Skip to main content

Posts

Showing posts from October 23, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mkuu akutana na balozi wa Belarus nchini

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Oktoba 24. 2024 amekutana na Balozi wa Belarus nchini Tanzania Pavel Vziatkin, katika Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam. Katika mazungumzo hayo, Mheshimiwa Majaliwa amemweleza Balozi Pavel kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Belarus katika Sekta za Madini, Afya, Utalii, Kilimo na Biashara kwa faida ya nchi zote mbili

Miaka mitatu ya Rais Dkt Samia madarakani ongezeko la .akusanyo ya madini yapaa

• Tume ya Madini yaainisha mikakati yake kufikia 10% ya Pato la Taifa • Yasimamia ajira 18,853 za Watanzania katika kampuni za madini • Leseni za madini 34,000 zatolewa  • Katibu Mtendaji aipongeza Wizara ya Madini chini ya Waziri Mavunde kwenye usimamizi wa Sekta ya Madini. Mwandishi Maalum, Tume ya Madini. MIAKA mitatu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan madarakani, Tume ya Madini imeainisha mafanikio yake ikiwemo ongezeko la ukusanyaji wa maduhuli, kuongezeka kwa usimamizi kwenye biashara ya madini na ukaguzi wa migodi na mazingira sambamba na ushirikishwaji wa watanzania katika Sekta ya Madini. Akizungumza na Wahariri wa Vyombo vya Habari, leo Oktoba 24, 2024 katika ukumbi wa Chuo cha Utalii jijini Dar es Salaam, Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Ramadhani Lwamo amesema kupitia usimamizi unaofanywa na Tume ya Madini, kiwango cha makusanyo ya maduhuli ya Serikali kimepanda kutoka Shilingi bilioni 624.61 zilizokusanywa Mwaka ...

Tanzania na Belarus kuimarisha ushirikiano kwenye sekta ya madini

▪️Balozi wa Belarus aeleza utayari wao kubadilishana utaalam kwenye teknolojia* ▪️Waziri Mavunde anadi uwepo wa madini mbalimbali kuvutia wawekezaji zaidi.* ▪️Apigia debe mitambo na teknolojia kwa wachimbaji wadogo Waziri wa Madini, *Mheshimiwa Anthony Mavunde* leo tarehe 24 Oktoba, 2024 amekutaja na kufanya mazungumzo na Balozi wa Belarus nchini Tanzania, *Mheshimiwa Pavel Vziatkin*. Katika mazungumzo hayo, Balozi Pavel amebainisha kuwa lengo la ziara yake ni kuendelea kuimarisha diplomasia ya uchumi baina ya Belarus na Tanzania, kuzifahamu zaidi fursa zinazopatikana katika sekta ya madini nchini Tanzania na kuonesha namna Belarus ilivyopiga hatua katika teknolojia na utengenezaji wa mitambo imara inayoweza kutumika katika sekta ya madini. Akimkaribisha *Balozi Pavel*, *Waziri Mavunde* alieleza kwamba Nchi ya Tanzania imebarikiwa uwepo wa madini ya aina mbalimbali yakiwemo ya metali, Vito na madini mkakati na kusisitiza kuwa zipo fursa lukuki ambazo wawezekaji kutoka Belarus wanakarib...

Rais Samia mwanamkr pekee kumi bora kiuchumi afrika

 Uchumi wa Tanzania kumi bora Africa, Rais Samia kiongozi mwanamke pekee kati nchi zinazofanya vizuri! 🌍 Licha ya changamoto zinazokumba uchumi wa dunia, Tanzania imeendelea kuwa imara na kukua, ikijivunia kuingia kwenye orodha ya nchi 10 bora za Afrika kwa Pato la Taifa (GDP) kwa mwaka 2024, kwa mujibu wa IMF.  Ikiwa na GDP ya dola bilioni 79.87, maendeleo ya uchumi wa Tanzania yanaonyesha athari chanya za sera bora, uongozi madhubuti, na kujitolea kwa maendeleo chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan. 🇹🇿 Ingawa nchi nyingine zinaweza kuwa na takwimu kubwa zaidi, kupanda kwa Tanzania kunadhihirisha ukuaji endelevu na jumuishi, hususan katika sekta muhimu kama kilimo, utalii, na viwanda.  Mustakabali wa Tanzania unaangaza, tunapoendelea kujenga misingi hii, tukihakikisha ustawi kwa wananchi wote. 

Tume ya Madini yakutana na wahariri wa vyombo vya habari

Picha mbalimbali za matukio wakati wa mkutano wa wahariri wa vyombo vya habari nchini na watendaji wa Tume ya Madini unaoendelea muda huu jijini Dar es Salaam Kupitia mkutano huo, Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Eng. Ramadhani Lwamo anaelezea mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita kwenye usimamizi wa Sekta ya Madini sambamba na kutoa ufafanuzi wa masuala ya Sekta ya Madini.