizi ya fedha na kuwachukulia hatua wote wanaohusika na vitendo hivyo. Akichangia hoja za Kamati ya LAK bungeni jijini Dodoma, Novemba 4, 2026, Mhe. Kazala amepongeza wajumbe wa kamati hiyo kwa kazi kubwa waliyoifanya, akisema wameitendea haki Serikali na wananchi kwa kuhakikisha fedha za umma, ikiwemo fedha zilizotolewa na Rais, zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa. Katika hoja yake, Kazala amegusia maeneo mawili muhimu, ukusanyaji wa mapato ya halmashauri na upotevu wa fedha za umma, akibainisha kuwa hali ya utegemezi wa halmashauri kwa Serikali Kuu ni kubwa kutokana na udhaifu wa mifumo ya ukusanyaji wa mapato ya ndani. Amesema ripoti ya kamati imeonesha zaidi ya asilimia 80 ya halmashauri zinategemea Serikali Kuu, huku halmashauri zote 184 zikiwa na wastani wa utegemezi wa zaidi ya asilimia 78, hali inayodhihirisha ku...

TANGA NA MKAKATI WA KUINUA ZAO LA MACHUNGWA

 NA: DK. REUBENI LUMBAGALA Mkoa wa Tanga ni maarufu kwa uzalishaji wa matunda nchini. Machungwa ni miongoni mwa matunda yanayozalishwa kwa wingi katika wilaya za Muheza, Korogwe na Handeni mkoani humo. Wakulima wa zao hili hufanya jitihada kubwa za uzalishaji, lakini bado hawajafaidi vya kutosha jasho lao. Wakulima hutegemea baada ya kuvuna, wauze machungwa kwa bei nzuri ambayo itarejesha gharama za uendeshaji. Aidha, wakulima hao hutegemea kupata faida kwani kwao kilimo hicho ni ajira kwa ajili ya kuendesha maisha yao na kufanya mambo mengine ya maendeleo kama kusomesha watoto, kujenga nyumba, kufungua biashara, kununua vyombo vya moto za usafiri, kutaja kwa uchache. Miongoni mwa changamoto katika kilimo cha machungwa ni bei ndogo na kukosa soko la uhakika. Hili limesababisha wakulima kuuza machungwa yao mashambani kwa madalali. Kwa kufanya hivyo, wakulima wamejikuta wakiuza machungwa yao kwa bei ndogo huku madalali wakinufaika pasi na kumwaga jasho kama walivyomwaga wakulima. Kut...

AGNES MARWA AHOJI BUNGENI MPANGO WA SERIKALI KUJENGA VIWANDA MARA

 MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Mara, Mhe. Agnes Marwa, amehoji mpango wa Serikali wa kuanzisha kongani za viwanda wilayani Bunda na Jimbo la Musoma Mjini ili kuongeza fursa za ajira na kukuza uchumi wa wananchi wa mkoa huo. Akiuliza swali hilo leo Novemba 4, 2026, Bungeni jijini Dodoma, Mhe. Agnes Marwa amesema Mkoa wa Mara una historia kubwa katika taifa kutokana na kuwa chimbuko la Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, lakini bado unakabiliwa na changamoto ya kutokuwa na viwanda vya kutosha. Amesema serikali inampango Gani kupeleka kongani za viwanda katika mkoa wa Mara ikiwemo wilaya ya Bunda na Jimbo la Msoma Mjini. Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dennis Londo amesema Serikali ina dhamira ya kuhakikisha Mkoa wa Mara unakuwa na viwanda vya kutosha vitakavyoongeza thamani ya mazao na rasilimali zinazopatikana mkoani humo na kutoa ajira kwa Watanzania. Amesema Serikali imeelekeza halmashauri kutenga asilimia tano ya mapato yake ya ndani kwa aj...