Skip to main content

Posts

Showing posts from August 18, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

MARY SURATI ASHIRIKI USIKU WA TUZO KWA WADAU WA ELIMU SEKONDARI YA MANGA-TARIME

 Mbunge wa Jimbo la Serengeti, Mhe. Mary Daniel Surati, amewahimiza wanafunzi kuendelea kusoma kwa bidii, kuweka malengo makubwa na kutumia fursa za elimu kujijengea msingi imara wa maisha na maendeleo ya jamii. Mhe. Surati ameyasema hayo aliposhiriki Usiku wa Tuzo kwa Wadau wa Elimu uliofanyika katika Shule ya Sekondari Manga wilayani Tarime, ambapo hafla hiyo iliambatana na utoaji wa tuzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo. Hafla hiyo imekuwa sehemu ya kutambua na kuenzi juhudi za wanafunzi walioonesha umahiri katika masomo, huku ikiwahamasisha wengine kuongeza bidii ili kufikia mafanikio makubwa zaidi kitaaluma. Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Surati amesema amefurahishwa na jitihada zinazofanywa na wanafunzi, walimu, wazazi pamoja na wadau mbalimbali wa elimu katika kuhakikisha wanafunzi wanapata mazingira yanayowawezesha kufanya vizuri na kutimiza ndoto zao. Amesema mafanikio ya mwanafunzi hayajengwi na juhudi za mtu mmoja pekee, bali yanahitaji ushirikiano wa k...

Mkakati wa Taifa wa Nishati Safi ya Kupikia Waanza Kutekelezwa Mkinga

  📌*Mitungi ya gesi ya kilo sita 3,255 kuuzwa kwa bei ya ruzuku ya Shilingi 17,500* 📍*Mkinga, Tanga* Serikali imeanza kutekeleza kwa vitendo Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia katika Wilaya ya Mkinga, Mkoa wa Tanga, kupitia mradi wa usambazaji na uuzaji wa mitungi ya gesi ya kilo sita kwa bei ya ruzuku. Kupitia mradi huo, jumla ya mitungi 3,255 ya gesi ya kilo sita itasambazwa na kuuzwa kwa wananchi wa Mkinga kwa bei ya ruzuku ya Shilingi 17,500 kwa mtungi. Mwananchi anayehitaji kunufaika na mpango huo anatakiwa kuwa na Kitambulisho cha Taifa (NIDA). Mtungi huo utauzwa ukiwa tayari kwa matumizi, ukiwa na gesi pamoja na vifaa muhimu. Mradi huo ni sehemu ya utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia, unaolenga kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2034, asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia. Utekelezaji wa mradi huo unalenga kuongeza upatikanaji na matumizi ya nishati safi, salama na rafiki kwa afya na mazingira, huku ...

PAC YAKERWA NA MANUNUZI YA SH. BILIONI 29.77 MZUMBE

 Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC)  haijaridhishwa na maelezo yaliyotolewa na Chuo Kikuu cha Mzumbe kuhusu hoja zilizojitokeza katika Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa Fedha 2024/2025. Akizungumza na waandishi wa Habari leo Agosti 18,2026  Bungeni Jijini Dodoma, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mheshimiwa Devotha Minja amesema Kamat Kwa mujibu wa Taarifa ya CAG, Chuo hicho kilifanya manunuzi ya shilingi bilioni 29.77 ambazo zilitolewa na wazabuni wasiokidhi vigezo na shilingi bilioni 1.54 zilizotolewa kwa watu wasiokidhi viwango. Aidha, alisema Kamati haijaridhishwa na ujenzi wa barabara chini ya kiwango yenye thamani ya shilingi milioni 523 pamoja na madai ya ziada ya shilingi milioni 718 ambayo hayastahili na hayakuzingatia masharti ya mkataba. Mheshimiwa Devotha amesema Kamati inatafakari hatua zaidi za kuchukua ili kulishauri Bunge ipasavyo. Kamati ya PAC ilikuwa inajadili Taarifa ya Hesabu zilizokaguliwa za Chu...

DKT. YONAZI AVIASA VIKUNDI VYA WAVIU KUTUMIA MITANDAO YA KIJAMII KUWAFIKIA WATEJA

 Na. Mwandishi Wetu - Mwanza Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Dkt. Jim Yonazi ashauri kikundi cha Paza Sauti cha Watu Wanaoishi na Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (WAVIU) kutumia mitandao ya kijamii kutangaza na kuuza bidhaa zao ili kuweza kufikia wateja wengi zaidi huku akiwapongeza kwa juhudi na umoja wao katika shughuli zao za uzalishaji. Ametoa ushauri huo alipotembelea kikundi cha Paza Sauti cha wajasiliamali wanaoishi na VVU katika ziara yake ya ufatiliaji utekelezaji wa afua za VVU na UKIMWI katika Wilaya ya Nyamagana, Jijini Mwanza.   “Nikiingia kwenye simu yangu sioni kikundi cha Paza Sauti msibanwe na soko la machoni nendeni duniani kupitia mitandao ya kijamii, anzisheni akaunti ya Instagram muweze kuwafikia hata watu walipo nchi za nje" alisema Dkt. Yonazi Vilevile, Dkt. Yonazi alitembelea Kikundi cha Peace and Love kinachojishughulisha na kilimo cha nyanya na matikiti, kinachosimamiwa na Halm...

RAIS DKT. MWINYI: UWANJA WA AFCON FUMBA KUWA CHACHU YA FURSA ZA KIUCHUMI ZANZIBAR

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Uwanja wa AFCON unaojengwa Fumba utakuwa uwanja wa kisasa wenye hadhi ya kimataifa na chachu ya kufungua fursa mbalimbali kwa wananchi. Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, 18 Agosti 2026, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa Uwanja wa AFCON pamoja na Bandari ya Fumba, Mkoa wa Mjini Magharibi. Amesema kukamilika kwa uwanja huo kutaiweka Zanzibar katika nafasi nzuri ya kunufaika na fursa za biashara, huduma na shughuli nyingine za kiuchumi zitakazotokana na ongezeko la wageni, hususan wakati wa Michuano ya AFCON 2027. Rais Dkt. Mwinyi amesema Serikali itaendelea kuhakikisha miundombinu inayozunguka uwanja huo inajengwa kwa ubora na viwango vinavyokubalika kimataifa, ili kuongeza thamani ya eneo hilo na kuleta tija kwa Zanzibar kwa muda mrefu. Kwa sasa, ujenzi wa Uwanja wa AFCON umefikia takribani asilimia 80, huku miundombinu mbalimbali ikiendelea kujengwa, ikiwemo barabara ya kisasa itakayoboresha...

SERIKALI: ELIMU YA UJUZI YAANZA KUZAA MATUNDA

  Serikali imesema maendeleo yanayoonekana kwasasa katika mageuzi ya elimu ni ishara kwamba azma ya kuimarisha elimu ya ujuzi mashuleni imeanza kuzaa matunda, huku wanafunzi wakionesha uwezo mkubwa wa kufanya kazi za vitendo kwa kujiamini. Kauli hiyo imetolewa leo Agosti 18, 2026 jijini Tanga na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, baada ya kukagua maandalizi ya Mashindano ya Ujuzi 2026 na kutembelea banda la shule za sekondari za mkondo wa amali katika ufunguzi wa Maonesho ya Kitaifa ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara. Prof. Mkenda amesema wazo la kupeleka ujuzi mashuleni lilianza kusisitizwa na Rais mara tu baada ya kuapishwa, na limeendelea kuwa ajenda muhimu ya mageuzi ya elimu nchini. "Taswira ya wanafunzi, wakiwemo mabinti wanaowasilisha na kutekeleza kazi za kiufundi kwa umahiri, inaonesha kuwa vijana wanaanza kujenga uwezo wa kujitegemea kupitia elimu inayowaandaa kwa soko la ajira,"ame...

RAIS SAMIA AONGOZA UJUMBE WA VIONGOZI WA TANZANIA KATIKA MAZUNGUMZO NA RAIS TSHISEKEDI

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiongoza Ujumbe wa Tanzania kwenye mazungumzo Rasmi na Ujumbe wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ulioongozwa na Rais wa Nchi hiyo, Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo katika Ikulu Ndogo ya Zanzibar, tarehe 18 Agosti, 2026.