Skip to main content

Posts

Showing posts from July 11, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

JAB YAZINDUA RASMI MWONGOZO WA KISHERIA WA UTOAJI WA ITHIBATI YA MAISHA KWA WAANDISHI WA HABARI WAKONGWE

 Na Mwandishi Wetu Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imezindua rasmi Mwongozo wa Kisheria wa Utoaji wa Ithibati ya Maisha kwa Waandishi wa Habari Wakongwe, hatua inayolenga kutambua na kuthamini mchango wa waandishi wa habari waliolitumikia Taifa kwa muda mrefu na kwa utumishi uliotukuka katika maendeleo ya sekta ya habari nchini. Uzinduzi huo umefanyika leo, Julai 11, 2026, wakati wa maadhimisho ya JAB Day yaliyofanyika katika Banda la Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwenye Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba). Kupitia hotuba yake iliyosomwa na Dkt. Egbert Mkoko, Mwenyekiti wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari, Bw. Tido Mhando, alisema mwongozo huo umeandaliwa kwa kuzingatia mamlaka iliyopewa Bodi chini ya Sheria ya Huduma za Habari, Sura ya 229 pamoja na Kanuni zake, ili kuweka utaratibu wa utoaji wa Ithibati ya Maisha kwa waandishi wa habari wakongwe waliotoa mchango wa kipekee katika maendeleo ya taaluma hiyo. Alise...

USULUHISHI WA WIZARA YA SHERIA WAMALIZA MGOGORO WA BIASHARA

 Mkurugenzi wa Kampuni ya Colmat Bw. Tanziru Mahamudu Mkakere amesema ameridhishwa na huduma ya usuluhishi iliyotolewa na Ofisi za Wizara ya Katiba na Sheria baada ya kufanikiwa kutatua mgogoro wa kibiashara uliokuwa baina yake na kampuni ya Sewa. Akizungumza leo Julai 11,2026 katika banda la Wizara ya Katiba na Sheria lililopo kwenye maonesho ya 50 ya kimataifa ya wafanyabiashara maarufu kama Sabasaba Bw. Mkakere amesema mgogoro huo ulitokana na malipo ya kazi ya upakaji rangi wa takribani magari 200, ambapo walikubaliana kulipwa shilingi 270,000 kwa kila gari. Kiasi cha mkataba kilikuwa takribani shilingi milioni 54, lakini alilipwa shilingi milioni 48 pekee na kubaki na deni la takribani shilingi milioni 6. Amesema kutokana na kuchelewa kwa malipo, mgogoro uliwasukuma kufika katika Ofisi za Wizara ya Katiba na Sheria kwa ajili ya usuluhishi. Amesema kupitia huduma hiyo waliweza kusikilizwa, kuelewana na hatimaye kufikia makubaliano ya jinsi deni lililobaki litakavyolipwa. Kwa mu...

DIAMOND PLATNUMZ AZURU BANDA LA WIZARA YA HABARI SABASABA

 Mwanamzuki Nyota wa Tanzania, Nasib Abdul maarufu Diamond Platnumz, amepata nafasi ya kutembelea Banda la Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na michezo kwenye Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) kuona wizara inavyotoa huduma na elimu kwa wananchi. Mwanamuziki Diamond ametembelea banda hilo leo Julai 11, 2026 kufuatia mwaliko wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB).

MWEMBENI SEKONDARI YAPATA MSUKUMO MPYA KUPITIA AGNES MARWA

 SHULE ya Sekondari Mwembeni mkoani Mara imepata msukumo mpya wa kuinua kiwango cha taaluma baada ya Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Mhe. Agnes Marwa, kukabidhi projector ya kufundishia pamoja na taulo za kike kwa wanafunzi wa shule hiyo, huku akiwataka wanafunzi kujituma katika masomo na kuwa walinzi wa amani ya Taifa. Akizungumza katika hafla ya kukabidhi Projector ya kufundishia pamoja na Taulo za Kike katika shule ya sekondari Mwembeni, Mhe. Agnes Marwa Mbunge viti Maalumu Mkoa wa Mara, amesema ndoto yake ni kuona Shule ya Sekondari Mwembeni ikitajwa miongoni mwa shule zinazofanya vizuri kitaifa, akisisitiza kuwa mafanikio hayo yatapatikana kupitia nidhamu, juhudi na kujituma kwa wanafunzi. "Natamani sana kuisikia Mwembeni iking'ara kitaifa. Ninyi ndiyo mtakaolibeba na kulipandisha jina la shule yenu. Kumbukeni kuwa elimu mnayoipata ni uwekezaji wa maisha yenu wenyewe, hivyo jitumeni kwa bidii ili kutimiza ndoto zenu," amesema Mhe. Agnes. Mhe. Agnes amesema msaad...

TANZANIA KINARA WA HIFADHI YA GRAPHITE AFRIKA, MAHITAJI YA LITHIUM YAENDELEA KUONGEZEKA DUNIANI

 📍_Dar es Salaam_ Mjiolojia kutoka Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Njombe, Abbas Mruma, amesema Tanzania inaendelea kujijengea nafasi muhimu duniani kutokana na kuwa na hifadhi kubwa ya madini muhimu ya kimkakati, yakiwemo graphite, lithium na rare earth elements, ambayo ni nguzo muhimu katika maendeleo ya teknolojia za kisasa na nishati safi. Mruma ameyasema hayo wakati akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Richard Stanslaus Muyungi, alipotembelea banda la Tume ya Madini katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba). Amesema mahitaji ya madini ya lithium yanaendelea kuongezeka kwa kasi duniani kutokana na matumizi yake katika utengenezaji wa betri za magari ya umeme, simu za mkononi, kompyuta mpakato (laptops) na vifaa vingine vya kisasa vya kielektroniki. Amefafanua kuwa nchini Tanzania, madini ya lithium yanapatikana zaidi katika maeneo ya Dodoma na Ikungi, mkoani Singida. Akizungumzia madini ...