WAZIRI Mkuu mstaafu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amemuelezea Hayati Rais John Magufuli kuwa ni mtu mkali, ambaye hakupenda mzaha katika mambo yake, alikuwa mchpakazi, Mzalendo na alikuwa kiongozi Mwenye akili nyingi katika kutekeleza Majukumu yake kiufasaha. Amesema Uzalendo unajengwa Kwa unajengwa na uwajibikaji. Waziri Mkuu Mstaafu kasimu Majaliwa ameyasema hayo leo katika kumbukizi ya miaka mitano ya kifo cha Hayati rais Dk.John Magufuli Machi 17 katika viwanja vya makazi yake Chato mkoani Geita, Majaliwa amewataka Watanzania kuiga mambo mazuri yaliyofanywa na kiongozi huyo. Amesema yeye alikuwa ni mtu mkweli, hakuwa na mzaha katika mambo yake yaani mkali , alikemea maovu, wezi, wala rushwa, wabadhirifu wa mali za umma, na yule ambaye hakufuata misingi hii aliachana nae huo ndiyo ulikuwa utaratibu wake “Leo hii tunamkumbuka Hayati Magufuli, sisi ambao tulikuwa karibu naye tumeweza kushuhudia wakinufaika na busara zake, hekima zake katika kuongoza taifa hili, na kutambua r...
Marato tv - Sauti ya Jamii