Skip to main content

Posts

Showing posts from June 21, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Kikwete Apokea Milioni 52 Kutoka Kepa Kwenda Kukarabati Shule ya Msingi Chalinze

Mbunge wa Jimbo la Chalinze na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete Jana Juni 21, 2025 amepokea hundi yenye thamani ya milioni 52 kutoka Kiwanda cha KEDA kilichopo Chalinze mkoani Pwani kwa ajili ya kwenda kusaidia ukarabati wa Shule ya Msingi ya Chalinze iliyopo Jimboni kwake Chalinze.  Makabidhiano hayo yamefanyika Jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Johari Rotana ambapo hundi iliyotolewa ni sehemu ya mchango wa boksi 1,000 za tails ambapo vifaa hivi vitatumika katika ujenzi na ukarabati wa madarasa sita pamoja na kukamilisha bweni la wavulana wenye mahitaji maalumu. Aidha, Kikwete amepokea vifaa vingine kutoka Kiwanda cha KEDA ambavyo ni kompyuta 20 na meza zake, televisheni yenye ukubwa wa inchi 43, mashine ya kutolea nakala (photocopy), kamera, mipira ya michezo pamoja na jezi za wachezaji. Kikwete ameushukuru uongozi wa Kiwanda hicho na kutoa wito kwa wadau wengine kujitokeza katika kuchangia ukarabati wa shule hiy...

Ajuza, 80, Ajiunga Na Chuo Cha Kushona; Kwa Weledi Wake, Wanamwita ‘under 18’

AJUZA wa Mwenye Umri wa miaka 80 katika mtaa wa mabanda wa Mukuru-Kayaba, South B, Nairobi amewashangaza wengi baada ya kukiuka vikwazo vingi na kujiunga na kinamama wachanga kujifunza ushonaji. Kutana na Grace Wamucii Rua mwenye umri wa miaka 80 aliyezaliwa Limuru mwishoni mwa Vita vya Pili vya Dunia mwaka wa 1945. Kulingana na Grace, wazazi wake walikufa akiwa na umri wa miaka miwili. Anasema kutokana na kuwa yatima, alichukuliwa na nyanyake yake kabla ya wajomba zake kumchukua na kumlea kama mtoto wao baada ya Bibi yake kufariki. Alikuja Nairobi Machi 1997 ambapo anasema hakujaliwa kupata mtoto hadi 1998 alipopanga (adoption) mvulana na msichana ambao alipewa na rafiki yake. Amekuwa akiishi na watoto hao wawili Nairobi na amekuwa nao kama mama yao. Leo, binti yake ameolewa na kubarikiwa mtoto ambaye Grace anasema ni ‘mtoto wake’. Grace asema alikuwa Mkatoliki mwaminifu kabla kujiunga na Kanisa la All Nations PEFA South B. Alisimulia jinsi alivyowasihi viongozi wa All Nations kupata ...

Maua ya Alizeti Yavutia Masoko Ng'ambo

  Na Mwandishi Wetu;Nairobi ALIZETI ambayo kwa miaka mingi imekuwa ikitumika kama malighafi ya utengenezaji mafuta ya kupikia na kuunda chakula cha mifugo, maua yake sasa yameanza kushabikiwa kurembesha mazingira. Yamegeuka kuwa kivutio kipya na kuorodheshwa miongoni mwa maua ya mapambo yanayouzwa ng’ambo. Kenya, ikijivunia kuwa miongni mwa wazalishaji nguli wa maua duniani na kushikilia nafasi ya nne katika uuzaji wa maua hususan ya umaridadi, sasa inajumuisha alizeti kwenye orodha ya maua yenye ushindani mkuu sokoni. Aghalabu, Kenya husafirisha asilimia 99 ya maua yake kwa zaidi ya nchi 80 ulimwenguni haswa aina ya waridi ‘rose’, carnation na alstroemeria. Alizeti sasa imejiunga rasmi na utandawazi huu wa maua ya kuvutia. Alizeti sasa inakumbatiwa kama maua ya urembesho. Picha|Sammy Waweru Ikiwa nyuma ya Colombia na Ecuador, katika nafasi ya tatu kimataifa kwa uzalishaji wa maua yaliyokatwa, Kenya inalenga kubadilisha sura ya maua yake kwa kuingiza maua ya kiangazi (summer flower...

Waziri wa Ulinzi na Jkt awatunuku Makamanda wa Nchi 14 za Afrika

   Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mheshimiwa Dkt Stagomena Tax ametunuku Shahada ya uzamili na Stashahada kwa Maafisa 71 kutoka nchi 14 za Afrika katika Mahafari ya 39 ya Chuo cha Ukamanda na Unadhimu Tanzania leo tarehe 21 Juni 2025. Akizungumza wakati wa Mahafari hayo,Dkt Tax amewaasa wahitimu wa kozi ya Ukamanda na Unadhimu kutumia ujuzi walioupata kutoka chuoni hapo kushiriki katika uandaaji na upangaji wa mikakati ya kiusalama wa mataifa yao ili kulifanya bara la Afrika mahala salama.  Kwa Upande wake Mkuu wa Chuo hicho Meja Jenerali Stephen Justice Mnkande amesema kuwa Maafisa hao wamehitimu na kutunukiwa shahada ya Uzamili na Stashahada ya Juu Defence and Security Studies ambapo wamefaulu kwa viwango vya juu.  Naye Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Salum Haji Othman amesema kuwa Maafisa hao wanategemewa na Majeshi ya mataifa yao katika kusaidia kupanga mikakati mbalimbali ya Ulinzi na Usalama wa mataifa yao na kuwataka kufanya kazi kwa bidii na...

Waziri Wa Ulinzi na Jkt Awatunuku Makamanda wa Nchi 14 za Afrika

 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mheshimiwa Dkt Stagomena Tax ametunuku Shahada ya uzamili na Stashahada kwa Maafisa 71 kutoka nchi 14 za Afrika katika Mahafari ya 39 ya Chuo cha Ukamanda na Unadhimu Tanzania leo tarehe 21 Juni 2025. Akizungumza wakati wa Mahafari hayo,Dkt Tax amewaasa wahitimu wa kozi ya Ukamanda na Unadhimu kutumia ujuzi walioupata kutoka chuoni hapo kushiriki katika uandaaji na upangaji wa mikakati ya kiusalama wa mataifa yao ili kulifanya bara la Afrika mahala salama . Kwa Upande wake Mkuu wa Chuo hicho Meja Jenerali Stephen Justice Mnkande amesema kuwa Maafisa hao wamehitimu na kutunukiwa shahada ya Uzamili na Stashahada ya Juu Defence and Security Studies ambapo wamefaulu kwa viwango vya juu.  Naye Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Salum Haji Othman amesema kuwa Maafisa hao wanategemewa na Majeshi ya mataifa yao katika kusaidia kupanga mikakati mbalimbali ya Ulinzi na Usalama wa mataifa yao na kuwataka kufanya kazi kwa bidii na maarifa ka...

Mtendaji Mkuu Tanroads Akagua Ujenzi Wa Uwanja wa Ndege Sumbawanga, Ujenzi Wafikia Asilimia 70

Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Mohamed Besta, leo Jumamosi Juni 21, 2025 ametembelea uwanja wa ndege wa Sumbawanga kukagua maendeleo ya ujenzi wake ambao unaendelea kwa kasi. Akizungumza baada ya ziara hiyo, Mhandisi Besta amesema ujenzi wa uwanja huo umefikia asilimia 70, ambapo sehemu ya kuruka na kutua ndege (runway) tayari imekamilika, na kazi imebakia kwenye mita 15 tu kati ya jumla ya kilometa 1.7. Ameongeza kwa kusema kuwa, baada ya kukamilisha sehemu hiyo, mkandarasi ataanza kazi ya kuweka alama (markings) kwenye runway, barabara za kuingilia ndege (taxiways), maegesho ya ndege (apron), pamoja na kuweka taa maalum (flight lights) kwa ajili ya usiku. “Nimeridhishwa na maendeleo ya kazi hii na napenda kumpongeza msimamizi kutoka kampuni ya SMEC International kwa kusimamia kwa umakini na kuhakikisha kazi zinaendelea vizuri. Natarajia uwanja huu utakuwa tayari kutumika kuanzia mwezi Julai hadi Agosti,” alisema Besta. Aidha, amemuelekeza mkandarasi...

Kaeni Kimya Kama Hamjui Nchi Ilikotoka - Wasira

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira amesema tangu kupata uhuru Tanzania imepata maendeleo makubwa na kwamba wanaosema hakuna kilichofanyika ni vema wakakaa kimya, wasiwe na tabia ya kasuku kukariri wasiyoyajua. Wasira ameyasema hayo leo Juni 17, 2025 alipokuwa akizingumza katika mkutano wa hadhara Katoro, mkoani Geita akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama na kuzungumza na wananchi. Akieleza kuhusu maendeleo yaliyofanyika nchini tangu kupatikana kwa uhuru alisema ni makubwa na wenye umri mkubwa wanajua vizuri nchi ilivyokuwa na wamekuwa wakishuhudia hatua mbalimbali zinazofanywa na serikali inayoundwa na CCM. “Labda ninyi vijana hamwelewi lakini niwaambie wakoloni wa Kijerumani na wakoloni wa Kiingereza wamekaa Tanganyika miaka 75, Wajerumani wamekaa miaka 35, wamejenga reli kwa viboko bila malipo.  Waingereza  wamekaa miaka 40 walitumwa na Umoja wa Mataifa (UN) watuendeleze tujitawalie, lakini miaka 40 ya Waingereza wametuacha na wahandisi...

Rais Dkt. Samia Anatambua Mchango Wa Bunge Kwenye Kuhamaisha Michezo-Majaliwa

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Juni 21, 2025 amemuwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika tamasha la Grand Bunge Bonanza lililofanyika katika viwanja vya shule ya Sekondari ya John Merlin jijini Dodoma. Akizungumza katika bonanza hilo, Waziri Mkuu amesema kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia anatambua na kuthamini mchango wa Bunge la Tanzania katika kuimarisha umoja, Afya na mshikamano kupitia michezo mbalimbali. Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa tamasha hilo ni sehemu ya makakati wa bunge wa kuunga mkono jitihada za Rais Dkt. Samia za kuhamasisha watanzania kushiriki mazoezi ya viungo na lina mchango mkubwa katika kuhamasisha uwepo wa utamaduni wa kufanya mazoezi ya mwili  “Mazoezi haya mliyoyafanya kupitia Grand Bunge Bonanza yana umuhimu mkubwa si tu kwa afya, bali pia yanajenga urafiki na uhusiano mwema miongoni mwetu lakini pia yanaimarisha afya ya akili na hivyo kuongeza ufanisi katika utendaji wa majukumu yetu ya kila siku kwenye maeneo yetu” Kwa upande wake, Naibu Spika ...