Na Mwandishi Wetu SERIKALI imeahidi kuendelea kushirikiana na sekta binafsi katika elimu huku ikiipongeza shule ya St Anne Marie Academy ya jijini Dar es Salaam kwa kufanya vizuri kwenye matokeo ya mitihani ya kitaifa. Pongezi hizo zimetolewa leo jijini Dar es Salaam na Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam Gift Kyando wakati wa mahafali ya darasa la saba yaliyofanyika kwenye viwanja vya shule hiyo Mbezi Kimara kwa Msuguri. Alisema amefurahishwa na mazingira mazuri ya shule baada ya kutembelea maeneo mbalimbali ya shule hiyo na kuridhishwa pia na namna maktaba zilivyoboreshwa na kuwekwa vitabu vya kila aina kuwawezesha wanafunzi kupata maarifa wanayotaka. “Waswahili wanasema tembea uone, mimi leo nimejionea mwenyewe kwa macho yangu namna St Anne Marie Academy ilivyoboresha mazingira ya shule kwa kupanda miti ya kutosha, bustani za mboga mboga na matunda kiasi kwamba mnajitosheleza wenyewe kwa mboga mboga na matunda, naomba wengine nao waige kutoka kwenu,” alisema Alimpongeza ...