Tanzania imetoa wito kwa nchi za Afrika kuongeza kasi ya kuunganisha miundombinu ya usafiri, nishati na mifumo ya kidijitali ili kurahisisha biashara, kuimarisha minyororo ya thamani na kujenga uchumi wa bara wenye uwezo wa kukabiliana na misukosuko ya kimataifa. Akizungumza kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mkutano wa 8 wa Kamati ya Uratibu ya Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika uliofanyika El Alamein, Misri, Makamu wa Rais Mhe. Deogratius John Ndejembi amesema changamoto za hivi karibuni za kiuchumi zimeonesha umuhimu wa Afrika kuharakisha ujenzi wa viwanda, kuongeza biashara baina ya nchi zake na kuimarisha miundombinu inayounganisha masoko ya bara. Makamu wa Rais ametaja uwekezaji wa Tanzania katika TAZARA, Reli ya Kisasa ya SGR, bandari, usafiri wa anga na miradi ya kuunganisha mifumo ya umeme ya Afrika Mashariki na Kusini kuwa sehemu ya jitihada za kurahisisha biashara, kuimarisha usalama wa nishati na kucho...
Marato tv - Sauti ya Jamii