Skip to main content

Posts

Showing posts from March 3, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Prof. Shemdoe Aelekeza Maafisa Wanaosimamia Mradi Wa Lishe Kupatiwa Usafiri

Na OWM - TAMISEMI, GEITA Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu -TAMISEMI Mhe. Prof. Riziki Shemdoe ameelekeza Maafisa Lishe na Maendeleo ya Jamii wanaosimamia utekelezaji wa Mradi Jumuishi wa Lishe katika Mkoa wa Geita, Tabora na Iringa kupatiwa vyombo vya usafiri ili waweze kwenda kutoa huduma kwenye maeneo yanayokabiliwa na matatizo ya lishe kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano. Prof. Shemdoe ametoa maelelezo hayo leo Machi 03, 2026, wakati akizindua Mradi Jumuishi wa Lishe katika Mkoa wa Geita, ambao utawawezesha watoto wa  mkoa wa Geita kukua vizuri kimwili na kiakili, na kuwa na nguvu na afya bora.  “Katibu Mkuu na wataalam mnaosimamia mradi huu, hakikisheni kupitia bajeti za mradi mnawapatia Maafisa Lishe na Maendeleo ya Jamii vyombo vya usafiri katika halmashauri zote zinazotekeleza mradi huu ili waweze kutoka sehemu moja kwenda nyingine kuwahudumia watoto,” amesisitiza Prof. Shemdoe. Prof. Shemdoe amesema, kipekee anashukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa...

Chadema Yatakiwa Kutii Sheria za Nchi

  Mwanasheria na Wakili, Gido Thomas Simfukwe amewataka wanachama wa chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) kutii utawala wa kisheria huku akishangashwa kuona baadhi ya viongozi wachama wajiandaa kufanya shughuli za kichama hali ya kuwa shauri husika likiwa bado lipo mahakamani. Hayo amebainisha leo, machi 3, 2026, jijini Dar es Salaam na Wakili Gido Thomas Simfukwe wakati akitoa mrejesho wa usikilizwaji wa mashauri ya mgawanyo wa mali na shughuli za kisiasa katika kesi NA. 8323 ya mwaka 2025 iliyofunguliwa na Saidi Issa Mohammed na wenzake dhidi ya chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) ambapo amesisitiza kuwa kupanga, kutangaza na kuandaa makongamano na mikutano ya kisiasa si sahihi kwani yamezuiliwa kwa amri ya Mahakama tangu tarehe 10 juni 2025. Aidha, wakili Simfukwe amesema kuwa kumekuwa na baadhi ya watu wamekuwa wakitia dhana ya kuwa shauri hilo lililetwa na kikundi cha watu wachache hali ambayo si sahihi bali ni uwepo wa wanachama wenye nia ya kuona chama kina...

Tume ya Uchunguzi Yakutana na Wahariri wa Vyombo Vya Habari

*DAR ES SAALAM:*  TUME ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, leo Machi 3, 2026 imekutana na Wahariri wa vyombo vya Habari nchini. Mkutano huo wa Tume na Wahariri umefanyika katika ukumbi wa Kilimanjaro uliopo jengo la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) mkoani hapa, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Tume kukusanya taarifa, maoni na ushauri kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo wataalamu, watu wa kawaida, viongozi wa sasa na wastaafu. Katika mkutano huo hoja zilizojadiliwa zilihusu chanzo na tathmini ya athari za matukio hayo ndani ya nchi na kimataifa na ushauri wa hatua za kijamii na kisheria zinazochukuliwa ili kuimarisha amani, mshikamano wa kitaifa na matukio hayo yasijirudie tena. Tume inaendelea na mahojiano na waathirika wa Matukio hayo baada ya hivi karibuni Mamlaka ya Uteuzi kuiongezea Tume muda wa siku arobaini na mbili (42) kuanzia tarehe 20 Februari, 2026 ili Tume iweze kukamilisha uchunguzi wa matukio ya uvunj...

Tume ya Uchunguzi Yakutana na Abdulrahman Kinana

DAR ES SAALAM:  TUME ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, leo Machi 2, 2026 imekutana na mwanasiasa mkongwe wa Chama cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania, Abdulrahman Kinana. Mkutano huo wa Tume na Kinana umefanyika katika ukumbi wa Tanganyika uliopo jengo la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) mkoani hapa, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Tume kukusanya taarifa, maoni na ushauri kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo wataalamu, watu wa kawaida, viongozi wa sasa na wastaafu. Katika mkutano huo hoja zilizojadiliwa zilihusu maeneo ya tathmini ya athari za matukio hayo ndani ya nchi na kimataifa na ushauri wa hatua za kijamii na kisheria zinazochukuliwa ili kuimarisha amani, mshikamano wa kitaifa. Tume inaendelea na mahojiano na waathirika wa Matukio hayo baada ya hivi karibuni Mamlaka ya Uteuzi kuiongezea Tume muda wa siku arobaini na mbili (42) kuanzia tarehe 20 Februari, 2026 ili Tume iweze kukamilisha uchunguzi wa matukio...

Mbunge Agness Aunga Juhudi za Rais Samia Kwa Kuwezesha Vijana Kwa Vitendo

 MUSOMA. KATIKA kuunga mkono jitihada za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuwawezesha vijana,Mbunge wa viti maalumu mkoa wa mara Mhe, Agness Marwa amegawa vitendea kazi vya saloon za kike na kiume Kwa vijana zaidi 30 katika manispaa ya Musoma mkoa wa Mara. Dhamira hiyo ni kuwawezesha vijana kujikwamua kiuchumi na kuunga mkono serikali katika kuwawezesha wajasiriamali wadogo. Akizungumza katika kikao cha wajasiliamali leo March 3,2026 katika Manispaa ya Musoma, Mbunge Agnes amesema ataendelea kuyafukia makundi mablimabli wakiwemo wajasiliamali Mali wote katika mkoa wa mara. Mhe. Agnes amesema azma hiyo ni kuunga mkono jitihada za mheshimiwa rais Samia Suluhu Hassan zinazojikita kuwasaidia wajasiliamali wadogo wadogo katika kujikwamua kiuchumi. Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Manispaa ya Musoma Juma Chikoka amempongeza Mbunge huyo ambapo amewataka wajasiliamali hao kuvitumia vifaa hivyo Kwa Lengo lililokusudiwa ili kujiongezea kipato. Nao baadhi ya wajasiliamalia mali wamempongeza ...