📍Njombe MKOA wa Njombe unatarajiwa kuwa kitovu kipya cha uchumi wa madini nchini kufuatia uwekezaji mkubwa katika miradi ya uchimbaji na uchakataji wa madini ya chuma inayolenga kufungua maelfu ya ajira, kukuza biashara za ndani na kuongeza mapato kwa wananchi wa Wilaya ya Ludewa. Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Njombe, Mhandisi Lucas Mlekwa, amesema tayari moja ya miradi mikubwa inayosimamiwa na Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) kwa kushirikiana na kampuni ya kigeni imepata Leseni Kubwa ya Uchimbaji wa Madini baada ya utafiti wa kina uliofanyika kati ya mwaka 2012 na 2013 kubaini uwepo wa zaidi ya tani milioni 126 za madini ya chuma. Amesema tafiti hizo pia zimeonesha uwepo wa madini mengine yenye thamani kubwa yanayoambatana na chuma ikiwemo titanium na vanadium, hatua inayoongeza thamani ya kiuchumi ya mradi huo kwa Taifa. “Kwa sasa tupo katika hatua za mwisho za kukamilisha makubaliano kati ya Serikali na wawekezaji, na tunatarajia ndani ya mwaka mmoja utekelezaji rasmi wa mr...
Marato tv - Sauti ya Jamii