Skip to main content

Posts

Showing posts from March 31, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Tofauti za Mishahara Kwa Watumishi wa Umma Kushughulikiwa-Waziri Mkuu

Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba, amesema Serikali imebaini kuwepo kwa tofauti kubwa ya mishahara kati ya watumishi wa umma na wale wa sekta binafsi, hali inayohitaji hatua za haraka ili kurekebisha uwiano huo. Akiwasilisha hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2026/2027 bungeni jijini Dodoma, Dkt. Nchemba amesema jumla ya watumishi wa umma 7,447 wanapokea mishahara isiyoendana na majukumu yao, ambapo hadi Machi 26 mwaka huu, walilipwa mishahara ya binafsi yenye gharama ya shilingi bilioni 14.34. Amesema Serikali imeona umuhimu wa kuchukua hatua za kupunguza tofauti hiyo kwa kuwianisha viwango vya mishahara ili kuhakikisha malipo yanalingana na kazi zinazofanywa na kuondoa upungufu uliopo kwa baadhi ya watumishi. Aidha, Serikali imepanga kuhuisha sheria ya utumishi wa umma pamoja na kanuni zake zinazohusu utoaji wa vibali vya mishahara binafsi, sambamba na kufanya mapitio ya waraka unaohusu utaratibu wa kushughulikia maombi hayo ili kuongeza uwazi na ufanisi. Hatua hi...

Mheshimiwa Lukuvi Atakumbukwa Kwa Mengi -Waziri Mkuu

WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amesema aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) na Mbunge wa Isimani, Mheshimiwa William Lukuvi atakumbukwa kwa mengi na Watanzania kutokana na utumishi wake uliotukuka katika nafasi mbalimbali alizohudumu. “Mheshimiwa Lukuvi atakumbukwa kwa mengi na Watanzania kutokana na utumishi wake uliotukuka katika nafasi mbalimbali. Mchango wake kwa Jamii na Watanzania kwa ujumla katika nafasi mbalimbali alizotumikia kuanzia Chama, Jimboni na Serikalini umekuwa chachu katika kuleta maendeleo kwa wananchi,” amesema Waziri Mkuu ambaye ameongoza mazishi hayo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumanne, Machi 31, 2026) wakati akizungumza katika ibada ya mazishi ya marehemu iliyofanyika nyumbani kwake kwenye kijiji cha Idodi, wilayani Iringa, mkoani Iringa. "Kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan nitumie nafasi hii k...