Na Mwandishi Wetu, BRUSSELS KAMPUNI ya ndege ya Brussels Airlines ya nchini Ubelgiji imeandika historia mpya kwa kutangaza kuanza kwa safari za moja kwa moja kati ya Brussels nchini Belgium na Kilimanjaro International Airport kuanzia Juni 3, 2026. Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, safari hizo zitafanyika mara mbili kwa wiki, kila Jumatano na Jumamosi, hatua inayotajwa kuwa chachu mpya kwa sekta ya usafiri wa anga, biashara na utalii nchini Tanzania. Uzinduzi wa safari hizi unaonekana kufungua ukurasa mpya wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Ubelgiji huku ukirahisisha usafiri kwa watalii, wafanyabiashara na wananchi wa pande zote mbili. Kuanzishwa kwa safari hizi za moja kwa moja kunatarajiwa kuongeza ushindani wa huduma za usafiri wa anga kwa kupunguza muda wa safari na kutoa chaguo zaidi kwa abiria wanaosafiri kati ya Afrika Mashariki na Ulaya. Aidha, hatua hiyo inatajwa kuwa muhimu katika kukuza biashara ya ki...
Marato tv - Sauti ya Jamii