Skip to main content

Posts

Showing posts from January 4, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema kifo cha Jaji Werema ni pigo kwa Tasnia ya Sheria nchini

  Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe Hamza Johari amesema tasnia ya sheria nchini imepata pigo kubwa kufuatia kifo cha mwanasheria mkuu wa Serikaki mstaafu na Jaji mstaafu wa mahakama kuu Frederick Mwita Werema.  Ametoa kauli hiyo katika kijiji cha Kongoto wilaya ya Butiama mkoani Mara,wakati wa mazishi Jaji Werema, yaliongozwa na Jaji mkuu wa Tanzania mh Prof Ibrahim Juma, januari 4-2025. Akitoa salamu za Pole, Mwanasheria huyu Mkuu wa Serikali, amesema kuwa Jaji Werema alijitolea kwa hali na mali katika kuhakikisha kwamba Serikali inatekeleza majukumu yake kwa kufuata sheria na kwa uwazi.  Alipambana na changamoto nyingi zilizokuwa zikiikabili tasnia ya sheria na hakusita kuanzisha mabadiliko yaliyoleta matokeo chanya kwa wananchi na taifa kwa ujumla.  Huu ni urithi mkubwa ambao utaendelea kuwa mfano na msingi wa kazi yetu sote tunaoendelea nayo leo.  Aidha, Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesisitiza kuienzi na kuiendeleza misingi na mifumo ya sheria aliyoianzish...

Viongozi wa dini nchini Jamhuri ya Afrika ya kati Waishukuru Jwtz

Umoja wa Viongozi wa madhehebu ya dini nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wameonesha imani kubwa ya ulinzi wa amani unaotolewa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania nchini humu. Wakizungumza kwa nyakati tofauti mara baada ya kutembelewa na Kamanda wa Kikosi cha Nane cha Ulinzi wa Amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati Luteni Kanali Theofili Nguruwe wamesema uwepo wa JWTZ umekuwa na tija sana nchini humo kwani wamekuwa wakifanya kazi zao kwa weledi wa hali ya juu. Akizungumza kwa niaba ya Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Berberati Mhashamu Koffi Denis, Karibu Mkuu wa Jimbo hilo Padre Jean Ancelimo amesema mbali na Ulinzi wa Amani pia limekuwa likitoa misaada mbalimbali ya hali na mali huku akitolea mfano wa ujenzi wa shule ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ambayo imepewa jina la Serengeti. Naye Askofu Mkuu wa Kanisa la Evenjeliko (AEC) Mhashamu Lucian Nday amesema uwepo wa JWTZ nchini hapo umewafanya waishi kwa amani na zaidi ya yote limewezesha ukuaji wa lug...

Rea kusambaza mitungi ya gesi ya kilo sita mkoani Njombe

* Mitungi ya gesi 13,020 kusambazwa mkoani Njombe * Kila wilaya kupatiwa mitungi ya gesi 3,255  Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeingia mkataba na mtoa huduma kampuni ya Taifa Gas Tanzania Limited ambaye atahudumia wilaya zilizopo ndani ya Mkoa wa Njombe kwa kuuza kwa bei ya ruzuku mitungi ya gesi ya kilo sita pamoja na vifaa vyake katika maeneo ya vijijini na pembezoni mwa miji. Hayo yamebainishwa leo Januari 4, 2025 mkoani Njombe na Mhandisi wa miradi wa REA, David Malima wakati wa uzinduzi rasmi wa mradi wa ugawaji mitungi ya gesi ya kilo sita Kata ya Tandala, Wilaya ya Makete mkoani Njomb. Mha. Malima amesema kuwa mitungi ya gesi 13,020 itakayosambazwa mkoani Njombe itachochea kwa kiasi kikubwa matumizi ya nishati safi na salama.  "Lengo la mradi ni kukuza, kuchochea, kuwezesha na kuboresha upatikanaji wa huduma za nishati safi ya kupikia ili kupunguza ukataji wa miti ambapo takribani hekta 400,000 hukatwa kila mwaka, " Amesisitiza Mha. Malima. Mha. Malima amesema, Se...