Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unaendelea kutekeleza Mradi wa usambazaji wa mitungi ya gesi ya kilo 6 kwa bei ya ruzuku, ambapo inatarajia kugawa mitungi 26,040 katika mkoa wa Tanga, Mradi huo utagharimu jumla ya shilingi milioni 455. Mkuu wa mkoa wa Tanga, Mhe. Balozi, Dkt. Batilda Burian, tarehe 17 Desemba, 2024 ameupokea rasmi Mradi huo wa kusambaza mitungi ya gesi kwa Wananchi wa mkoa wa Tanga, ambapo mkoa unataraji kuanza zoezi la kusambaza mitungi hiyo kwa Wananchi mwezi Januari, 2025. REA, iliingia mkataba na mtoa huduma; kampuni ya Manjis Logistic Ltd, kampuni ambayo, itahudumia wilaya 8 za Mkoa wa Tanga kwa kuuza mitungi hiyo ya gesi ya kilo 6 kwa bei ya ruzuku ya shilingi 17,500 pamoja na vifaa vyake, katika maeneo ya vijijini na pembezoni mwa miji. Mhe. Balozi, Dkt. Batilda Burian, amewaomba REA kuhakikisha kuwa teknolojia za nishati safi ya kupikia, zinapatikana kwa wakati na kuwafikia Wananchi muda wote ili kuhakikisha matumizi ya nishati safi yanakuwa endelevu. Mku...
Marato tv - Sauti ya Jamii