Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa 11 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Nchi za Afrika, Karibiani na Pasifiki (OACPS), uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Sipopo kilichopo Jijini Malabo nchini Guinea ya Ikweta. Katika ufunguzi wa Mkutano huo, salamu za Viongozi mbalimbali zimesisitiza umuhimu wa hitaji la kufanya mageuzi ya Kitaasisi na kimfumo kuwezesha Jumuiya ya Nchi za Afrika, Karibiani na Pasifiki (OACPS) kukabiliana na changamoto zinazoikabili Dunia kwa sasa ikiwemo, migogoro ya kisiasa, vita pamoja na mabadiliko ya tabianchi. Vilevile, Ufunguzi wa Mkutano huo, umeweka mkazo kwa nchi wanachama kutoa michango kwa wakati ili kuifanya Taasisi ya OACPS kujitegemea kifedha na kuwa sauti huru kwenye jumuiya ya kimataifa. Pia msisitizo umewekwa katika kutumia vema rasilimali watu ambao ni bilioni 1.5 waliopo ...
Marato tv - Sauti ya Jamii