Skip to main content

Posts

Showing posts from November 29, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt Mwigulu akagua uharibifu wa kituoo cha Polisi Kikatiti

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Novemba 30, 2025, amekagua Kituo cha Polisi Kikatiti ambacho kiliharibiwa kutokana na vurugu zilizotokea Oktoba 29, 2025, mkoani Arusha. Akizungumza na wakazi wa eneo hilo, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amewataka wananchi kuwa makini dhidi ya watu wasiolitakia mema Taifa kwa kuchochea vurugu na kuharibu miundombinu ya umma na ya binafsi. Mheshimiwa Dkt. Mwigulu yupo mkoani Arusha kwa ziara ya kukagua uharibifu uliojitokeza kufuatia vurugu za Oktoba 29, 2025. Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Amosi Makalla.

Dkt.Mwigulu awasili mkoani Arusha

WAZIRI Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba amewasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) ambapo atakagua ulioandikwa na vurugu zilizotokea Oktoba 29, 2025 mkoani Arusha. Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amepokelewa na viongozi wa Serikali pamoja na Chama

Mhe.Ndejembi awahakikishia wakazi wa Kigamboni umeme wa uhakika

📌Afanya Ziara katika Kituo cha Dege  📌Aelekeza hatua za haraka kuchukuliwa kunusuru hali ya umeme Kigamboni 📌Umeme wa Megawati 22 kupatikana kwa hatua za haraka  📌Upanuzi wa Kituo cha Dege wafikia asilimia 60  Waziri wa Nishati Mhe. Deogratius Ndejembi amefanya ziara ya kikazi ndani ya Mkoa wa kitanesco wa Kigamboni na kuagiza kuchukuliwa hatua za haraka za kuhakikisha hali ya umeme katika Mkoa wa Kigamboni inaboreshwa na kuwapa wakazi wa eneo hilo huduma ya uhakika alipotembelea Kituo cha Kupokea, Kupoza na Kusambaza umeme cha Dege tarehe 29 Novemba, 2025. “Leo tumekuja kuona ni namna gani Shirika letu la TANESCO linaweza kutatua changamoto hii kwa haraka zaidi na wameweka mipango mizuri ya muda mrefu katika kuhakikisha wanawezesha kupatikana kwa umeme wa uhakika kwa kujenga na kukiongezea nguvu Kituo cha Dege kwa kuweka transfoma ya MVA 120”, ameeleza Mhe. Ndejembi.  Ili kukabiliana na changamoto ya huduma ya umeme iliyopo kwa haraka, Shirika limekuja na suluhi...

Waziri Mavunde awaasq wamiliki wa leseni za uchimbaji madini kuzingatia sheria na kanuni za uchimbaji

●  Maboresho ya Kanuni za Haki Madini za Mwaka 2025 yaongeza ufanisi kwa wenye maduara na kupunguza migogoro, ●  Wamiliki wa Leseni za Utafiti wasioendeleza Leseni kufutiwa Leseni ●  Vikundi vya vijana na wanawake  vyaendelea kunufaika na utekelezaji wa Programu ya MBT, ●  Waziri Mavunde asisitiza amani na utii wa Sheria kwa wachimbaji wadogo, 📍Nyang'wale, Geita Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde akiwa ziarani Wilayani Nyang'wale amewaasa na kuwataka wamiliki wa leseni za uchimbaji wa madini kuzingatia Sheria ya Madini Sura ya 123 na Kanuni zake katika utekelezaji wa majukumu yao. Akizungumza katika ziara hiyo iliyofanyika kwenye eneo la mgodi wa Kasubuya wilayani Nyang’hwale, Waziri Mavunde amesema wachimbaji wadogo kwa sasa wanachangia zaidi ya asilimia 40 ya mapato yatokanayo na sekta ya madini, akibainisha kuwa mchango wao unaendelea kuongezeka kutokana na maboresho makubwa ya Sheria, Kisera na Kiutendaji yanayofanywa na Serikali. Waziri Mavunde a...