Skip to main content

Posts

Showing posts from September 19, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Mdau wa Maendeleo mkoani Geita atoa msaada kwa waandishi wa habari

Mdau wa maendeleo Mkoani Geita, ambaye pia ni Katibu wa Elimu, Malezi na Mazingira, Paschal Mapung'o, leo ametimiza ahadi yake kwa kikundi cha wanahabari cha Geita Media Group (GMG). Katika hafla hiyo, Mapung'o amekabidhi televisheni pamoja na kisimbuzi kwa kikundi hicho ambacho kinajihusisha na uandishi wa habari ndani ya Halmashauri ya Mji wa Geita. Akiwa anakabidhi msaada huo, Mapung'o alieleza kuwa lengo ni kuwasaidia wanahabari wa GMG kuboresha shughuli zao za utoaji wa habari kwa umma kwa kuwa na nyenzo za kisasa. Aliwahimiza kuendelea kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia maadili ya taaluma yao kwa maslahi ya jamii nzima ya Geita. Kikundi cha GMG, kinachoongozwa na wanahabari wa eneo hilo, kilipongeza msaada huo na kusema kuwa ni chachu ya kuimarisha uwezo wao wa kutoa habari bora kwa jamii, hususan katika kueneza taarifa zinazohusu maendeleo ya mkoa wa Geita. Msaada huu unatarajiwa kuboresha ushirikiano kati ya wadau wa maendeleo na wanahabari katika kuhakikisha taa...

Mbunge Mavunde azindua ujenzi wa Jengo la Mapumziko Hospitali ya Mkoa Dodoma

Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini, Anthony Mavunde amezindua ujenzi wa jengo la mapumziko la wananchi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na kusema kuwa ujenzi huo ni sehemu ya utatuzi wa changamoto zinzazowakabili wananchi. Mavunde amesema kuwa nje ya jengo hilo kuna eneo ambalo wanakaa wananchi ambao asilimia kubwa hawaishi katika Jiji la Dodoma na wanatumia sehemu ile kama sehemu ya kupumzikia kwa ajili ya kusubiri muda wa kuwaona wagonjwa wao.  Ameongeza ujenzi wa Jengo hilo ni muhimu kutokana na kuwepo kwa baadhi ya watu ambao hawana sehemu ya kulala na hawana makazi Dodoma na hawawezi kurudi walipotoka kwasababu ya umbali na gharama za usafiri. Kwa mujibu wa mbunge huyo ambaye pia ni Waziri wa Madini kuna wakati mwingine wakina mama,baba na watoto wanachanganyikana na kulala sehemu moja. "kulingana na maadili ya kitanzania sio vema sana kuchanganyika watu wa jinsi tofauti sehemu moja na hasa ambao kwa namna moja au nyingine hawana uhusiano wowote. jambo hili lilinigusa...

Balozi Nchimbi afanya mazungumzo na Balozi wa Brazil nchini

  Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Brazil nchini Tanzania, Mhe. Gustavo Martins Nogueira, kuhusu masuala mbalimbali ya kuimarisha uhusiano kati ya Brazil na Tanzania, leo tarehe 19 Septemba 2024, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar Es Salaam.

Rais Dkt.Samia Amuapisha Ndugu Baraka IIdephonce Leonard Kuwa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Ndugu Baraka Ildephonce Leonard kuwa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye hafla fupi ya Uapisho iliyofanyika Ikulu, Jijini Dar es Salaam tarehe 19 Septemba, 2024.

Dkt. Kiruswa ashuhudia utiaji saini mikataba ya utoaji huduma migodini

*Atatua Mgogoro kati ya Kampuni Mantra na Wananchi uliodumu zaidi ya miaka 11* *Akagua maendeleo ya mradi wa uchimbaji Madini ya Urani Namtumbo* *Ashiriki Ukaguzi wa ujenzi wa miundombinu ya Uwanja wa Ndege Ruvuma* Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa ameshuhudia Utiaji Saini wa Mikataba ya usambazaji na utoaji wa huduma mgodini katika mgodi wa uchimbaji Madini ya Urani uliopo katika Kijiji cha Likuyu kilichopo Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma. Mikataba hiyo imesainiwa Septemba 18, 2024 ambayo imehusisha Kampuni ya Ako Group Tanzania Limited ambayo ni mzabuni wa Kampuni ya Mantra na vikundi vilivyoundwa na wazawa vitakavyo toa mahitaji mbalimbali kwa mzabuni huyo. Ako Group wanatoa huduma ya chakula na usafi katika mradi huo, hivyo mikataba hiyo itasaidia ununuzi wa mahitaji muhimu ya chakula na usafi kufanyika ndani ya Wilaya ya Namtumbo na kukuza uchumi wa jamii hiyo.   Aidha, Dkt. Kiruswa amekagua maendeleo ya mradi wa uchimbaji Madini ya Urani katika mgodi wa Mantra ...

Rais Dkt. Samia Amuapisha Nenelwa Joyce Mwihambi Kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Ndugu Nenelwa Joyce Mwihambi kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania kwenye hafla fupi ya Uapisho iliyofanyika Ikulu, Jijini Dar es Salaam tarehe 19 Septemba, 2024.

Tume ya madini yapata mkurugenzi mpya wa huduma za tume

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Huduma za Tume, CPA. William Mtinya amekabidhi Ofisi kwa Nsajigwa Kabigi aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Usimamizi wa Rasilimali watu kutoka Wizara ya Afya. Akizungumza kwenye ofisi za makao makuu ya Tume ya Madini jijini Dodoma mbele ya Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Ramadhani Lwamo,CPA Mtinya ameshukuru watendaji wa Tume ya Madini kwa ushirikiano mkubwa waliouonesha tangu aliposhika nafasi hiyo na kuwataka kuendelea kumpa ushirikiano Kaimu Mkurugenzi mpya wa Huduma za Tume. Naye Kaimu Mkurugenzi Mpya wa Huduma za Tume, Nsajigwa Kabigi ameomba watumishi wote wa Tume ya Madini kuendeleza ushirikiano ili kuhakikisha Sekta ya Madini inaendelea kuwa na mchango mkubwa kwenye Pato la Taifa. Amesisitiza kuwa Ofisi yake itaendelea kutatua changamoto mbalimbali sanjari na kuboresha mazingira ya ofisi zote za madini nchini kwa kuhakikisha zinapata vitendea kazi ili kutoa huduma za uhakika kwa wadau wa madini waliopo katika maeneo mbalimbali nchini. Wa...

Waziri Mavunde atekeleza ahadi kwa vitendo

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony MAVUNDE ametimiza ahadi yake ya kuwapatia Vijana wa Hamasa wa Chama Chamapindizi(CCM)Dodoma Mjini vifaa ikiwemo seti moja ya Matarumbeta na Ngoma kwa ajili ya kuchagiza shughuli mbalimbali.  Akikabidhi vifaa hivyo,Mavunde ambaye pia ni Waziri wa Madini amewaasa vijana hao kuvitumia vifaa vilivyotolewa kama kitega uchumi cha kujiongezea mapato kupitia sherehe mbalimbali. Matarumbeta na Ngoma yamegharimu shilingi millioni mbili na nusu huku Mavunde akiahidi Kuongeza seti nyingine mbili ili kuboresha huduma inayotolewa na vijana hao kwenye sherehe mbalimbali.  Mbali na Matarumbeta na Ngoma,Mavunde pia amewapatia vijana wa Hamasa(CCM)Dodoma Mjini mashine ya kufyatua matofali yenye thamani ya shilingi millioni kumi.  Kwa upande wake,Uongozi wa Vijana wa Hamasa(CCM)Dodoma Mjini wamemshukuru Mbunge Mavunde kwa kutimiza ahadi yake kuwapatia vifaa hivyo na kuahidi kuvitumia kwa malengo yaliyokusudiwa ya kujiongezea kipato. 

Serikali kujenga vituo vya zana za kilimo nchi nzima

Serikali imetangaza kujenga vituo vya zana za kilimo nchi nzima pamoja na kuanza kugawa ruzuku ya mbegu za mahindi. Hayo yameelezwa na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe wakati wa ziara yake katika kituo cha ununuzi wa mahindi Madaba ambapo ameahidi kula sahani moja na walanguzi wanaowanyonya wakulima nchini.  Amesema kuwa Serikali inatambua adha wanayokutana nayo wakulima kutokana na uhaba wa Zana za kilimo pamoja na maumivu yatokanayo na kukodi Trekta, pawatila pamoja ulanguzi katika mbegu na mbolea. “Rais Samia Suluhu Hassan kwa nia ya dhati kabisa ameamua na kutenga fedha za kujenga zaidi ya vituo 45 vya zana za kilimo nchi nzima ili kutatua changamoto zinazowakabili wakulima,”amesema. Vituo hivyo vitakuwa na zana za kilimo kama matrekta na zana zake zikiwemo plau, haro, planters, boom sprayers na tela za kusafirishia mizigo pamoja na Combine Harvester Waziri Bashe ameitaja mikoa itakayonufaika na awamu ya kwanza ya ujenzi huo kuwa ni Mwanza,Simiyu,Geita,ShinyangKigoma,Mara,Tabora,...

Waziri Bashe awataka wakulima na wafugaji kuishi kwa amani

  Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amewaasa wafugaji wa jamii ya Wasukuma wanaoishi katika kata ya Ndalila Wilayani Songea, kuhakikisha kuwa wanaishi kwa amani na wakulima wa jamii zingine wilayani humo. Bashe amesema hayo akiwa katika kata ya Njalila  Wilayani Songea wakati wa mwendelezo wa ziara yake kukagua miradi ya kilimo  katika mikoa mbalimbali nchini ambapo amezungumza na wananchi kuhusu kero zao na mipango ya serikali katika kutatua kero hizo.  Ameelekeza viongozi wa taasisi za serikali kuchukua hatua na kufanya usanifu wa barabara na bwawa kwa ajili ya kumwagilia hekari 6000, pamoja na kujenga zahanati na kituo cha afya.  “Mkurugenzi wa Umwagiliaji na mhandisi wa Umwagiliaji mkoa pia yupo hapa, Kwa mwaka huu tutaanza na usanifu ambapo wataalamu watakuja kwa ajili ya kujua gharama, na masuala mengine muhimu kabla ya Kuanza utekelezaji”, alisema Bashe na kuongeza kuwa ”Serikali ifanye usanifu wa barabara kwa ushirikiano wa TARURA na Tume ya Taifa ya Umwagi...

Waziri Mkuu kumwakilisha Rais Unga79

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameondoka nchini leo (Alhamisi, Septemba 19, 2024) kwenda Marekani ambako atamwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano wa 79 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA79). Mkutano huo unaotarajiwa kufanyika kuanzia Septemba 20-26, 2024, utafanyika jijini New York, Marekani ambapo masuala ya kiuchumi, biashara, nishati, siasa, mazingira, afya, vijana na watoto yatajadiliwa. Masuala mengine ni ya maji, bahari, athari za hali ya hewa na haki za binadamu. Katika mkutano huo ambao hufanyika kila mwaka, viongozi wa nchi mbalimbali wanatarajiwa kushiriki mijadala tofauti chini ya mada kuu ambayo ni “Hakuna kuachwa nyuma yeyote: Kushirikiana pamoja kuendeleza amani, maendeleo endelevu na heshima ya binadamu kwa vizazi vya sasa na vijavyo" (Leaving no one behind: Acting together for the advancement of peace, sustainable development and human dignity for present and future generations). Mbali na kukuza diplomasia, ushiriki wa Tanzania kwenye mkutano hu...