Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran limetangaza kuwa, licha ya shinikizo la muda mrefu kutoka kwa maadui wake kutaka kusitishwa kwa mapigano, Tehran ilisimama imara na kukataa hadi sasa ilipoona malengo yake ya kijeshi yanafikiwa. Katika taarifa hiyo, Iran imesema kuwa baada ya takribani siku 40 za vita, imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika operesheni zake na imewaweka maadui katika hali inayodai ni ya udhaifu mkubwa. Hata hivyo, imeonya kuwa mapambano yanaweza kuendelea ikiwa mafanikio hayo hayatatafsiriwa katika ushindi wa kisiasa na usalama wa kudumu katika eneo la Mashariki ya Kati. Kwa kufuata mwongozo wa viongozi wake wa juu, Iran sasa imekubali kuingia katika mazungumzo na Marekani, yatakayofanyika mjini Islamabad, nchini Pakistan kuanzia Ijumaa ijayo. Lengo la mazungumzo hayo Baraza limesema ni kuweka mfumo wa makubaliano ya kudumu ndani ya kipindi kisichozidi siku 15. Iran imesisitiza kuwa imewasilisha mapendekezo yake yenye masharti maalumu 10 kupitia Pakistan, ambayo...
Marato tv - Sauti ya Jamii