Skip to main content

Posts

Showing posts from September 26, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

BRELA YAENDELEA KUTOA ELIMU GEITA

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) umewahamasisha wafanyabiashara na wajasiriamali wanaoshiriki Maonesho ya Tisa ya Madini mkoani Geita kutumia fursa hiyo kupata elimu na huduma za usajili wa biashara, majina ya biashara, kampuni na nembo. Akizungumza na waandishi wa Habari katika banda la BRELA kwenye maonesho ya 9 ya  Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika kwenye viwanja Vya Dkt. Samia Suluhu Hassan mkoani Geita Afisa wa BRELA, Salum Makuka, amesema wakala huo umeweka huduma zake katika maonesho hayo ili kuwafikia wananchi kwa urahisi na kuwawezesha kupata elimu pamoja na huduma za usajili papo hapo. Makuka amesema huduma zinazotolewa na BRELA ni pamoja na usajili wa kampuni, majina ya biashara, nembo za biashara (trademarks), viwanda vidogo, leseni za biashara za Daraja A pamoja na usajili na ulinzi wa bunifu kupitia hati miliki (patent). Ameongeza  kuwa wananchi wanaofika katika banda hilo kwa ajili ya kupata huduma za usajili hawatozwi gharama za urahi...
  UKOSEFU WA MTAJI NA TEKNOLOJIA KUWAFANYA WACHIMBAJI WAONE LESENI KAMA MZIGO  Na Richard Mrusha  Umuhimu wa ushirikiano kati ya wachimbaji wadogo na watoaji wa msaada wa kiufundi (TSA) umeibuka wazi katika Siku ya Wachimbaji Wadogo iliyoadhimishwa Septemba 26, 2026 ndani ya Maonesho ya Tisa ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika Viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan mkoani Geita. Kupitia simulizi iliyosimuliwa na Emmanuel Francis Jirab kutoka Kampuni ya Yi Xing Kuangye Mining Co. Ltd, ilibainika jinsi ukosefu wa mtaji na teknolojia unavyoweza kumfanya mchimbaji aone leseni yake kama mzigo. Jirab alieleza kuwa mchimbaji mmoja alifikia mahali pa kuandika barua kwenda Wizara ya Madini kuomba leseni zake zifutwe baada ya maduara yake kujaa maji na kushindwa kuendelea na shughuli kwa muda mrefu. Wawekezaji walipokuja, walikuja wenyewe nyumbani, mimi sikuwatafuta. Wakatembelea na kukubali kwamba tutafanya nao uchimbaji," alisema Jirab akielezea namna wawekezaji...

MAGEREZA YAITIKISA NGOME YA JWTZ, YAIBUKA NA USHINDI WA SETI 3–2

 Na Ssgt Mawazo Mtondo - MWANZA Timu ya mpira wa wavu wanaume ya Jeshi la Magereza 25 Septemba, 2026 imepata ushindi wa kusisimua wa seti 3–2 dhidi ya Timu ya Ngome ya JWTZ, katika mchezo mkali na wa kuvutia wa Mashindano ya Bammata 2026 yanayoendelea Jijini Mwanza. Mchezo huo uliokuwa na mashambulizi makali, ulinzi imara na mabadiliko ya kasi ya mchezo, uliifanya kila timu kupigania kila pointi. Magereza ilionyesha uthubutu na umakini hadi hatua za mwisho na hatimaye kuibuka na ushindi huo wa muhimu, uliowapa wachezaji morali na hamasa zaidi kuelekea michezo inayofuata. Kocha Mkuu wa timu hiyo, Ssgt Mussa Shabani, amesema ushindi huo umetokana na umoja, nidhamu, kujituma na kupambana kwa wachezaji, huku akisisitiza kuwa timu itaendelea kuongeza nguvu na kuboresha maeneo yaliyobainika katika mchezo huo. Naye Kapteni wa timu hiyo, Wdr Martin Anthony, amesema ushindi huo umeongeza morali ndani ya kikosi na kwamba wachezaji wataendelea kupambana kwa moyo, nguvu na mshikamano, wakileng...