Skip to main content

Posts

Showing posts from October 6, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Rais Mwinyi kushiriki siku ya wazee pemba

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amewasili Pemba kushiriki maadhimisho ya siku ya Wazee duniani. Katika uwanja wa ndege wa Pemba, Rais Dk. Mwinyi akiwa na Mama Mariam Mwinyi , walipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mattar Zahor Masoud na Viongozi mbalimbali wa Serikali, Chama Cha Mapinduzi na Vyombo vya Ulinzi na Usalama.  Dk. Mwinyi atakuwa Mgeni Rasmi kwenye kilele cha maadhimisho ya siku wa Wazee duniani ambayo kwa Zanzibar yanaadhimishwa viwanja vya Tibirinzi, Wilaya ya Chake chake, Mkoa wa Kusini Pemba, leo tarehe 07 Oktoba, 2024.

Tanzania na Comoro zajadiliana kushirikiana katika ngazi ya miji

Balozi wa Tanzania nchini Comoro Mhe. Saidi Yakubu amekaribishwa rasmi katika mji wa Bangoi Kuoni na kuzungumza na uongozi wa mji huo kuhusu ushirikiano na miji ya Tanzania. Katika hafla hiyo ambapo wakazi wa mji huo walimvika rasmi ukaazi wa heshima Balozi Yakubu, viongozi wake walimueleza pia kuwa huo umekuwa ni utamaduni wao wa kushirikiana na Mabalozi wa Tanzania nchini Comoro na kumueleza historia ya mji huo na Tanzania hususan Zanzibar na Tanga. Aidha, walimueleza kuwa viongozi wa Tanzania waliowahi kutembelea mji huo ni pamoja na Marehemu Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, Rais wa Zanzibar Mstaafu Amani Abeid Karume, Kiongozi wa Upinzani wa Zanzibar, Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad na pia kumtajia viongozi kadhaa wa Tanzania wenye asili ya mji huo. Kwa upande wake, Balozi Yakubu alishukuru kwa kutuzwa Ukaazi wa Heshima na kuwaahidi kuendeleza utamaduni huo na kutekeleza masuala yote yalioahidiwa na Mabalozi waliomtangulia ikiwemo kuwasaidia kuwa na darasa mahsusi la Kiswahili kwa...

Waziri mkuu aagiza watumishi wanne kigamboni wafikishwe mahakamani

*Aagiza kusimamishwa kazi kwa Bi. Annie Maugo wa Kitengo Jumuifu cha Amana, TAMISEMI *Aipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kwa kuchukua hatua za awali. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameelekeza kufikishwa mahakamani mara moja kwa maafisa wanne wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni na watumishi wanne wa kitengo cha Akaunti Jumuifu ya Amana (TSA) kilichopo TAMISEMI kwa tuhuma za ubadhirifu wa shilingi milioni 165.6. Aidha ameagiza Bi. Annie Nyabugumba Maugo wa Kitengo cha Akaunti Jumuifu ya Amana asimamishwe kazi kutokana na ushiriki wake kwenye muamala uliohamisha fedha kutoka TAMISEMI kwenda katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni. Ametoa maagizo hayo leo (Jumapili, Oktoba 06, 2024) wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi. Waziri Mkuu yupo mkoani Dar es Salaam kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. Mheshimiwa Majaliwa amefikia maamuzi hayo kutokana na uchunguzi uliofanywa na ...

Udini ni hatari,kuchoma nguo ni utoto;Nchimbi

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amewahimiza Watanzania kuendelea kushirikiana na CCM, akisisitiza kuwa chama hicho kimeonyesha kwa vitendo uwezo wa kuongoza nchi na dhamira ya kuwahudumia wananchi wanyonge. Dkt. Nchimbi alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Lamadi, Wilaya ya Busega na Kata ya Dutwa, wilayani Bariadi, mkoani Simiyu, kwa nyakati tofauti leo, tarehe 6 Oktoba 2024. Hii ni sehemu ya ziara yake ya kikazi ya siku tatu katika mkoa huo, ambapo alieleza kuwa CCM imekuwa ikiandaa viongozi wake kwa ufanisi. “Kiongozi aliyeandaliwa vizuri hueleza mipango yake waziwazi anapopewa nafasi, kwamba nikitwaa madaraka, nitafanya moja, mbili, tatu. Lakini kiongozi ambaye hajakomaa, akipewa nafasi ya kuzungumza anaanza kuhamasisha maandamano, kuchoma nguo, au kuzomea watu. Hapo unajua bado hajakomaa na anahitaji muda wa kujifunza zaidi.” “Katika CCM, hatuna viongozi wanaoshikilia madaraka kwa miaka 40. Viongozi wanachaguliwa,...

Dr. nchimbi apokelewa Simiyu kwa Kishindo

HODI SIMIYU, NCHIMBI AKIANZA ZIARA YA SIKU 3 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akizungumza na wananchi wa Lamadi, Wilaya ya Busega, Mkoa wa Simiyu, leo tarehe 6 Oktoba 2024, ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake ya siku tatu mkoani humo.  Balozi Nchimbi ambaye ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Ndugu Amos Makalla na Katibu wa NEC - Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (Suki), Ndugu Rabia Hamid Abdalla, ameanza ziara mkoani Simiyu kwa ajili ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020 - 2025, kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi, kukagua uhai wa Chama kuanzia ngazi ya mashina na pia kuhamasisha wananchi kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, utakaofanyika mwezi Novemba, mwaka huu.

Waziri mkuu ameagiza sekta binafsi kushirikishwa katika mipango ya maendeleo

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka watumishi wa halmashauri nchini kuendelea kuweka mikakati ya kushirikisha sekta binafsi katika mipango ya kimaendeleo. Amesema kuwa kwa kufanya hivyo kutasaidia kuongeza wigo wa utoaji huduma kwa wananchi  na uzalishaji wa bidhaa ikiwemo za kwenye sekta ya mifugo. Amesema hayo leo (Jumapili, Oktoba 06, 2024) wakati alipozungumza na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa chuo cha Maendeleo ya Wananchi. Waziri Mkuu yupo mkoani Dar es Salaam kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. “Sera yetu ndani ya Serikali inahamasisha sekta binafsi kuwekeza na kutoa huduma, katika idara yako ni lazima ujiulize sekta binafsi imechangia kiasi gani katika kutoa huduma”. Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amewataka madiwani kwenye halmashauri zote nchini kushiriki katika kufanya makadirio ya makusanyo kwenye halmashauri zao kwa kushirikiana na watendaji wa Halmashauri, Kata na Vijiji. “Baraza la Madiwani kafanyeni Surve...