Skip to main content

Posts

Showing posts from September 2, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Bei ya Nishati ya Mafuta yashuka Nchini

 GMTV'-DODOMA  Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei kikomo za mafuta zinazotumika kuanzia leo Septemba 3, 2025, zikionesha kupungua kwa kwa shilingi 36 kwa bei ya petroli na shilingi 23 kwa bei ya dizeli kwa mafuta yaliyopokelewa bandari ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara mtawalia. Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt James Andilile, bei ya petroli katika soko la dunia imepungua kwa asilimia 0.2 %, dizeli kwa 5.5 % na mafuta ya taa kwa 3.5%. Vilevile, kwa bei za mwezi Septemba, 2025, wastani wa gharama za kubadilisha fedha za kigeni umepungua kwa 3.96% Gharama za kuagiza mafuta katika Bandari ya Dar es salaam zimeongezeka kwa wastani wa 20.73% kwa mafuta ya petroli, 7.75% kwa mafuta ya dizeli na 2.62% kwa mafuta ya taa; katika Bandari ya Mtwara hakuna mabadiliko, na kwa Bandari ya Tanga zimepungua kwa 12.66% kwa mafuta ya petroli na 12.66% kwa mafuta ya dizeli. Aidha, wafanyabiashara wanakumbushwa kuuza mafuta kwa bei zilizoi...

Bilioni 88 Zatolewa Miaka Minne ya Rais Samia, Kutekeleza Miradi ya Maendeleo Ngorongoro

. _Rc Makalla apokelewa kwa shangwe, akifanya ziara yake Wilayani Ngorongoro . Wananchi wamshukuru Rais Samia kwa miradi mingi ya maendeleo_  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla amefanya ziara ya Kikazi Wilayani Ngorongoro leo Jumanne Septemba 02, 2025, akimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania kwa kutoa zaidi ya Bilioni 88 kwaajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo Wilayani humo, ikiwemo Bilioni 18.9 zinazotekeleza miradi 17 ya Maji kwenye Kata mbalimbali za Ngorongoro. Mhe. Makalla ameyaeleza hayo mara baada ya kupokelewa Wilayani Ngorongoro na kuzungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, akimpongeza pia Mkuu wa Wilaya hiyo Brigedia Jenerali Wilson Christian Sakulo kwa kuongeza makusanyo kwenye sekta ya mifugo kutoka Shilingi Milioni 13 kwa mwaka hadi zaidi ya Milioni 200 na kusema fedha hizo zitasaidia kuongeza uwezo wa Halmashauri hiyo katika kuwahudumia wananchi. "Wilaya ya Ngorongoro inapokea fedha nyingi, miradi mingi mfano uki...

Rais Mwinyi: Amani Chachu ya Maendeleo Zanzibar |

 02 Septemba 2025 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema mafanikio makubwa ya maendeleo yaliyopatikana katika uongozi wa Awamu ya Nane yamechangiwa na kudumu kwa amani, mshikamano na utulivu nchini. Akizungumza na jopo la wahariri na waandishi wa habari Ikulu Zanzibar, Rais Dkt. Mwinyi alibainisha kuwa mazingira hayo yameiwezesha Serikali kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo kwa ufanisi. 📌 Mambo muhimu aliyoyasisitiza: Ukusanyaji bora wa mapato na matumizi sahihi ya fedha za Serikali. Uwezo wa Serikali kukopa na kuendesha miradi mikubwa, kutokana na nidhamu ya kifedha na utaratibu bora wa kulipa madeni. Uanzishwaji wa akaunti maalum ya kulipia madeni (Debt Management Account) ambapo Serikali huweka dola milioni 15 kila mwezi (sawa na dola milioni 180 kwa mwaka). Kuwekeza katika maendeleo ya wataalamu wa ndani na kuimarisha vyuo vya amali ili kuwajengea vijana stadi za kazi za kuajiriwa na kujiajiri. 🗳️ Kuhusu Uchaguzi Ujao Ra...

Mbio za Kukinadi Chama cha Mapinduzi Mkoani Geita zaanza Kwa Kishindo

📌 Majimbo 7 kati ya 9 yapita bila kupingwa 📌 Kata 92 kati ya 122 zapita bila kupingwa 📌 Maelfu wakusanyika kusikiliza Ilani ya CCM 2025-2030 📌 Dkt. Biteko awasisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi kumpigia kura Dkt. Samia Suluhu Hassan 📌 Asisitiza mshikamano kabla na baada ya uchaguzi Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Geita leo Septemba 2, 2025 kimezindua kwa kishindo kampeni za kuinadi Ilani ya CCM 2025-2030 kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ambapo imeelezwa kuwa mpaka sasa tayari Majimbo 7 kati ya 9 ya Ubunge yamepita bila kupingwa huku kata 92 kati ya 122 zikipita bila kupingwa. Mgeni rasmi katika uzinduzi huo uliofanyika katika Kata ya Uyovu Wilaya ya Bukombe, Mkoani Geita ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa huo, Nicholaus Kasendamila amesema Chama cha Mapinduzi kinaingia kwenye kampeni kikiwa na mtaji mkubwa wa uadilifu, uaminifu, uchapakazi na busara ya mgombea Urais wa kwa tiketi ya CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan. Amesema kupitia kwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ...

Mmiliki wa Kiwanda Cha Kutengeneza Ndege Morogoro Aongeza Mkataba wa Uwakilishi wa Heshima

Balozi wa Tanzania katika Jamhuri ya Czech mwenye makazi yake Berlin, Ujerumani, Mhe. Hassani Iddi Mwamweta wamewekeana saini mkataba na Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania katika Jamhuri ya Czech, Bw. Roman Glorig wa kuhuisha rasmi nafasi yake ya uwakilishi wa heshima. Balozi Mwamweta alisaini mkataba huo Septemba 02, 2025 kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (Mb). Kusainiwa kwa mkataba huo na Bw. Glorig ambaye ni mmiliki wa kiwanda cha kutengeneza ndege cha Airpalane africa limited kilichopo mkoani morogoro, ni kielelezo cha dhamira ya dhati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuimarisha na kupanua wigo wa ushirikiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Czech. Hatua hii inalenga si tu kudumisha urafiki uliopo, bali pia kuchochea ushirikiano mpya katika sekta muhimu zikiwemo afya, elimu, biashara, uwekezaji, na utalii. Kupitia ushirikiano huu, Serikali ina matarajio makubwa ya kuona ongezeko la ubadilishanaji wa ...