Skip to main content

Posts

Showing posts from June 2, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Majaliwa Mgeni Rasmi Katika Jukwaa la Vijana na Mazingira

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Juni 03, 2025 ni mgeni rasmi katika jukwaa la vijana na mazingira linalofanyika katika ukumbi wa maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Jukwaa hilo la vijana na mazingira lina malengo ya kuwaunganisha vijana kutoka sehemu mbalimbali nchini, kuwajengea uelewa kuhusu masuala ya mazingira pamoja na kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika kubuni na kutekeleza mikakati ya kutatua changamoto za mazingira nchini. Tuliko hilo ambalo ni sehemu ya maadhimisho kuelekea siku ya Mazingira Duniani, limeandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) kwa kushirikiana na Taasisi ya Africa Carbon Agency.

Mkuu wa Kikosi Ffu Mara Ahamasisha Wadau Kuandaa Matukio ya Michezo

Na Shomari Binda-Musoma  MKUU wa Kikosi cha Kuzuia na Kutuliza Ghasia ( FFU) mkoani Mara ASP Edwin Mwaisanila amewaita wadau wa michezo kujitokeza kuandaa mashindano mbalimbali. Wito huo ameutoa leo juni 2,2025 kwenye uwanja wa Kamnyonge shule ya msingi kwenye mchezo wa kirafiki kati ya FFU Mara na Buhare fc. Mchezo huo ulikuwa maalum kuikabidhi cheti cha ushindi timu ya FFU Mara baada ya kuibuka washindi kwenye bonanza la miaka 61 ya Muungano. Akizungumza uwanjani hapo Mwaisanila amesema  Musoma na mkoa wa Mara kuna vipaji vikubwa na vinapaswa kuendelezwa. Amesema kuendelezwa kwa vipaji hivyo ni kuandaliwa kwa mashindano mbalimbali yakiwemo mabonanza. Mkuu huyo wa FFU Mara amesema viongozi wa michezo wanapaswa kuwa karibu na wadau na kuwashawishi kuandaa michezo hiyo. " Musoma na mkoa wa Mara kuna vipaji vikuÉ“wa vya michezo ambavyo vinapaswa kuendelezwa ili baadae wanufaike kiuchumi kupitia michezo. " Kuendelezwa ni pamoja na kuanzishwa kwa michezo na mabonanza mbalimbali ka...

Kampuni ya Crje Yawakutanisha Watanzania na Mataifa Mbali Mbali Kusheherekea Tamasha wa Wachina la Dragon Boat

Na Mwandishi Wetu Kampuni ya CRJE (East Africa) Limited imeungana na mataifa mbali mbali jijini Dar es Salaam kusheherekea Tamasha la Utamaduni la watu wa China la Dragon Boat ambalo ni mahususi kwa kudumisha utamaduni. Tamasha la Dragon Boat, pia linajulikana kama Tamasha la Duanwu, kwa kawaida huangukia siku ya tano ya mwezi wa tano katika kalenda ya mwandamo ya Kichina. Ambapo Iliadhimishwa mwaka huu siku ya jumamosi Mei 31 jijini Dar es Salaam. Wakati wa tamasha hilo lililofanyika eneo la Masaki jijini Dar es Salaam, watu kutoka mataifa mbali mbali walifurahia tamaduni mbali mbali za watu kutoka China kama vile kula Zongzi (wali unaonata) ili kumkumbuka Qu Yuan, mshairi na mwanasiasa wa Kichina aliyeheshimika wa kipindi cha miaka ya 475 B.C.-221 B.K. Akizungumza katika tamasha la kwanza, lililoandaliwa na CRJE (East Africa) Ltd jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa CRJE Jiang Yuntao alisema kuwa tukio hilo pia lililenga kukuza mabadilishano ya kitamaduni na maelewano kati ya China na...

Rais Mwinyi:Zanzibar Inatambua Mchango Mkubwa wa China

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatambua mchango mkubwa unaotolewa na Serikali ya China katika nyanja mbalimbali, ikiwemo timu ya madaktari kutoka China wanaokuja kutoa huduma za kibingwa katika hospitali za umma, pamoja na fursa za ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa Zanzibar. Dkt. Mwinyi ameyasema hayo alipokutana na Balozi Mdogo mpya wa China, Mhe. Li Quanghua, aliyefika Ikulu Zanzibar leo 02 Juni 2025, kwa ajili ya kujitambulisha rasmi pamoja na ujumbe wake. Katika mazungumzo hayo, Rais Dkt. Mwinyi ametaja maeneo mahususi ya ushirikiano ambayo Serikali ya Zanzibar imeyapa kipaumbele, yakiwemo: kuhamasisha uwekezaji kutoka China, kukuza biashara baina ya pande mbili, na kuimarisha programu za kuwawezesha vijana kupitia mafunzo ya ufundi stadi ili kupunguza changamoto ya ajira kwa vijana wengi wanaokosa ujuzi unaohitajika katika soko la ajira. Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amesisitiza umuhi...

Ccm Kufadhili Kitabu Cha Mzee Songambele Kuenzi Historia ya Nchi, Chama na Serikali

_Balozi Nchimbi atoa neno, akimwakilisha Dkt. Samia msibani_ Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amesema kitabu alichoandika Alhaj Mzee Mohamed Mustafa Songambele kitakuwa mojawapo ya rejea adhimu za historia ya Tanzania.  Balozi Nchimbi amesema kuwa kitabu hicho kiitwacho “_*Safari ya Karne*_”, kina utajiri wa maelezo kuhusu mapambano ya kutafuta uhuru wa Tanganyika, kupatikana kwa nchi na taifa la Tanzania na kuundwa kwa CCM.  Dkt. Nchimbi amesema hayo alipokuwa akitoa salaam za pole na rambirambi  kwenye msiba wa Hayati Alhaji Mzee Songambele, akimwakilisha Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, mjini Songea, mkoani Ruvuma, leo Jumatatu tarehe 2 Juni 2025. “Kutokana na heshima na mchango mkubwa wa Mzee Songambele kwa nchi yetu, taifa letu na chama chetu, Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuguswa sana na msiba huu, ameniagiza rasmi kumwakilisha na ameagiza Chama na Serikali kuc...

Balozi Nchimbi Awasili Songea Mazishi ya Mzee Songambele

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Songea, mkoani Ruvuma na kupokelewa na viongozi wa Chama na Serikali mkoani humo, wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed na Katibu wa CCM Mkoa wa Ruvuma, Mohamed Ali Khalfan, leo Jumatatu tarehe 2 Juni 2025.  Balozi Nchimbi amewasili mjini Songea, kwa ajili ya kushiriki mazishi ya mwanasiasa mkongwe na mmoja wa wapigania uhuru wa Tanganyika, na waasisi wa Chama cha TANU na CCM, Alhaj Mzee Mustafa Mohamed Songambele, aliyefariki usiku wa kuamkia Juni 1, 2025 jijini Dar es Salaam na kutarajiwa kuzikwa leo mjini Songea.