Skip to main content

Posts

Showing posts from July 2, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri wa Ulinzi na Jkt Azindua Mashindano ya Mkuu wa Majeshi Nchini

 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) Dkt. Stergomena Lawrence Tax, Julai 02 mwaka 2025 amezindua rasmi Mashindano ya Mkuu wa Majeshi (CDF CUP), huku akisisitiza umuhimu wa kudumisha uzalendo, amani, mshikamano ukakamavu ikiwa na lengo la kuunga mkono dhamira ya amiri jeshi mkuu na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania DK SAMIA SULUH HASSAN katika kukuza sekta ya michezo hapa nchini. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, katika uwanja wa AZAM COMPLEX Dkt. Tax amesema kwakua michezo ni nyenzo muhimu katika kuunganisha jamii na taifa kwa ujumla, ni dhahiri kuwa upo muhimu kwa jeshi na wananchi kushirikiana katika kuinua na kuiendeleza sekta hiyo kikamilifu ambayo pia licha michezo kuwa sehemu ya mazoezi lakini pia inalenga kupata wanamichezo watakashindana kupata timu za jeshi kwaajili ya kushiriki katika mashindano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa. Aidha DK TAX amempongeza mkuu wa majeshi nchini Jenerali Jacob John Mkunda kwa kuendeleza mashindano ya majeshi kwani lich...

Mhe. Rais Samia Apongezwa Kutekeleza Mkakati wa Taifa wa Nishati Safi ya Kupikia Kwa Vitendo

Na Ada Ouko, Musoma. JUMLA ya mitungi ya gesi 561 pamoja na majiko yake ya sahani mbili inatarajiwa kutolewa kwa Watumishi wa Jeshi la  Magereza Mkoa wa Mara.    Zoezi hilo ambalo limeanza kutekelezwa leo Julai 2, 2025 ambapo mitungi 81 na majiko yake imetolewa kwa Maafisa na Askari wa Gereza Musoma huku mitungi 480 na majiko iliyobaki itapelekwa katika Magereza 6 za mkoa huo. "Mei 8, 2024, Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan alizindua Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia. Toka kuzinduliwa kwa mkakati huo, Serikali imefanya juhudi mbalimbali kuhakikisha Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ili kuokoa mazingira pamoja na vifo vilivyokuwa vinatokana na matumizi ya nishati isiyokuwa safi na salama ya kupikia" Alisema Mjumbe wa Bodi ya Nishati vijijini(REB) Lucas Malunde wakati wa hafla  ya ugawaji wa mitungi hiyo. Malunde alizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi hiyo Mhe, Balozi Meja Jenerali (Mstaafu...

Asanteni Wana Ruangwa -Majaliwa

WAZIRI MKUU, na Mbunge wa Jimbo la Ruangwa Kassim Majaliwa leo Julai 2, 2025 ametangaza rasmi kutokugombea tena ubunge wa jimbo la Ruangwa baada ya kulitumikia jimbo hilo kwa miaka 15. Akizungumza na wajumbe wa kamati ya Siasa ya Mkoa na Wilaya ya Ruangwa Mheshimiwa Majaliwa ametumia fursa hiyo kuwashukuru wananchi kwa kumuunga mkono wakati wote ambao amekuwa mbunge wa jimbo hilo. "Imefika wakati kwa mshikamano tulioujenga  sasa ni wakati wa kutoa fursa kwa Wana-Ruangwa wengine wapenda maendeleo waweze kuunganisha nguvu hizi ili Kauli mbiu yetu ya Ruangwa kwa maendeleo inawezekana iweze kusonga mbele zaidi." Aidha, ametoa wito wajumbe wa kamati ya siasa ya Wilaya kuwapa ushirikiano wagombea wote wenye nia ya kugombea ubunge wa jimbo hilo. Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa amewasihi Wana-Ruangwa kuendelea kushikamana na itakapofika siku ya uchaguzi waweze kuchagua wagombea wote watakaowakilisha chama cha Mapinduzi kwenye uchaguzi huo.  "viongozi wetu Mheshimiwa Dkt. Samia Su...